Maswali ya mwisho juu ya Escrow

Maswali ya mwisho juu ya Escrow

Kulikuwa kuna issue mbili tofauti, ya tanesco na escrow ilishatolewa maamuzi zamani sana na Kikwete kalielezea hilo, rudia hotuba yake, kama una uwezo huo.

Na pia kulikuwa kuna utata kati ya wabia na ndiyo huo ulipelekea IPTL kuwa chini ya RITA, baada ya mgogoro huo kwisha na kwa kuwa tatizo la IPTL TANESCO liliisha amuliwa na ICSID ikawa hakuna tena kadhia nyingine bali kupata ushirikiano wa pande zote zinazohusika na ndicho kilichafanyika na kufikiwa muafaka uliopitishwa na mahakama.

Na isitoshe, mahakama ikahakikisha kuwa Ruge analipwa na kodi analipa na PAP wanakubali kuwekeza tena kwa bei nafuu kabisa.

Naona mnazunguka mbuyu tu, yote yako wazi kama mchana wa saa sita.
Escrow imezaliwa baada ya hukumu hiyo ya ICSID na kweli Mh Rais alilieleza hili. Mh Rais pia alieleza kuwani malalamiko ya Tanesco baada ya hukumu hiyo ndiyo yalipelekea kufunguliwa kwa akaunti hii. Malalamiko hayo mpaka leo yapo na hayakutatuliwa kabla fedha hizo hazijachotwa. Mnapotasha makusudi kuhalalisha, lakini ni kuwa Escrow haikufunguliwa kwa sababu ya mgogoro wa wanahisa bali kwa sababu ya malalamiko ya tanesco kuhusiana na capacity charge au gharama za uwekezaji!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Bosi wangu wa zamani aliniasa kuwa, Ukitaka kusema uongo mmoja yaani mara moja, inabidi ujifunze kusema uongo mwingine mara mia moja kwa ajili ya kuulinda huo uongo mmoja. Mkulu wetu hayajui hayo.

Wewe unalolijuwa nini?

Badala ya kubwabwaja na kuhororoja, kuna maazimio ya bunge manane kapelekewa Kikwete, tuoneshe wewe katika hayo manane utatatuwa vipi badala ya alivyofanya Kikwete.
 
Majibu yenu mlio wengi sio mazuri hata chembe, kauliza ili apate majibu sio mengineeee
 
Naona na utaahira unakuanza sasa wa kutaka kubadili neno kujiuzulu na kuingiza neno kujiudhuru. Ajuza alisema ana udhuru hivyo hataweza kuhudhuria sherehe za leo. Werema ameamua kujiuzulu (na siyo kujiudhuru) nafasi yake ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Acha ubishi wa kipumbavu na wa kitoto.

Mmevifanya kuwa viwili tofauti kwa kutokujuwa kwenu Kiswahili fasaha na chimbuko la maneno.

"uzulu" ni simply broken udhuru ambayo mimi siikubali mpaka leo na hata useme nini. "Uzulu" si Kiswahili fasaha, kujiudhuru ni kutoa udhuru kama alivyofanya Werema, kajiudhuru kuwachia wadhifa wake kama AG.
 
Escrow imezaliwa baada ya hukumu hiyo ya ICSID na kweli Mh Rais alilieleza hili. Mh Rais pia alieleza kuwani malalamiko ya Tanesco baada ya hukumu hiyo ndiyo yalipelekea kufunguliwa kwa akaunti hii. Malalamiko hayo mpaka leo yapo na hayakutatuliwa kabla fedha hizo hazijachotwa. Mnapotasha makusudi kuhalalisha, lakini ni kuwa Escrow haikufunguliwa kwa sababu ya mgogoro wa wanahisa bali kwa sababu ya malalamiko ya tanesco kuhusiana na capacity charge au gharama za uwekezaji!
Malalamiko bado yako kwa nani sasa ikiwa wawili waliokuwa wakilalamikiana yaani tanesco na iptl waliyamaliza na ndo pesa zikatoka.hebu twambie nani anaelalamika tena kati yao?
Ukiangaliwa makubaliano ya power purchasing agreement haijakiukwa,na pia hata hiyo account ilikua na mkataba ambao ulifuatwa kabla account haijafungw.
 
Wewe unalolijuwa nini?

Badala ya kubwabwaja na kuhororoja, kuna maazimio ya bunge manane kapelekewa Kikwete, tuoneshe wewe katika hayo manane utatatuwa vipi badala ya alivyofanya Kikwete.

Nitakapokuwa Rahisi wa Jamuhuri ya muungano ya Wadanganyika nitakueleza unachouliza leo. Wewe ni mdanganyika binti taabani.
 
Anayebisha kuwa pesa siyo za IPTL natilia shaka sana akili zake huenda zinashida mahala fulani.
Umenifanya nitilie shaka utashi wako. Yaani bila wasiwasi unasema pesa yote ni ya IPTL!? Ulikuwepo wakati wanakokotoa hizo hesabu za 'capacity charges' na wakakubaliana pesa zote ni za IPTL? Uhalisia ni kwamba bila ukokotoaji wa hesabu za capacity charges kwa pande zote mbili pesa haziwezi kujulikana zipi ni za IPTL na zipi ni za TANESCO.
Hapa kinachoendelea ni 'betting' au 'utabiri tu'. Zile pesa hazikupaswa kutolewa mpaka hizo hesabu zitakapofanywa maana ndio msingi wa mgogoro.
Hata wakaja kufanya ukokotoaji na ikaonekana ni kweli pesa yote ni ya IPTL mnaosimamia kwa sasa pesa ni ya IPTL hamko sahihi bali mtakuwa mmeshinda kwa 'kutabiri'.
Logically, haijulikani ni kiasi gani gani ni pesa ya TANESCO wala ya IPTL. Kilichotokea ni kwamba pesa imechukuliwa bila kujulikana aliyechukua mgao wake ni kiasi gani, yeye kachukua yooote!!
Haihitaji elimu kubwa kulifahamu jambo hili ndugu!
 
Mkuu WildCard naomba majibu kwa maswali haya marahisi:

1. Je, waziri ulipwa mshahara kwa nafasi yake ya uwaziri? Ama upokea tu mshahara wake wa Ubunge?

2. Je, waziri na katibu mkuu, mteuzi wao ni nani? Kama mteuzi wao ni mmoja, kwanini uwajibikaji wao uwe tofauti?
 
Last edited by a moderator:
Mniwie radhi kwa kuuliza. Nauliza kwa mara ya mwisho. Sitauliza tena. Nitabaki kimya hata kisemwe au kifanywe niní. Sitauliza tena juu ya Escrow. Nitasubiria tu kashfa za bomba la gesi na sukari. Basi.

Kwakuwa tumeambiwa na Rais kuwa mabilioni yaliyokuwemo Escrow yote yalikuwa ya IPTL. Na kwakuwa tumeambiwa na kuaminishwa na Rais kuwa mabilioni ya Escrow yalilipwa au kupewa mwenyewe ambaye ni IPTL.

Na kwakuwa mwenye mabilioni,IPTL,amechukua chake kiutaratibu na Serikali ilijua. Je,uchunguzi na hatua zinazoendelea kuchukuliwa hivi sasa zinalenga niní? Wanaochunguzwa wanachunguzwa kwa makosa yapi hasa?

Hata nisipojibiwa,nitaridhika kama mwafrika!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Bado kuna maswali mengi.... Je miamala iliyofanyika Mkombozi na Stanbic bank ilikuwa halali kwa sheria za kibank hapa tanzania? Walonufaika ni watumishi wa umma je ilikuwa ni per Diem au mishahara wanalipwa.? Fedha ni za IPTL kwanini zipo ktk vitabu vya Tanesco? Je kuna hati halali ya mahakama iliyoandikwa kwenda BoT na Tanesco kuonesha mgogoro umeisha. Je TRA wamekwisha omba radhi kuwa walikosea kudai kodi kwa fedha ambazo hazistahili kulipiwa kodi? Rugemalira amesharudishiwa kodi yake maana pesa hiyo haistahili kulipiwa kodi? Kodi ya ongezeko la mtaji , Mabadiliko ya wanahisa na dokyument halali zilishakabidhiwa kwa Brella, fedha zote ni za IPTL SAWA je hivi ndivyo madeni yote na kesi zinazofanana ni hizi hushughulikiwa na Bank Kuu. Au ndiyo mambo ya mkuu wa nchi kuuita sarafu yake madafu.
 
Naona na utaahira unakuanza sasa wa kutaka kubadili neno kujiuzulu na kuingiza neno kujiudhuru. Ajuza alisema ana udhuru hivyo hataweza kuhudhuria sherehe za leo. Werema ameamua kujiuzulu (na siyo kujiudhuru) nafasi yake ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Acha ubishi wa kipumbavu na wa kitoto.

Juu huko umeshanisoma, hili nimekwambia hata useme nini, kwangu NO. Mnakiharibu Kiswahili, uzulu linatoka wapi? udhuru ukili trace utajuwa exactly limetoka wapi.

Werema katoa udhuru upi alipowachia wadhifa wake? Sasa soma hii, Werema katoa uzulu upi alipowachia wadhifa wake?

Chaguo ni lako, unaonesha shule walimu wako wamepata taabu sana, kwani uelewa wako uko finyu sana.
 
Nitakapokuwa Rahisi wa Jamuhuri ya muungano ya Wadanganyika nitakueleza unachouliza leo. Wewe ni mdanganyika binti taabani.

Sasa umekosa hoja unaanza viroja na kuhororoja, kama umeishiwa kaa pembeni waache wenzako tuendelee kuwapa darsa.
 
Bado kuna maswali mengi.... Je miamala iliyofanyika Mkombozi na Stanbic bank ilikuwa halali kwa sheria za kibank hapa tanzania? Walonufaika ni watumishi wa umma je ilikuwa ni per Diem au mishahara wanalipwa.? Fedha ni za IPTL kwanini zipo ktk vitabu vya Tanesco? Je kuna hati halali ya mahakama iliyoandikwa kwenda BoT na Tanesco kuonesha mgogoro umeisha. Je TRA wamekwisha omba radhi kuwa walikosea kudai kodi kwa fedha ambazo hazistahili kulipiwa kodi? Rugemalira amesharudishiwa kodi yake maana pesa hiyo haistahili kulipiwa kodi? Kodi ya ongezeko la mtaji , Mabadiliko ya wanahisa na dokyument halali zilishakabidhiwa kwa Brella, fedha zote ni za IPTL SAWA je hivi ndivyo madeni yote na kesi zinazofanana ni hizi hushughulikiwa na Bank Kuu. Au ndiyo mambo ya mkuu wa nchi kuuita sarafu yake madafu.

Kwa porojo tu haujambo, lakini ukweli NIL.

Hilo ndiyo tatizo lenu kubwa bavichaa.
 
Mirembe wanakusubiri wakatibu akili yako iliyoanza kuharibika,wahi kabla hali haijawa mbaya zaidi. Na kwa taarifa yako shule kwangu ilikuwa ni rahisi mno kwa sababu nilijua wajibu wangu kama mwanafunzi, hivyo tangu darasa la kwanza mpaka vyuoni nilikuwa napeta tu kwa raha zangu.

Juu huko umeshanisoma, hili nimekwambia hata useme nini, kwangu NO. Mnakiharibu Kiswahili, uzulu linatoka wapi? udhuru ukili trace utajuwa exactly limetoka wapi.

Werema katoa udhuru upi alipowachia wadhifa wake? Sasa soma hii, Werema katoa uzulu upi alipowachia wadhifa wake?

Chaguo ni lako, unaonesha shule walimu wako wamepata taabu sana, kwani uelewa wako uko finyu sana.
 
FaizaFoxy sijapiga porojo bali nimeuliza maswali yanayonisumbua mimi mwenye ubongo mdogo usioweza kufikiri kwa kina. Nakuamini sana kuwa wewe ni genious utaweza kutupatia majibu sisi wenye akili ndogo.
 
Ndugu FaizaFoxy sijapiga porojo bali nimeuliza maswali yanayonisumbua mimi mwenye ubongo mdogo usioweza kufikiri kwa kina. Nakuamini sana kuwa wewe ni genious utaweza kutupatia majibu sisi wenye akili ndogo.
 
Ziliwekwa kule kwa muda kwa kuwa kulikuwa na kesi kati wanahisa wa IPTL.Zikawekwa kwenye akaunti ya ESCROW ambayo hakuna mwenye hisa yeyote angeweza kuchukua hadi kesi imalizike.Zingewekwa akaunti ya IPTL mwanahisa yeyote angeweza amka asubuhi na kuzitoa pesa zote ndio maana zikawekwa kwenye ESCROW ACCOUNT.
Unaweza kutukumbusha kesi ilimaliizika lini.
 
Escrow imezaliwa baada ya hukumu hiyo ya ICSID na kweli Mh Rais alilieleza hili. Mh Rais pia alieleza kuwani malalamiko ya Tanesco baada ya hukumu hiyo ndiyo yalipelekea kufunguliwa kwa akaunti hii. Malalamiko hayo mpaka leo yapo na hayakutatuliwa kabla fedha hizo hazijachotwa. Mnapotasha makusudi kuhalalisha, lakini ni kuwa Escrow haikufunguliwa kwa sababu ya mgogoro wa wanahisa bali kwa sababu ya malalamiko ya tanesco kuhusiana na capacity charge au gharama za uwekezaji!

Usipotoshe, jisomee halafu tuonesha hayo usemayo yako wapi?, hotuba mbona ipo karibu:

Ndugu Wananchi;
Mwaka 1998 TANESCO walifikisha kwenye Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji, London, malalamiko kwamba gharama za uwekezaji za IPTL ni kubwa mno kuliko kiasi halisi walichowekeza. Mwaka 2001 Kituo cha Usuluhisi kilifanya uamuzi wa shauri hilo. Madai ya TANESCO yalikubaliwa kuwa uwekezaji halisi uliofanyika ni Dola za Marekani 127 na siyo Dola milioni 163.17 walizodai IPTL. Kutokana na kupungua huko kwa gharama za uwekezaji, tozo ya uwekezaji (capacity charges) nayo ilipunguzwa kutoka Dola za Marekani milioni 3.6 kwa mwezi mpaka Dola za Marekani milioni 2.6 kwa mwezi. Kituo pia, kilitoa mwongozo kuhusu ukokotoaji wa tozo hiyo.

Ndugu Wananchi;
Miaka minne baadaye TANESCO ilianza vuguvugu la kutaka kupata nafuu zaidi. Waliamua kugomea kulipa tozo ya uwekezaji kwa mkokotoo wa mwaka 2001. Nimeambiwa kuwa wanasheria wa TANESCO walishauri Shirika hilo lidai ukokotoaji kiwango cha tozo ya uwekezaji wa IPTL ufanyike kwa kuzingatia thamani ya hisa walizolipia wawekezaji ambayo ni shilingi 50,000 badala ya kutumia msingi wa mtaji uliotokana na mkopo wa Dola za Marekani milioni 38.16 wa wanahisa uliotumiwa na usuluhisho wa kwanza ICSID-1.
Wakati wakisubiri mchakato wa usuluhishi wa mzozo huu mpya kuanza, pande zote mbili zilikubaliana kuanzisha Akaunti ya Escrow ya Tegeta. Tarehe 5 Julai, 2006, akaunti hiyo ikaanzishwa kwa mkataba uliyotiwa sahihi na IPTL upande mmoja na Wizara ya Nishati na Madini kwa niaba ya TANESCO upande mwingine. Aidha, Benki Kuu iliteuliwa kuwa wakala wa kutunza akaunti hiyo nayo ilitia sahihi.

Ndugu Wananchi;

Kwa mujibu wa mkataba huo, Kampuni ya IPTL iliendelea kupeleka madai ya tozo ya uwekezaji kwa TANESCO ambayo nayo iliwajibika kulipa madai hayo. Malipo hayo yalitakiwa kupelekwa kwenye Akaunti ya Escrow ya Tegeta tofauti na ilivyokuwa kabla ambapo yalipelekwa IPTL moja kwa moja. Utaratibu huu mpya ulikubaliwa kutumika hadi pande mbili zitakapofikia mwafaka kuhusu kiwango cha ukokotoaji. Kwa upande wa malipo ya gharama ya umeme (energy charges) TANESCO imeendelea kulipa moja kwa moja kwa IPTL bila kupitia Akaunti ya Tegeta ESCROW maana hizo hazikuwa na mgogoro.

Ndugu Wananchi;

Kwa miaka saba tangu tarehe 5 Julai, 2006, akaunti hiyo ilipoanzishwa mpaka tarehe 5 Septemba, 2013, wakati Mahakama Kuu ilipokabidhi shughuli zote za IPTL kwa PAP, hakuna hatua stahiki zilizochukuliwa kutafuta ufumbuzi wa mzozo wa tozo ya uwekezaji baina ya ITPL na TANESCO. Pande mbili husika hazikuwahi kukaa kuzungumza na wala hakuna shauri lililofikishwa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Mogogoro ya Uwekezaji kama ilivyofanyika mwaka 1998.
Wakati wote huo, TANESCO iliendelea kulipa madai ya tozo ya uwekezaji ya IPTL na kupeleka malipo hayo kwenye Akaunti ya Escrow. Ulipaji ulisimama katika kipindi kifupi wakati kampuni ya IPTL ilipowekwa kwenye ufilisi. Kwa mujibu wa taarifa ya CAG, wakati akaunti hiyo inafungwa tarehe 20 Novemba, 2013, kulikuwa na fedha taslimu shilingi 8,020,522,330.37; Hatifungani zenye thamani ya shilingi 159,231,370,000 na Dola za Marekani 22,198,544. Fedha zote hizo ni sawa na shilingi bilioni 202.9.

Ndugu Wananchi;

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kama TANESCO ingelipa tozo ya uwekezaji ipasavyo, wakati huo Akaunti hii ingekuwa na shilingi bilioni 306.7. Kwa sababu ya kutolipa fedha zote ipasavyo, wakati Akaunti inafungwa TANESCO walikuwa wanadaiwa na IPTL shilingi bilioni 103.8. Kwa mujibu wa Mkataba wa Mauzo ya Umeme (PPA) malipo yaliyocheleweshwa, yanatozwa riba ya asilimia mbili ya fedha zote ambazo hazikulipwa kwa wakati. Hivyo basi, riba iliyotokana na TANESCO kuchelewesha malipo ilikuwa Dola za Marekani milioni 33.6.
Ni matumaini yangu kuwa ufafanuzi uliotolewa katika Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali unasaidia kuweka kumbukumbu sawa na sahihi kuhusu kiasi gani kilichokuwepo kwenye Akaunti ya ESCROW siku uamuzi wa Mahakama ulipofanya akaunti hiyo ifungwe. Kwa kifupi Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaeleza kuwa Akaunti hiyo ilikuwa na shilingi bilioni 202.9 na siyo shilingi bilioni 306.7 kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
 
Back
Top Bottom