Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania ilihitaji Dikiteta, tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,179
Wanabodi,

Angalizo. Neno dikiteta sio neno baya kama lengo la matumizi yake ni lengo jema. Tukisema Rais Magufuli ni dikiteta, hatumaanishi ni dikiteta katili kama Hitler, Musolini, au Iddi Amini, no way, Magufuli ni dikiteta mwema au dikiteta mzalendo anayeitwa a Benovelent Dictator!, kama Seretse Khama wa Botswana, Tito wa Yugoslavia, Lee Kuan Yew wa Singapore, Mustafa Kemal wa Uturuki and the like, hawa wote walitawala kwa mkono wa chuma na kuleta mapinduzi makubwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi kwa nchi zao, kwa kuzibadili toka kwenye umasikini, hadi kugeuka kuwa ni nchi tajiri, hivyo Tanzania pia sio nchi masikini, tuko kwenye umasikini huu kwa sababu tulikosa mtu imara wa kutuongoza, hivyo hapa tulipofika, ili Tanzania tutoke kwenye umasikini huu, tunamuhitaji mtu kama huyu Magufuli ili mambo yaende!.

Siku zote Watanzania tumekuwa tukilia kuhusu utajiri mkubwa wa rasilimali na maliasili za nchi yetu tulizobarikiwa nazo, huku wajanja wakija na kujiokotea na kujivunia Rasilimali zetu kama shamba la bibi, huku nchi yetu kuendelea kuwa ni nchi masikini huku Watanzania tukiishi kwenye lindi la umasikini uliotopea hivyo tukamlilia Mungu atupatie mkombozi wa kutuokoa na kuliokoa taifa letu.

Hatimaye Mungu kasikia kilio chetu akatupatia mkombozi, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kuja kutukomboa na kulikomboa taifa letu Tanzania, kutoka kwenye lindi hili la umasikini uliotopea na kuligeuza taifa letu kuwa nchi ya neema, Tanzania ya viwanda, Tanzania tajiri, a donor country, nchi ya ahadi, mabomba nchi nzima yatatoa maziwa na asali.

Kwa vile muasisi wa taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, aliwahi kutoa unabii kuhusu udikiteta Tanzania, na inawezekana, ujio wa Magufuli ni kutimia kwa maneno ya unabii huu, lakini kitu ambacho Mwalimu hakikujua wakati akitoa unabii huo ni kuwa hakujua Tanzania tutafikia mahali, tukamuhitaji kiongozi dikiteta!.

Kwanza watu wengi hawakujua ya kuwa Magufuli anaweza kuja kuwa rais wetu wa awamu ya tano, akina sisi, mimi nikiwa ni mmoja wapo, hili tuliliona tangu mwezi August mwaka 2014 na tukalisema humu japo watu hawakulitilia maanani lakini limekuja kutokea, Magufuli sasa ndio rais wetu!. Hata baada ya Magufuli kuwa rais, bado kuna baadhi ya wenzetu wanaamini Magufuli amekuwa rais wetu kwa bahati tuu!, sisi waumini wa everything happens for a reason, tunaamini kunayo sababu kwa nini ni Magufuli, na nimeieleza humu!.Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 ni John Pombe Magufuli!.

Mchakato wa kumtafuta mgombea kupitia CCM ulipoanza, nikawachambua wagombea wote wa CCM, na miongoni mwa vigezo vyangu, hili la udikiteta pia nililisemea!.
Yajue Makundi 10 Top Ten wa CCM, Ambamo Watatoa Top 5, Top 3 na kumtoa Rais wa 5 wa Tanzania!.

Baada ya kuchaguli kwa Magufuli kuhusu udikiteta wake nilisema hivi.
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki
.

Kwenye suala la Zanzibar, mara kibao tumewauliza CUF kwa nini wanapiga tuu kelele bila kuchukua hatua?!.
Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchuku hatua!.
CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima .
Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar?.


Kuhusu kususa kwa CUF kushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar, nilisema CUF wasitake kutisha watu kuhusu amani na utulivu wa Zanzibar, kwa sababu Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT, hivyo amani na utulivu wa visiwa hivyo, sio jukumu la Wanzanzibari wenyewe tuu pekee yao, bali ni jukumu la JMT na mwenye dhamana ya amani na utulivu wa nchi hii ni Amiri Jeshi Mkuu, wa vikosi vya ulinzi na usalama wa nchi hii. Jana ameonya mtu yoyote atakayeleta fyoko fyoko atashikishwa adabu!. Hivyo CUF mshiriki uchaguzi wa marudio au msishiriki, uamuzi ni wenu, tunachotaka sisi ni heshima, adabu, amani
na utulivu, vinginevyo mtaisoma hii namba!.

Magufuli na Mapinduzi ya Uchumi wa Tanzania.
Kama nilivyosema mwanzo, Tanzania sio masikini bali ni tajiri sana, ndio maana imekuwa ikifanywa ni shamba la bibi, baada ya kumpata Magufuli, ameonyesha nia ya dhati kwa kauli na matendo, anataka kujenga Tanzania ya Viwanda, Tanzania ya uchumi wa gesi, Tanzania kuwa ni nchi ya uchumi wa kati. Kuyatekeleza yote haya sio kazi ya lele mama, ni kazi ya shuruba, na by nature Watanzania ni wavivu, tumezoea kubembelezwa, hivyo sasa kwa Magufuli, hakuna kubembelezana!, sasa hapa ni kazi tuu!.


Katika kutimiza majukumu haya ya sasa ni kazi tuu, lazima kuna watu wataumia, wale wavivu wavivu wenzangu na miye tuliozoea kupiga deal, sasa hakuna tena dili na tenders za dili dili, sasa ni kuchapa tuu kazi hata ikibidi kwa mijeledi. Ndivyo walivyofanya kina Seretse Khama wa Botswana, Tito wa Yugoslavia, Lee Kuan Yew wa Singapore, Mustafa Kemal wa Uturuki, hawa wote walitawala kwa mkono wa chuma kuzikomboa nchi zao toka umasikini na kuzigeuza tajiri.

Hivyo sasa Magufuli ataigeuza Tanzania kuwa Doner Country but only if kama atapatiwa muda wa kutosha. Kipindi cha miaka 10 haitoshi, kujenga Tanzania ya viwanda, kuroll out SGR nchi nzima, kukamilisha miradi yote ya kimkakati na kuifanya Tanzania iwe ni nchi ya uchumi wa kati, minimum ni angalau miaka 20!.
Hitimisho.
Iwe ni kweli Magufuli ni dikiteta, au sio dikiteta, hoja ya msingi ni Tanzania mahali tulipofikia, ili kuondoka hapa kwenda kule tunakopaswa kuwapo, tulihitaji mtu kama Magufuli, watu tukasali kwa kumuomba Mungu atupatie kiongozi bora, kiongozi imara, kiongozi shujaa, hatimaye Mungu akaisikia sala yetu, akakisikia kilio chetu, ndipo akatutumia mkombozi kwa kutupatia Magufuli.

Maadam sasa mkombozi tumempata, whatever the names, be it or not, twende naye ili tufike kule tunakotakiwa kufika, na safari nyingine ni ngumu, kuna wengine wataishia njiani, na kuna wengine watafika wakiwa hoi bin taabani, wengine watafika wakiwa majeruhi, maadam dereva bingwa tumempata, sasa ni safari tuu, mbele kwa mbele, mwendo mdundo mpaka tufike safari yetu, the bottom line ni kufika safari yetu salama ya Tanzania tajiri, Tanzania donor country, Tanzania ya viwanda, wasiwasi wangu ni muda tuu wa miaka kumi hautoshi, kama ni kweli Tanzania tumedhamiria kuleta mapinduzi ya kweli ya nchi ya uchumi wa kati, kuna ubaya Magufuli akipewa extension of time asiruhusiwe kuondoka hadi atimize malengo yake ya kuifanya Tanzania a donor country?.

Jumapili Njema.

Paskali
 
Ukweli utabaki kua kweli na iko siku atakua ukweli hawezi kuingilia ya Zanzibar ataingilia ya Burundi Congo tusubiri tutaona dunia itamuangalia tu mwache apeleke majeshi akaue watu wasio na hatia atakuja jua baadae viongozi asokua na hikima wala busara alicho ongea kimeeleweka
 
Siasa ni mchezo mchafu sana,nahisi Lowassa ndio analitambua hilo sasa. Hata wewe Pasco?

Hukumsikia Gwajima? Huyu ndo alikua akileta nyuzi ooh JK muombe radhi lowassa huku akiweka picha za mafuriko kuhakikishia watu Lowassa ndiye Rais ajaye....

Usishangazwe sana hao ndio wabongo!!! Akili zao ni nyepesi mno kuwa influenced na vitu vidogo kiasi cha kusaliti misimamo yao....
 
TATIZO LAO PASCO HUWA SIKUELEWI KWANI MARA UEGEMEE KWA LOWASA MARA USEME HIVI SASA SIJUI MISIMAMO YAKO NI IPI?
Kuna watu wa aina tatu, wanaojielewa, wasio jielewa, na wapo wapo tuu, kwenye kujielewa hawapo, kwenye kutokujielewa hawapo, wao wapo wapo tuu!.

Wanaojielewa!. Hawa ni watu wakweli daima. Walikuwa na Lowassa wakati wa uchaguzi. Uchaguzi umekwisha, aliyetangazwa mshindi ni Magufuli, haijalishi kama ameshinda kihalali, kwa mbinu chafu, au bao la mkono, ila the end justify the means, Magufuli ndie rais wetu kwa sasa na this is a fact, ndio ukweli halisi, Magufuli ndie rais wa waliomchagua, ndie rais wa wasio mchagua na ndio rais wa wote hata ambao hawakupiga kura!. Magufuli ndie rais wa Lowassa, ndio rais wa Chadema ndie rais wa nchi, hivyo wakweli wote hili wanalielewa hata Lowassa mwenyewe anaelewa Magufuli ndie rais wake!.

Kama na wewe ni mtu unaejielewa utanielewa, kama uko kundi la wasio jielewa hutanielewa na ukiwa ni kundi la wale ambao wapo wapo tuu, kwenye thread zangu utaona giza tupu!.

Pasco
 
Hatuhitaji kiongozi dikteta bali tunahitaji mfumo wa kidikteta! Kwa mujibu wa katiba yetu, the maximum time rais kuwa madarakani ni miaka 10 sasa hata ukiwa na huyo kiongozi "dikteta" ina maana baada ya miaka 10 atakuja mwingine ambae anaweza kuwa tofauti na kurudi kwenye business as usual. Tunahitaji mfumo imara unaoweza kum-shape yeyote! Ikiwa tunaamini kiongozi mzuri ndo huyo dikteta, basi tunakuwa na mfumo ambao hata akiingia mtu kama Mwinyi mfumo unambadilisha manake inakuwa sio choice tena bali ndo ada yenyewe kutokana na mfumo wetu!
 
Magufuli si dictactor hapo uko wrong!! Aliyoyasema Jana kiongozi yeyote Wa nchi ni kawaida sana kuyasema!!!!

Hata JK aliwatisha waliojiandaa kulinda kura!!

Kusema ni jambo moja kutenda ni jambo lingine!!!

Madikteka huwa hawaogopi yeyote na wala hawana lugha za Mungu sijui mtuombee....

Magufuli ni mtiifu kupitiliza kwa Mkapa na hata msimamo Wa ZNZ anakokotwà na Mkapa!!

Dikteta hakokotwi!!!
 
Ukweli utabaki kua kweli na iko siku atakua ukweli hawezi kuingilia ya Zanzibar ataingilia ya Burundi Congo tusubiri tutaona dunia itamuangalia tu mwache apeleke majeshi akaue watu wasio na hatia atakuja jua baadae viongozi asokua na hikima wala busara alicho ongea kimeeleweka

Acha kuandika pumba kwani nini Majeshi yetu yakaue watu wasio kuwa na hatia?

Vyombo vyetu vya usalama viko kwa ajili ya kulinda usalama wetu hivyo yoyte yule atakayedhurika ni kwamba hakutii Sheria za nchi yetu ni rahisi kihivyo tu, ikitokea kweli kwamba kuna mtu hatii sheria basi ni lazima vyombo vitamshughulikia lkn ukiwa raia mwema hakuna wa kukugusa!
 
