Maoni ya Mwanakijiji juu ya Escrow baada ya wahusika kukamatwa

Jc Simba

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
302
500
Mojawapo ya mada ambazo zijawahi kuzitolea maoni ya kina ni sakata zima la escrow. Tangu kuibuliwa kwa kashfa hii sikutaka kutoa maoni ya ndani zaidi ya mawazo yangu. Sikufanya hivyo kwa sababu kubwa mbili, kwanza ni mojawapo ya kashfa za kipumbavu kabisa (foolish) ambazo zimewahi kutokea nchini. Ukilinganisha na ile ya fedha za EPA hii ya escrow ilikuwa ni rahisi sana kuonekana ufisadi wake kwani ilikuwa wazi kwa mtu yeyote yule anayefuatilia. Pili, kashfa hii ilionesha tu jinsi gani tuligoma kujifunza kutoka kashfa nyingine zilizopita. Nimewahi kuandika mwaka 2009 mada ya TEMPLATE OF CORRUPTION.

Katika mada hiyo nilidokeza tu jinsi gani mafisadi wa ndani wanafanya kazi kushirikiana na mafisadi wa nje na with some minor modifications wanatumia njia zile zile kuliibia taifa. Hii ya escrow haikuwa tofauti.

Sote tunajua kina nani walipewa fedha za escrow kwa mtindo wa kuchoteana kidogokidogo. Bahati mbaya wengi walichukulia zoezi lile hasa kuwan ni utakatishaji fedha (money laundering). Katika utakatishaji huu mtu anachukua fedha kwa njia haramu halafu anajaribu kuzibadilisha na kuziingiza kuzifanya ziwe halali; yaani fedha chafu zinasafishwa ili ziwe safi. Mtu anaweza kwenda kujengea nyumba, kuanzishia biashara, kutoa msaada mahali, kusomesha watoto, kutengeneza ajira n.k mwisho wa siku watu watashukuru kwani jamaa badala ya kuzila fedha amezitumia vizuri kwenye jamii.

Kama nilivyosema jana usicheze kamari dhidi ya Magufuli (don't bet against Magufuli) naomba kurudia leo kuwa wale wote waliochukua na kula fedha za EPA wakiamini kuwa wameweza ku 'get away with it' huu kwao ni muda wa kujitafakari haraka. Wasije wakadhania au kuamini kuwa nyavu hii iliyorushwa itawakwepa. Wasije wakajifungia ndani na kuomba kwa miungu yao kuwa 'kikombe hiki kiwaepuke'. Sala zao hazitajibiwa.

Waamue kwa hiari yao wenyewe wazirudishe fedha hizo kabla hawajapewa nafasi ya kuzirudisha zote na adhabu juu (with penalty). Naamini - na nina sababu nzuri ya kuamini hivyo kutokana na kilichowahi kufanyika huko nyuma (predence) - hawa ndugu zetu wataambiwa wazirudishe fedha zote walizozipokea toka mikononi mwa Rugemalira na wenzake. Kama wana chembe ya hekima na uadilifu wajipeleke wenyewe machinjioni.

Kuna sababu kubwa mbili kwanini wanatakiwa wazirudishe:

1. Walionesha kuwa siyo waadilifu kwa kupokea fedha hizi. Wote waliopokea fedha za escrow walipaswa kugundua mara moja kuwa "something is very wrong". Karibu wote ni wasomi na wengi wao ni watumishi wa umma au wa jamii. Baada ya taarifa za kuwa waligawiwa mamilioni ya fedha kwa makundi makundi na mtu ambaye anatajwa kuhusika na kashfa ya IPTL ambayo ilikuwa inajulikana kwa muda mrefu basi watu hawa wote kama wangekuwa na uadilifu hata kidogo tu wangesema hizi fedha za moto!

Badala yake katika njaa zao na ukosefu wao wa uadilifu (lack of integrity) wakazipokea kwa mikono mitupu na kila mmoja akijielezea kwanini anapaswa kubaki nazo. Unapokea fedha vipi wakati unaona majina ya watu toka TRA, Ikulu, wabunge, majaji, viongozi wa dini na bado ukadhani uko salama?

2. Tangu wapokee fedha hizo miaka kadhaa nyuma ndugu zetu hawa nina uhakika kama kuzila walishazila na kama kuzifanyia shughuli wameshafanyia shughuli zao mbalimbali. Lakini wamekula kisicho chao na wameshiriki kula visivyoruhusiwa kwao. Walifanya hivyo kwa sababu waliamini kabisa kuwa "they got away with it". Kwamba, wakija kuulizwa wao watasema tu "si tumepewa jamani kosa letu ni nini?". Tatizo ni kuwa hawa wote ni viongozi ambao wanajua kabisa au walipaswa kujua shetani hana zawadi ya bure (the devil has no free gifts).

Ukikuta hela imeingia kwenye akaunti yako ambayo hujui imetokana na nini au kwanini usikimbilie kuitumia tu. Mwezi Machi 2012 huko Philadelphia kijana mmoja wa miaka 22 alijikuta ameingiziwa kwenye akaunti yake dola 70,000 wakati yeye alikuwa na dola 35 humo. Jamaa akajua amebarikiwa akawa anaenda kwenye ATM kutoa hela, kwa karibu wiki mbili hivi akawa ametumia dola 2000! Benki ikagundua kosa na jamaa akaja kukamatwa na polisi kwa kupokea na kutumia fedha za wizi!

Huko Georgia kijana wa miaka 18 alijikuta ameingiziwa dola 30,000 kwa makosa kwa vile jina lake na ambaye alikuwa anatakiwa kuingizwa fedha yalifanana na teller alichanganya tu. Kijana huyo akaamua kuzila hizo fedha, aliposhtakiwa na kukutwa na hatia na kuwekwa chini ya uangalizi wa mahakama kwa miaka 10 na kutakiwa kurudisha fedha alizotumia.

Sasa ndugu zetu hawa wote maafisa wa umma, unapokea vipi fedha kwa mamilioni bila kushtuka isipokuwa kama ulikuwa umeshajua fedha zinakuja na unatakiwa uchangamkie. Hisia zangu ni kuwa sehemu ya fedha hizo zilirudishwa kwa kina Ruge au watu wengine (ikiwa sehemu ya utakatishaji) lakini sehemu yake ilibakia na kuliwa na waliokubali akaunti zao zitumiwe.

Huu ni ufisadi tu.

Sasa, hawa ndugu zetu wasome alama za nyakati (signs of the times); hawako salama, Mali zao haziko salama, uhuru wao hauko salama, na wasipoangalia familia zao zitajikuta haziko salama na kila walichodhania ni kinga kwao hakipo tena. Walikingiwa kifua na utawala wa Kikwete, lakini there is a new sherrif in town and he ain't bulls@$!!g!

Ili labda yasiwakute:
1. Ombeni utaratibu wa kurudisha fedha zile wenyewe kabla hawajawajia. What you gonna do when they come for you!

2. Na kama mna utimamu andikeni cheki mzirudishe fedha hizo kwa serikali iziweke kwenye mfuko maalum ambapo zitakusanywa.

3. Serikali inakuja dhidi yenu kuzirudisha fedha hizo na adhabu juu. Jiandaeni kwan labda... labda... labda.. mnaweza MSIPIGISHWE MAGOTI NA KUCHUCHUMAISHWA!

mmm
 
Punainen

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,201
2,000
Hiyo ni kwa wale waliojulikana ile % ngapi vile sijui.... Haya na kwa wale waliochukua ile % nyingine tuliyoambiwa walibebea kwenye viroba na sandarusi?
 
charles mususa

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
289
250
So kw

a rugemalila Tellar alikosea? kuna watu kweli walipokea rushwa lakini kuna watu walipokea michango, askofu anahitaji rushwa ya nini hapo labda kama alihongwa amuombee na dhambi ya Escrow.Pesa za dhambi zimejaa makanisani lakini watoaji hawajawahi kusema hizi ni pesa za wizi.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
82,691
2,000
Pesa zile si za umma - Kikwete .

Halafu ningependa kujua kama hii nayo ni ID ya Mwanakijiji ?
 
bne

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
1,618
2,000
Wote nao hawana kosa. Mwenye kosa ni yule aliyetangazia umma na kuruhusu zichotwe. Mbona huyu mtu hammsemi?
Huyu ndiye chimbuko LA yote kwann mnazunguka mbuyu?
Kwa kauri yake mwenyewe alisema " PESA HIZI SI ZA UMMA, NI ZAO, SISI TULIZIWEKA KWA MINAJILI YAO SASA KELELE ZA NINI?"
 
mliberali

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
8,488

huyu jamaa anaandika vitu laini, ni nani aliidhinisha gala itoke hazina
 
MR MAJANGA

JF-Expert Member
Oct 4, 2014
2,345
2,000
Mkuu hao vijana uliotolea mifano Ni wameingiziwa pesa bila kumjua aliyewawekea, lakini wakina tibaijuka wamewekewa na aliyewawekea yupo na kakiri aliwapa, kisheria wakina tibaijuka hawana kosa
 
MR MAJANGA

JF-Expert Member
Oct 4, 2014
2,345
2,000
Halafu hawa Ni walio chukua mkombozi tunawajua lakini wale wa stanbic bado hatujawajua na usishangae rais akasema wasitajwe
 
mvujajasho

Member
Oct 27, 2010
24
45
Angeanza kuandika hii post bila kuanza na " Maoni ya Mwanakijiji baada ya...." swali lako la pili lingekuwa valid. Soma tena post yake utaelewa

Halafu ningependa kujua kama hii nayo ni ID ya Mwanakijiji ?[/QUOTE]
Angeanza
 
Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,108
2,000
So kw

a rugemalila Tellar alikosea? kuna watu kweli walipokea rushwa lakini kuna watu walipokea michango, askofu anahitaji rushwa ya nini hapo labda kama alihongwa amuombee na dhambi ya Escrow.Pesa za dhambi zimejaa makanisani lakini watoaji hawajawahi kusema hizi ni pesa za wizi.

naona una mix kusikia maaskofu

board of directors wa mkombozi bank ni hao unaowaita maaskofu

hakuna msafi pale
 
frank nyantu2

JF-Expert Member
Jun 26, 2016
299
250
Mkuu hao vijana uliotolea mifano Ni wameingiziwa pesa bila kumjua aliyewawekea, lakini wakina tibaijuka wamewekewa na aliyewawekea yupo na kakiri aliwapa, kisheria wakina tibaijuka hawana kosa
Ki vyovyote wansjua ni za nini! Utetezi wao ni laini sana!
Imagine jamaa anakuijia nakuambia njoo nikupe zawadi ya millioni mia! lazima upagawe ikibidi utagoma tu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom