Daima maji hufuata mkondo,ndio maana uchaguzi wenye RUSHWA huzaa Serikali ya wala RUSHWA,CCM isiyoshinda kihalali inakosa BARAKA ZA MOLA WETU.MUNGU ni MTAKATIFU na hivyo hawezi kuibariki serikali inayoiba na kutembea kifua mbele ikijisifia kwa wizi iliyoufanya,ndio maana CCM imejaza wezi watupu,ambao hawataki kufanya kazi na hivyo kuelekeza nchi kuwa ombaomba,mpaka mataifa ya wenzetu yanatushangaa na rasilimali zote tulizonazo,Rais mzururaji ameamua kuwa Vasco da Gama,sindibad the sailor.Wenzetu wanatoza wananchi wao kodi kutufadhili sisi,kibaya zaidi baadhi ya mawaziri kama akina Pombe Magufuli wanasema eti mwacheni Rais azulule atutafutie fedha kumbuka hayo maneno yanatoka kwenye mdomo wa Doctor sasa jiulize kuna Elimu kwenye kichwa cha namna hiyo kama sio upumbavu na janga kwa Taifa.Tukumbuke kwamba kuombaomba na kutegemea misaada ni UTUMWA na FEDHEHA KWA TAIFA.Wengine kama akina Andrew Chenge na Willam Ngeleja kila dili wamo nadhani hata mshipa wa AIBU Ulishakufa wanataka hadi vitukuu vijue kuwa wao ni wezi konkodi.MAWAZIRI wengine wanaoitwa maprofesa wanasema eti watanzania wanaweza kuwekeza kwenye juisi peke yake na siyo gesi,anatamka hivyo baada ya kulewa madaraka na kujisahau kwamba anatumikia ofisi ya UMMA na UMMA ndio uliomtuma kazi anayofanya kama waziri wa nishati na madini na si kutoa matusi kwa watanzania.Kumbe watanzania tusishangae haya yanayoendelea na matunda ya namna serikali ilivyopatikana.Wengine wakajiita maspika wa standard and speed kumbe ni vichaa tu,walishachanganyikiwa zamani.Tunaisihi CCM na serikali yake isichezee AKILI ZA WATU WENYE MAARIFA.Ndugu zangu watanzania tujifunze hasa tunapokuwa kwenye OFISI ZA UMMA kuwatumikia watanzania wenzetu maskini na kuacha majigambo,majivuno,dharau,kejeli,matusi ili kuwatumikia watanzania kwa upendo mkuu bila kujali rangi,kabila wala dini ya mtu.