Ukweli utabaki kua kweli na iko siku atakua ukweli hawezi kuingilia ya Zanzibar ataingilia ya Burundi Congo tusubiri tutaona dunia itamuangalia tu mwache apeleke majeshi akaue watu wasio na hatia atakuja jua baadae viongozi asokua na hikima wala busara alicho ongea kimeeleweka
Magufuli atapeleka majeshi Zanzibar kwenda kusimamia amani na utulivu, ikitokea majeshi yakaua mtu, itakuwa mtu huyo ameleta fyoko fyoko!. Mtu akileta fyoko fyoko atashughulikiwa kikamilifu.

Ikitokea wengine wasi na hatia wakadhurika katika kututuliza hizo fyoko fyoko, then aliyesababisha madhara hayo ni muanzisha wa fyoko fyoko na sio mtulizaji au mdhibiti wa fyoko fyoko!.

Dawa ni moja tuu kwa Wanzanzibar, baada ya kumsikia Amiri Jeshi Mkuu akiwaonya msilete fyoko fyoko, hili sio ombi ni amri, hivyo msilete fyoko fyoko!.

Pasco
 
Kila jamii inatafsiri udikteta kwa namna yake. China, Singapore, Malaysia, Viewa ni Vietnam, Korea Kusini/Kaskazini, Urusi nk nk zote zinaongozwa kwa udikteta wa aina yake. Kubwa ni kuleta maendeleo yenye manufaa na tija kwa watu wake. Raisi wetu anaonyesha njia iliyochelewa kuonekana zaidi ya miaka 20; tumuunge mkono.
 
Hapa ndio naposhindwa kuelewa na niseme wazi labda itanichukua miaka mia kuelewa ZANZIBAR SIO NCHI NI SEHEMU YA JAMUHURI PASCO ,naomba unijibu swali langu katiba tuliyo nayo imeweka hayo maswala ya usalama kwenye Muungano ,ila mambo mengine kama ya ZEC hayapo kwenye Muungano ,kulikua na tatizo gani wa Zanzibar kudai haki yao kama nchi kamili?

Ikiwa wanaona haki yao ya kufanya maamuzi imechukuliwa na bara ? Kwanini Warioba na Wananchi wengi waliona serikali tatu ni suluhisho la matatizo ya Muungano? Na kwa kauli hiyo Wanzanzibar si watanendelea kuona Tanganyika imewakalia kimabavu ,kwamba baba kama mzazi kwa mtoto wa kambo jukumu lake ni kumridhisha mama wa mtoto kimapenzi ila sio kumsomesha huyo mtoto ,huoni hilo ni tatizo?

Kilicho kufanya uandike tunachotaka sisi ni adabu ,heshima ,amani na utulivu ni nini? sisi ni kina nani ??? Kudai haki kama unaona umedhulumiwa ni kukosa adabu na heshima?

Au kauli hiyo umetoa baada ya kuskia Manyerere Jacton kasifiwa unataka usafirie nyota yake?

NB Nyerere alishaona hili na akasema kwa katiba tuliyo inaweza kumfanya mtu kuwa dikteta wa ajabu, kwanini tuendelee kuing'ania katiba hii ambayo hata walio itengeneza wametoa angalizo zao?

Kama Zanzibar ni nchi kama Magufuli alivyosema hawezi kuingilia tume ya uchaguzi ya nchi nyingine ,kulikua na sababu gani ya nchi kutambulika kama nchi kwa maneno ila haina majeshi yake ya ulinzi na usalama?
 
Magufuli atapeleka majeshi Zanzibar kwenda kusimamia amani na utulivu, ikitokea majeshi yakaua mtu, itakuwa mtu huyo ameleta fyoko fyoko!. Mtu akileta fyoko fyoko atashughulikiwa kikamilifu...
Ikitokea majeshi yakaua mtu ,mtu atakua ameleta fyokofyoko ?? Yaani majeshi ya wananchi wa Tanzania yakatumike kuua watu wake ambao sio wanajeshi halafu hapa unatetea udikteta fyongo kwamba Magufuli sio dikteta, nini maana ya utawala wa sheria?

Kuna tofauti ya kuwa Mkali na kuwa dikteta tofautisha hilo na kwa hali nchi ilipofikia hakika inahitaji kiongozi mkali ila pia anayefuata sheria au la afute utawala wa sheria aongoze nchi kidikteta
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom