Masibayi
Member
- Jan 2, 2018
- 19
- 65
Rejea katika historia
Hii ni kinyume kidogo Na utaratibu tuliozoea kusikia au kushauriwa na wataalamu Wa kiuchumi au wahamasishaji,motivational speakers. Dhana ya kuweka akiba imekuwa ikielezwa katika misingi ya vitu mbalimbali Na ikipata mashiko kutoka kwenye biblia Na vitabu vingine.Ingawa kuna aina nyingi za akiba kutoka kwenye mazao mpaka nguo,mafuta, bidhaa n.k ila makala hii inajikita zaidi katika akiba ya fedha.
Zipo kanuni mbalimbali zinazotawala nguvu ya pesa ambazo zinabadilika kutoka kizazi hadi kizazi. Mfano; kanuni iliyotawala fedha kipindi cha zama za viwanda (industrial age) ni tofauti na kanuni inayotawala pesa kipindi cha zama za taarifa (information age). Nyakati za mapinduzi ya viwanda pesa ilikuwa ni kitu halisi na kilipewa nguvu kwa kutumia dhahabu. Zama za leo pesa si kitu halisi,ndo maana inaitwa "currency"; kwa maana ya kitu kinachomiminika kama maji na ndo maana serikali zinaweza kuchapisha noti mpya au la kwa kuzingatia mambo fulani fulani.
Mchwa wanaotafuna akiba ya pesa
Maamuzi ya uwekaji akiba wa pesa ni mithili ya mbwa aliyeficha mfupa kwa kuuchimbia ardhini. Huko kuna wadudu wanaoanza kuushambulia mara baada ya kuwa ameufukia. Baadhi ya mchwa wanaoshambulia pesa ni hawa wafuatao; kodi,tozo za benki,mfumko wa bei. Tutaangazia mchwa hawa kwa kisio kwamba mtu kaweka akiba ya pesa benki.
- Mfumko wa bei: Huu ni ule unaotokana na uchapaji wa pesa kwa wingi na kupelekea pesa kufurika kwenye mzunguko. Ni mbali na ule utokanao na uhaba wa bidhaa. Haijalishi pesa umeiweka benki au chini ya godoro lazima iathiriwe na mchwa hawa. Ni kodi ya kimya kimya ambayo hakuna anayeweza kuikwepa kuanzia tajiri mpaka masikini. Mfumko wa bei unasababisha kushuka kwa uwezo wa pesa kununua bidhaa. Kwa lugha rahisi ni kwamba bidhaa ambazo noti ya shilingi 1000 inaweza nunua leo ni nyingi ukilinganisha na bidhaa ambazo inaweza kununua baada ya miaka 10. Haijalishi umeweka akiba wapi,ila ujue wazi thamani ya pesa yako itapungua kutokana na mfumko wa bei.
- Kodi; Kanuni ya benki juu ya uwekaji wa akiba inaruhusu kulipa kodi katika viwango vya mapato,income tax cap rates. Kwa hiyo kama uliweka akiba kwa riba ya asilimia 5 kwa mwezi basi utakapokuja kuchukua pesa yako utatozwa kodi barabara na nanuni ya tozo la kipato. Kwa hiyo ukiachia mbali inflation bado kuna kodi ya serikali,PAYE( pay as you earn), ambayo itaitafuna hela yako.
- Tozo za benki; Hii ni gharama za utunzaji wa pesa kwenye akaunti benki.
Baada ya kuona mchwa hao unakuja kuona kwamba kuliko kuweka akiba ya pesa ni bora kuwekeza. Swali ni kwamba unawekeza kwa staili gani?
Ikiwa umeona kuna kodi,tozo na mfumko wa bei basi ni muhimu kuwekeza katika fursa ambazo zinafidia punguzo kinalotokana na mchwa hao.
Kwa hiyo tunaweza kusema kuwa kanuni ya pesa katika zama za taarifa ni kuwekeza na siyo kuitunza kama akiba.
Aina za uwekezaji
Kuna kuwekeza kwa staili nyingi sana. Baadhi ya aina hizo ni hizi hapa chini;
- Uwekezaji kwa ajili ya ongezeko la mtaji; Hii ni pale mtu anapoamua kununua bidhaa au kitu kwa gharama ndogo na kuuza kwa gharama kubwa. Faida anayoipata ndio inaitwa ongezeko la mtaji,capital gain.
- Uwekezaji kwa ajili ya mtiririko wa pesa; Hii ni pale mtu ananunua assets ambazo zinakuwa zinampatia fedha mara kwa mara,(Investing for cashflow).Kwa mfano nyumba ya kupangisha. Hii ni mali ambayo inakupa pesa kila mwezi kwa kukusanya pango. Haijalishi kuna mfumko au mdololo wa bei.
- Uwekezaji kwa ajili ya misamaha ya kodi(tax incentives); Huu ni uwekezaji katika miradi yenye misamaha ya kodi, miradi ambayo ni kipaumbele kwa serikali. Kwa mfano; miradi ya makazi, kilimo na ufugaji sanjari na uchimbaji wa madini. Aina hii ya uwekezaji huisaidia serikali kutoa huduma ambazo ilitakiwa kuzitoa. Kwa lugha rahisi ni uwekezaji unaoisaidia serikali kutekeleza majukumu yake kama vile utoaji wa ajira. Miradi hii hupata misamaha ya kodi.
Ushauri wangu
Badala ya kuweka hela benki,wekeza kwenye biashara au miradi ambayo itafidia thamani ya pesa yako kwa baadae kwa kuzingatia misamaha ya kodi na mfumko wa bei unaosababishwa na kuwepo kwa fedha nyingi kwenye mzunguko.
Kwa mfano; ukinunua nyumba kaa ajili ya kupangisha utapata ongezeko la mtaji kutokana na kupanda kwa thamani ya eneo, thamani ya nyumba na pia utapata mtiririko wa pesa wa kudumu kutokana na ukusanyaji wa pango.
Ikitokea soko la nyumba limedolola bado utaendelea kupata pesa za pango maana makazi ni hitaji la kila siku. Pia mapato ya pango kwa sasa hayatozwi kodi na serikali. Haijalishi kuna mdololo wa uchumi,kuna mdololo wa thamani ya pesa au la. Bado unauhakika wa kupata kipato.
Kumbuka,matajiri hawaweki akiba ya pesa benki. Wanawekeza kwenye mzunguko wa pesa. Tumia kanuni hii kunufaika na pesa yako.
Asante sana!