Singo Batan
JF-Expert Member
- Apr 24, 2020
- 292
- 191
Ligi yetu ya NBC sasa inaonesha kuwa na ushindani mkubwa na malengo ya kufika mbali. Hii inachagizwa sana na jeuri na nguvu ya pesa kutoka kwa matajiri wetu wa Bongo.
Battle ya fedha sasa inaonekana kwenye soka, hii sio tu inaleta raha na ushabiki kindaki ndaki katika soka, pia imezidi kufungua fursa ya ajira kwa vijana. Tizama Familia ya Bakhresa na Azam FC yao, kule kutana na Familia ya Dewji na Simba yao, upande mwingine kina Gharib na Yanga yao.
Kuna hawa vijana wa Singida walioanza jina la DTB na sasa "Singida Big Bullets" (wenye nayo si mnawajua?).
Geita kwa wachimba dhahabu nako sio haba, pesa inaleta kiburi na ujeuri. Ni pesa tu kila mahali. Kutunishiana misuli kwa hawa madigala ndio kunafanya tujadili sana kuhusu soka. kunafanya tupate wachambuzi mahili na wale wa "Michongo". Pesa inawabadilishia "chawa" timu za kushabikia, si mnamkumbuka Steve kulia lia? na Yule Mtoto wa Mzee Sunday Manara .
Tufurahie vita ya pesa katika SOKA, na vikumbo kutoka kwa Big 3 giants GSM, BAKHRESA na Bwana MO DEWJI.
tupoteze stress za TOZO kidogo au sivyo😅😅.