Matajiri wa Moshi miaka ya 90 hadi 2000's

Matajiri wa Moshi miaka ya 90 hadi 2000's

Changbay inamilikiwa na mama mmoja hivi ambaye alianza kuwa maarufu kwa jina la “mama kuku”.

Basi lilotumbukia mto Karanga, lilikuwa likiitwa Safina! Kuna watu walitajirikia pale, maana wafanyabiashara enzi hizo walisafiri na kiasi kikubwa cha pesa kwenda kununua bidhaa kutoka Dar to Arusha na Moshi.

Mzee Mwariko sina uhakika kuhusu alipo kwa sasa, ila alikuwa na gallery maeneo ya Dar St kama sikosei ilikuwa ikiitwa Mwariko’s Art Gallery. Enzi hizo mzee Makassy akiwepo kama sikosei.
If you still in moshi nikija ntakutafuta
Hahaha mo town yerewiii
 
Ndo ungese wa maisha hakuna formula maalum. Kuwa tajiri ni kuamua tu. Kuna jamaa namfahamu aliamua kukwapua pesa akaenda kusoma ili awe professional serial killer. Na jamaa ni pro kwelikweli na analipwa vitita virefu na wanaomtuma kazi.
Hahahah wa moshi ama?
 
Opposite na benki ya mawenzi kulikua na kaduka ka mhindi anauza juice ya kutengenezea nyumbani. Mnamkumbuka? Nadhani jina lake 'bandia'. Alikuwa anavaa KAPTULA tu. Juisi chupa ndogo fupi. Juisi sijui zina spices gani zile za kihindi hindi ila tam sana. Hivi mzee bandia kuna aliemuona sk za karibuni?

Halaf mtaa huo huo kuna mhindi mwingine mwembamba anapenda kutoa meno nje nae toka miaka hiyo anavaa kaptula hadi leo!
Mhindi yule anaitwa bandia msemo wake maarufu ukienda kunywa juice anakwambia ""taka moto au taka baridii''
 
Mzee Sambeke alikuwa na watoto wa aina zote Babu alikuwa jambazi,Kaka yake upadri alianzia West Africa.Kulikuwa na story nyumbani kwake pale karanga kulikuwa na handaki eti gari likiingia linatoka limebadilishwa kila kitu
Hapo palikuwa ni kwa singasinga mmoja akiitwa mayuri.ndie alikuwa na gereji dizaini hiyo.
 
Aliandika maishapopote

Nimegundua watu wa aina niliyoitaja hapo Juu,Hawajulikani kabisa Hapa Dar es Salaam,sijajua sababu ila nadhani matajiri wa hapa Dar wanapata media Coverage nyingi na pia wanapata connection nyingi mno na Kuwa Mega kama sio Super Rich Kabisa au Maarufu kuliko wa mikoani.


Kwa kuwa wanaaminika na na kujulikana mno huwa wanawafunika wa Mikoani kwa Kila kitu,na hata hawa wa mikoani wakija Hapa Dar huwa wanakosa exposure na kujiamini kabisa.

Leo nawaleta kwenu watu Maarufu,Matajiri,Watoto wa Mjini,ambao wapo Mkoa wa Kilimanjaro hususani Moshi Mjini na Arusha,Naomba wadau wa Mikoa hii wanisaidie kujazia Nyama na Information na kutaja majina Mengine Ambayo yatasaidia kuwapa Exposure Wenzetu Hawa

Karibuni


1.Patrick Ngiloi Ulomi: Mfanyabiashara maarufu mno mikoa Hiyo anamiliki vituo vya Mafuta vya kutosha,Hotel za Kitalii za Kutosha,supermarket za kutosha, na Pia Anamiliki timu ya Mpira wa Miguu iliyoyoko Ligi Daraja la Kwanza Tanzania.
  • Anapendwa Mno
  • Anaheshimika Mno
  • Amesaidia Vijana wengi Ajira
kwa sasa Anaishi Moshi baada ya Kuhama Dar es Salaam

2.Laswai 🙁Trust Bureau de Change)
Huyu Ni Mfanyabiashara mwingine maarufu mno mkoani kilimanjaro,hayupo social sana ila anajulikana anamiliki hoteli kadhaa za kitalii ikiwemo Kibo Palace,pia akiwa kama Main Importer wa betri za Tiger,Utitiri wa bureau de change(mkumbuke Moshi na Arusha ni miji ya Kitalii)
na biashara nyingine nyingi.
  • Anaheshimika Mno
  • Multi Trade
Anaishi Moshi na Arusha.

3.Philemon Ndesamburo (Retired MP-CDM)
Need to say More?
  • Keys Hotel And Apartments( Moshi,Dar and Arusha)
  • Keys Hotel and apartments (London)
  • Keys Tours and Safaris-hapa Vehicles zote ni VX
  • Kilimanjaro Marathon Host and owner
4.Willy Lucas Tarimo-Snow Crest Original Owner
  • utitiri wa Vituo vya Mafuta
  • Hotel za Kitalii,ikiwemo snowcrest( ina Mgogoro)
  • and other Business.

5. Papa King-Mining
Owner of Triple A Investment.

Update:

6.Sunda: Mining and other Investment

7.Benson :Electronics Internet and Mobile Networks

7. Mrema: Impala Hotels,Ngurdoto Hotel,Naura Springs

8.Mathias Manga: Mining esp.Tanzanite

9.Willy Chambulo..aka Kaburu: Tourism and Hospitality ( Kibo Guides and Hotels)

10.Michael Ngaleku Shirima: Aviation ( Precision Air)

11.Pandit: Tanzanite

12.Kanunga;Tanzanite and Mining

13.Mbise: Hotels and Accomodation

14.Shidollya Tours;Tourism and Hospitality

15.Charles Makoi: Hotels and Hospitality

16.Alex Masawe (*******) tumweke au tumtoe

17.Mawalla Advocate; lawyers and Advocates

18.Gody : Tanzanite and Gemstone

19.Curthbert Swai: Ahsante Tours Moshi

20.Seif : cultural heritage( Vinyago na urembo)


naendelea kuzibadilisha kadri itakavyoonekana,inaonekana Makoi watu wanaona kashachoka,kuna kina Njake sijaona katajwa humu,list ikifika watu 100 wanaoeleweka tunaanza kuwapanga kwa number from baba lao,to upcoming Bilionairs.

Moshi naona mmezubaa wengi hapa ni matajiri wa arusha,siwaoni kina maleko,boisafi na wengineo nashindwa kuwachomeka maana sijui vizuri hali zao kwa sasa...pls update me






Karibuni

Mkuu vipi buni ramole mwenye osy grand

Na mwenye moshi view hotel

Au golden view hotel

Usisahau seven eleven
 
Mkuu vipi buni ramole mwenye osy grand

Na mwenye moshi view hotel

Au golden view hotel

Usisahau seven eleven
711 waliwahi kuihusisha na yule jamaa aliyewahi kuwa waziri kama sikosei. Bado ipo vyema tu na wapangaji.Sema kuna wakati ilikuwa ni floors kadhaa tu na hivyo bado inatakiwa kuendelezwa.

OSY Grand ya Buni Ramole bado ipo.

Hiyo Golden view ni ya kina Malya ambao ni ndugu na Babuu Sambeke(Nadhani Sambeke Malya ambaye ni baba yake Babu, na huyu mwenyeGolden view ni mtu na kaka yake).

Moshi view naikumbuka lakini imenitoka kidogo, labda unikumbushie maeneo.

btw Vincent Laswai mwenye Kibo Palace, anajenga na yeye hotel moja karibu kabisa na Osy Grand ya Buni Ramole. As we speak, nadhani ujenzi unaendelea kwa kasi.
 
Wakuu kuna bar ya seven up, tausi nazo za zamani kweli tangu niko mdogo nasoma jamhuri

Siku izi zimekuwa za kisasa kweli
Hayo maeneo yote sasa hivi ni lami tupu! Hapo Seven Up maeneo hayo pameendelezwa kiasi flani, ila miundo mbinu ndo poa.
 
Back
Top Bottom