Azam inamtaka Ibenge

Izy_Name

JF-Expert Member
Apr 9, 2020
647
1,295
Wakati Azam FC ikibakiza mechi tano kumaliza msimu wa Ligi Kuu Bara, tayari imeanza kimyakimya kutafuta kocha mpya atakayeiongoza msimu ujao ambao imepania kutwaa ubingwa huku kocha wa Al Hilal ya Sudan, Mkongomani Florent Ibenge akitajwa kutinga kikosini hapo ndani ya kipindi hiki cha mwisho wa msimu na mwanzo wa msimu ujao wa ligi kuu.


Azam ilianza msimu huu ikiwa na kocha Mmarekani mwenye asili ya Somalia Abdihamid Moalin, ikiwa na malengo ya kuchukua ubingwa ikafanya usajili mkubwa, lakini baadaye akaondoshwa kutokana na mwenendo mbaya na mikoba yake kuchukuliwa na Mfaransa Denis Lavagne.

Lavagne nae alifukuzwa na timu kubaki chini ya kocha wa makipa Mhispania Dani Cadena akishika majukumu ya kukinoa kikosi akisaidiwa na Kally Ongala na kocha mchezaji Aggrey Morris ambao uongozi upo kwenye mchakato wa kuwaletea kocha mkuu ambaye atakinoa kikosi hicho.

Hata hivyo Azam ina mpango wa kuboresha kikosi kizima kuanzia benchi la ufundi hadi wachezaji kupunguza madhaifu madogo madogo ikiwemo kuongeza wachezaji endapo watatakiwa na kocha ajae.

Taarifa kutoka ndani ya Azam zinaeleza, mabosi wana majina ya makocha wanne mezani akiwemo Ibenge ambao wanajadiliwa ili apatikane mmoja atakayetua Chamazi kabla ya msimu huu kumalizika ili akione kikosi kilichopo, apendekeze usajili na aende na timu kujiandaa na msimu kuhakikisha lengo la ubingwa linatimia.

Pia inasemekana kuwa, katika majina hayo hakuna kocha mzawa hata mmoja aliependekezwa katika orodha hiyo lakini moja ya majina ambayo matajiri hao wa Chamazi wanawaza kumwaga pesa ili kulipata nijina la Ibenge anayekinoa kikosi cha Al Hilal ya Sudan.

Inaelezwa mabosi wa juu wa Azam wanaamini wakimpata Ibenge ataibadili timu ndani ya muda mfupi kama alivyofanya Al Hilal na kufikia malengo na tayari wamemtumia ofa ambayo bado hajaijibu licha ya kuwepo na mawasiliano ya mara kwa mara baina ya pande zote mbili. Azam kwa sasa ipo nafasi ya nne kwenye msimamo na alama 47 nyuma ya vinara Yanga wenye 65, Simba (57) na Singida Big Stars (48) katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.

SOURCE AZAM INAMTAKA IBENGE
 
Mama kawabana wachumia tumbo wafanye fasta kutumia fursa.
 
Club kongwe zenye hekaheka mjini sijui lini zitapotea lini ziwapishe na wengine
Kule kwa madiba, Kizer Chiefs na Orlando Pirates zilipotea kumpisha Mamelod Sundowns.

Azam ana kila uwezo wa kufanya hivyo isipokuwa ana hujumiwa na rasilimali watu, ambapo kwa hapa Tz kila mtu either ni Simba Sc au Yanga.

Apunguze wazawa kwenye uongozi wa team kama jinsi ambavyo wenzake wamefanya kule South, kisha asajili Quality players wenye uchu wa mafanikio ya kucheza kimataifa.

Akifanya hivi mbona kitaeleweka tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom