Mniwie radhi kwa kuuliza. Nauliza kwa mara ya mwisho. Sitauliza tena. Nitabaki kimya hata kisemwe au kifanywe niní. Sitauliza tena juu ya Escrow. Nitasubiria tu kashfa za bomba la gesi na sukari. Basi.
Kwakuwa tumeambiwa na Rais kuwa mabilioni yaliyokuwemo Escrow yote yalikuwa ya IPTL. Na kwakuwa tumeambiwa na kuaminishwa na Rais kuwa mabilioni ya Escrow yalilipwa au kupewa mwenyewe ambaye ni IPTL.
Na kwakuwa mwenye mabilioni,IPTL,amechukua chake kiutaratibu na Serikali ilijua. Je,uchunguzi na hatua zinazoendelea kuchukuliwa hivi sasa zinalenga niní? Wanaochunguzwa wanachunguzwa kwa makosa yapi hasa?
Hata nisipojibiwa,nitaridhika kama mwafrika!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Wewe punguani kweli kweli, hebu rudia hotuba ya Kikwete, kuna mambo makuu manne tofauti katika sakata hili.
Zinazochunguzwa siyo kama pesa ni za umma au la hilo limeshatolewa majibu, si za umma.
Kuna mengi sana ya kuchunguzwa, mfano, kama kuna rushwa imetendeka au la, kama Mhongo anahusika au la, kama Maswi anahusika au la, kama benki ya Stanbic inasafisha pesa chafu au la, kwanini TANESCO hawajalipa pesa zote, kama akina Kilaini na Kanisa katoliki walihusika au la kwani na wao wamepata mgao.
Kuna mengi sana ya kuchunguza lakini si hilo la pesa kama ni za umma au la. Hukumsikia Kikwete? basi kama hukumsikia basi si urudie hotuba yake, ipo mtandaoni kimaandishi na video, badala ya kukurupuka? hilo la kama pesa za umma au la ni historia na kishasema hizo si za umma ni za IPTL au kwa sasa PAP. Halina ubishi kabisa.
Kwani kazi ya kwanza ya CAG mpya alivyokwisha apishwa alisema itakuwa ni hiyo ili kuondoa utata, itabidi CAG aseme za umma au la na nnauhakika CAG kasema si za umma. Kikwete huwa hakurupuki.
Hapo sasa.
Ziliwekwa kule kwa muda kwa kuwa kulikuwa na kesi kati wanahisa wa IPTL.Zikawekwa kwenye akaunti ya ESCROW ambayo hakuna mwenye hisa yeyote angeweza kuchukua hadi kesi imalizike.Zingewekwa akaunti ya IPTL mwanahisa yeyote angeweza amka asubuhi na kuzitoa pesa zote ndio maana zikawekwa kwenye ESCROW ACCOUNT.
Kwahiyo kesi ilimalizika vizuri ndiyo mahakama ikakubali IPTL walipwe fedha zao ?
Kweli wewe ndiyo hujitambui , kama hizo fedha siyo za umma......By FaizaFoxy![]()
Wewe punguani kweli kweli, hebu rudia hotuba ya Kikwete, kuna mambo makuu manne tofauti katika sakata hili.
Zinazochunguzwa siyo kama pesa ni za umma au la hilo limeshatolewa majibu, si za umma.
Kuna mengi sana ya kuchunguzwa, mfano, kama kuna rushwa imetendeka au la, kama Mhongo anahusika au la, kama Maswi anahusika au la, kama benki ya Stanbic inasafisha pesa chafu au la, kwanini TANESCO hawajalipa pesa zote, kama akina Kilaini na Kanisa katoliki walihusika au la kwani na wao wamepata mgao.
Kuna mengi sana ya kuchunguza lakini si hilo la pesa kama ni za umma au la. Hukumsikia Kikwete? basi kama hukumsikia basi si urudie hotuba yake, ipo mtandaoni kimaandishi na video, badala ya kukurupuka? hilo la kama pesa za umma au la ni historia na kishasema hizo si za umma ni za IPTL au kwa sasa PAP. Halina ubishi kabisa.
Kwani kazi ya kwanza ya CAG mpya alivyokwisha apishwa alisema itakuwa ni hiyo ili kuondoa utata, itabidi CAG aseme za umma au la na nnauhakika CAG kasema si za umma. Kikwete huwa hakurupuki.
Hapo sasa. :
Ziliwekwa kule kwa muda kwa kuwa kulikuwa na kesi kati wanahisa wa IPTL.Zikawekwa kwenye akaunti ya ESCROW ambayo hakuna mwenye hisa yeyote angeweza kuchukua hadi kesi imalizike.Zingewekwa akaunti ya IPTL mwanahisa yeyote angeweza amka asubuhi na kuzitoa pesa zote ndio maana zikawekwa kwenye ESCROW ACCOUNT.
Anayebisha kuwa pesa siyo za IPTL natilia shaka sana akili zake huenda zinashida mahala fulani.
Mkuu umenichanganya kabisa.kwenye katiba inayopendekezwa chama chetu kimeruhusu viongozi wa umma wawe na account nje ya nchi.Je hizo account ni kwa ajiri ya kupokelea mshahara tu?Wanachunguzwa kwa uvunjaji wa maadili ya uongozi wa umma.Mfano Waziri Tibaijuka aliomba msaada kwa ajili ya Shule halafu hela ikawekwa kwenye akaunti yake binafsi badala ya akaunti ya shule.Kama kiongozi alitakiwa ahakikishe pesa ile inaenda akaunti ya shule.
Sasa wengine wanafuatiliwa kwa misingi ya namna hiyo
Shangazi FaizaFoxy nami nimekuwa mvivu naomba kufahamu AG amaendika barua ya kujiuzulu akidai ushauri wake haukueleweka na kupelekea kuchafua hali ya hewa, kwa nini asifafanue tena huo ushauri wake ili aeleweke na kwanini bosi wake ambaye ni JK aridhie kujiuzulu kwake?Hilo swali tumeshalijibu humu, unaonesha ni mvivu wa kutembea-tembae JF kwenye mada zinazohusu hii kadhia, si kitu, hili hapa jibu la aliyeuliza kama wewe, nawe litakufaa:
ndio mkuu
Mkuu hapa serikali iliingiaje?au nayo ina hisa IPTLZiliwekwa kule kwa muda kwa kuwa kulikuwa na kesi kati wanahisa wa IPTL.Zikawekwa kwenye akaunti ya ESCROW ambayo hakuna mwenye hisa yeyote angeweza kuchukua hadi kesi imalizike.Zingewekwa akaunti ya IPTL mwanahisa yeyote angeweza amka asubuhi na kuzitoa pesa zote ndio maana zikawekwa kwenye ESCROW ACCOUNT.
Kweli wewe ndiyo hujitambui , kama hizo fedha siyo za umma.....
Unachunguza kama rushwa imetendeka, Kwanini rushwa itendeke?
Kwanini Maswi achunguzwe kama anahusika? Anahusika na nini sasa?
Kwanini muhongo anachunguzwa kama anahusika , anahusika kwa nini sasa kama mambo yote yalifuata utaratibu na fedha si za umma?
Stanbic inasafisha pesa chafu au la , km pesa siyo za umma hao stanbic wanachunguzwa ya nini na kulikuwa na haja gani ya wao kusafisha hela ya malipo halali kutoka BOT?
Na huyo CAG kasema lini hizo hela siyo za umma?
Kuficha wizi ni kazi sana.
Taratibu mtaendelea kuumbuka, just wait.
Mmoja wao ni Prof.Mwandosya,Wassira na Mwigulu mawaziri katika Serikali ya ccmAnayebisha kuwa pesa siyo za IPTL natilia shaka sana akili zake huenda zinashida mahala fulani.
Maazimio haya yalifikiwa na Bunge(Wananchi) kwa kuamini/kujua kuwa pesa zile zilikuwa ni za Umma.Kwa Kuwa mkuu wa nchi amethibitisha kuwa pesa zile hazikuwa za umma,Mapendekezo yale yalitakiwa yawe yamejifuta yenyewe.Kuendelea kuchunguza tuhuma hewa ni ufisadi mwingineNaona unachanganya mambo.
Kuna mambo manne makuu tofauti katika suala la escrow, Jee, unayajuwa au unakurupuka tu?
Hilo la kuchunguza ni azimio la Bunge, sasa waulize wabunge wako kwanini walitaka ufanyike uchunguzi? au ulitaka uchunguzi usifanyike kama azimio la bunge lilivyoazimia? Na Kikwete kalielezea hilo wazi wazi na hatua zilizochukuliwa, hili hapa:
Azimio la Tatu: Linasomeka; "Bunge linaazimia kwamba TAKUKURU, Jeshi la Polisi na vyombo vingine husika vya ulinzi na usalama vichukue hatua stahili kwa mujibu wa sheria za nchi yetu dhidi ya watu waliotajwa kwenye taarifa maalum ya Kamati husika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya Akaunti ya ESCROW, na watu wengine watakaogundulika kufuatia uchunguzi mbalimbali unaoendelea kuhusu kuhusika kwao katika vitendo hivyo vya jinai"
Vyombo husika vimekwishaagizwa kufanya hivyo na kazi imeanza na inaendelea. Ikiwa wapo watu wenye makosa hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria.
Wewe ndiyo unakurupuka na kujaribu kupotosha.Naona unachanganya mambo.

Escrow is money or property which is given to someone, but which is kept by another person until the first person has done a particular thing or met a particular requirements( mainly LEGAL).Mkuu hapa serikali iliingiaje?au nayo ina hisa IPTL