Matajiri mara nyingi tunaamini masikini Ni wavivu lakini sio kweli

Naam,

Na kuna wengine wanarithi mambo genetically kabisa, mtu anakuwa na addictive personality, hata akishika hela kubwa ndiyo kwanza anakuwa mlevi wa pombe au madawa, pesa badala ya kumletea maendeleo, zinamuua. Kwa sababu genetically ana addictive personality ya kurithi.

Yani huyo bora awe masikini ndiyo anaweza kuishi muda mrefu, akiwa na hela ni majanga matupu.

Sasa huyu naye tusipomuelewa tunaweza kusema huyu jamaa lofa mlevi tu, kumbe ana matatizo ya kibaiolojia kwenye vinasaba hatujui tu.
Sahihi mkuu. Mchungaji anasema ni pepo njoo nikuombee. 😂
 
Ukiwa masikini navUkisha oa na kuanzisha familia na kuzaa watoto na uka play your role as responsible father or mother kunaitaji kujitoa sadaka Kwa familia yako..

Ndio maana hata ukiambiwa uende kuzamia ughaibuni ukifikiria familia uliyo ianzisha una ghairi
Kweli mkuu , hata ukiwa hauna familia responsible unakuwa MTU Wa tahadhari Sana hata gari Unaendesha Kwa ustaharabu maana unajua huku nyuma kuna watu wanakutegema ili maisha yaende.


Hivyo I agree with you mkuu.
 
Kwema jamani!
Mara nyingi watu tukiwa na umwezo huwa tunaimani kwamba masikini walio wengi ni wavivu .

Nimejaribu kufuatilia kiundani nimegundua Hawa jamaa wanapambana usiku na mchana but Neema ya Mungu haipo upande wao kwa Sasa.

Hivyo ukiwa juu jitahidi kumuomba Mungu akupe Neema ya kuendelea kuwa imara kiuchumi pia karibu kuwashika mikono waliochini ambao unadhani wanauelekeo halisi wa mapambano ya kiuchumi.
Kama Mungu wako anabagua simtaki
 
Kwema jamani!
Mara nyingi watu tukiwa na umwezo huwa tunaimani kwamba masikini walio wengi ni wavivu .

Nimejaribu kufuatilia kiundani nimegundua Hawa jamaa wanapambana usiku na mchana but Neema ya Mungu haipo upande wao kwa Sasa.

Hivyo ukiwa juu jitahidi kumuomba Mungu akupe Neema ya kuendelea kuwa imara kiuchumi pia karibu kuwashika mikono waliochini ambao unadhani wanauelekeo halisi wa mapambano ya kiuchumi.
Yote kwa yote masikini wenzangu tuache uvivu tupambane, kama tunapambana na hatupati basi tuongeze juhudi na maarifa na kuendelea kupambana zaidi.

Uvivu upo, na mara nyingi hatuna focus tunawajibika sana hasa kwa kujaribu kila kitu hatuwezi kukomaa na jambo moja, malengo yetu huwa hayazidi mwaka na kutimiza huwa ni kazi.

Msitutetee ili tujione na sisi tuna jambo, mna haki ya kutusema na sisi tutabadilika taratibu taratibu, ingawa yaweza isiwe kama nyinyi matajiri.

Oya we, maskini tupige kazi!
 
Kweli mkuu , hata ukiwa hauna familia responsible unakuwa MTU Wa tahadhari Sana hata gari Unaendesha Kwa ustaharabu maana unajua huku nyuma kuna watu wanakutegema ili maisha yaende.


Hivyo I agree with you mkuu.
Much appreciation sanaaa kwako mkuu 😊😊😊😊🤓😊
 
ila tajiri Mimi sikupingi hata!! but naomba unisaidie mtaji Mimi kijana mpambanaji 300k, only naenda kutoboa
 
Hoja nzuri sana. Binafsi nimekuwa nikiifikiria sana.

Kitu muhimu kuelewa ni kwamba, katika maisha, mambo mengi hayako katika ndiyo/hapana, off/on, mambo mengi yapo katika spectrum, mchanganyiko, probability, percentage.

Kwa hivyo, swali zima la "umasikini wa masikini unasababishwa na uvivu, kweli/si kweli?" lina makosa ya kufikiri kwenye hizo absolute terms za false dichotomy ya ndiyo/hapana.

Suala muhimu zaidi ni, asilimia ngapi ya umasikini inasababishwa na uvivu? Kuna probability gani ya mtu kuwa masikini akizaliwa Tanzania?

Kwa sababu, mtu mwingine anapozaliwa tu tayari kashashinda bahati nasibu ya kuuaga umasikini.

Unaweza kumsifia Mo Dewji kwamba amekuwa si masikini kwa sababu yeye si mvivu kweli?

Sawa, inawezekana Mo Dewji si mvivu, kajiongeza sana, kapiga shule mpaka Georgetown, kajifunza biashara za familia.

Lakini, angalau yeye kakuta familia ina biashara kubwa tayari. Angalau yeye kakuta familia inaweza kumpeleka Georgetown University tayari. Hivyo kuna mambo mengi kapata kwa urahisi.

Kuna watu wengi sana wana ari ya kazi kama ya Mo Dewji, na pengine kumzidi, lakini wameishia kwenye umasikini kwa kukosa support system, kwa kukosa bahati ya kuzaliwa na wazazi matajiri, kwa kukosa kujuana na watu wenye kuweza kuwapa mikopo na mentorship.

Ukimuangalia Aliko Dangote naye ni hivyo hivyo. Kwao kulikuwa na biashara kubwa zamani sana.

Sasa, watu kama hawa, hata wakifanya jitihada binafsi kidogo tu, mtandao wao wa kifamilia unawainua sana tu.

Na kuna wengine wa daraja la kajambanani, hata wakijiongeza saaana kwa kupigania maisha, ile kukosa mtandao mzuri wa kuwasaidia tu kunawaangusha sana.

Kwa hivyo, tukiangalia spectrum ya asilimia ngapi ya umasikini au utajiri wa mtu inatokana na juhudi binafsi, tunaweza kukuta hata kama juhudi binafsi ipo, sehemu kubwa inabebwa na bahati ya kuzaliwa na wazazi matajiri, kuwa na network nzuri, na pengine bahati tu ya kuwa sehemu nzuri, wakati mzuri. Kuna sababu nchi kama Marekani ina mabilionea wa US dollars wengi sana kulinganisha na Tanzania.

Sikubaliani na Andrew Tate kwenye mambo mengi sana. Lakini, alisema kitu kimoja nakubaliana naye.

Alisema kwamba, ukiwa mtu masikini uliyezaliwa Tanzania, naweza kuelewa kwa nini wewe ni masikini, lakini ukiwa umezaliwa Marekani, ukawa mtu masikini, basi hapo umejitakia mwenyewe.

Andrew Tate is a dickhead, lakini hapa namuelewa. Alimaanisha ile bahati tu ya kuzaliwa Marekani tayari umeshashinda bahati nasibu ya kuongeza nafasi za kuwa tajiri kulinganisha na mtu anayezaliwa Tanzania.

Wewe unafikiri Bill Gates angezaliwa Tanzania angekuwa bilionea wa dunia? Kwani Tanzania siku aliyozaliwa Bill Gates hakukuwa na watu wenye uwezo wa kiasili kama wa Bill Gates waliozaliwa siku hiyo?

Wako wapi sasa?

Kwa hivyo, mara nyingi tunaangalia sana juhudi binafsi za mtu, kuliko kuangalia sehemu ya bahati.

Inabidi tuangalie sababu kama spectrum, kama percentage, kama probability, si absolutes za yes or no.
Hii ndio ilitakiwa iwe thread na thread iwe comment tu.
 
Kila mtu anapambana mkuu, ila kupambana kwa masikini kunaweza kuonekana kirahisi.

Matajiri wanapambana ndani ya ofisi zenye viyoyozi, wanapambana na madeni yao, wanapambana na TRA kukwepa kodi, wanapambana na kesi zao wanasheria wao wanajua, wanapambana kuongeza biashara zao maana pesa hata zikiwa nyingi biashara zinatakiwa kuongezeka tu, wanapambana kulinda walichopata wasipokonywe, wanapambana kutafuta wateja, unakumbuka Mengi alivyopambana na matajiri wa kihindi mpaka akasema wanataka kumuua? Wanapambana kuacha legacy.

Bakhressa na utajiri wake wote bado anapambana kujenga viwanda Malawi sasa hivi. Anaongeza biashara.

Maisha ni kupambana. Sema kuna wengine mapambano yao yanaonekana kirahisi zaidi.
We jamaa nakupa nyota tatu za jeshi la marekani .

Maana hili jambo nililitafakari juzi watu huwa wanasema matajiri hawana sleepless nights Ila hawajui tu Kuwa sleepless nights inakuwa kubwa kutokana na hiyo situation ya kodi, kulinda ulichonacho na kulipa wafanyakazi n.k compare to watu ambao wapo broke.
 
Kwema jamani!
Mara nyingi watu tukiwa na umwezo huwa tunaimani kwamba masikini walio wengi ni wavivu .

Nimejaribu kufuatilia kiundani nimegundua Hawa jamaa wanapambana usiku na mchana but Neema ya Mungu haipo upande wao kwa Sasa.

Hivyo ukiwa juu jitahidi kumuomba Mungu akupe Neema ya kuendelea kuwa imara kiuchumi pia karibu kuwashika mikono waliochini ambao unadhani wanauelekeo halisi wa mapambano ya kiuchumi.


"Matajiri mara nyingi tunaamini"

When you vocally claim, you are not!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom