Maswali ya Kipima Joto yanaboa

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Nimefuatilia maswali ambayo yanaulizwa na ITV kwa kile kinachoitwa "Kipima Joto". Maswali haya ambayo yana lengo la kupoll kujua watu wana misimamo gani juu ya masuala mbalimbali ya kisiasa na kijamii. Naomba nikiri kuwa hadi hivi sasa maswali haya tayari yanaashiria wanataka jibu gani (suggestive questions) kiasi kwamba ni vigumu kweli kupata mtu anayepinga au mwenye msimamo tofauti.

Pendekezo: Jaribu kuuliza maswali ambayo hayaashirii jibu mnalolitaka.

Huwezi kumuuliza mtu "Je, mauaji ya Albino yalaaniwe?" au "Unafikiri wanaokula rushwa wafikishwe mahakamani?"!
 
Totally agree with you! Creativity hakuna tena. Nimekuwa niki-hisi kuna pressure behind it. Is Hakielimu sponsoring kipimajoto?
 
mimi huwa sisikilizi, wala huwa sitilii maanani kabisa, uwa naona kama utoto vile, na ni mawazo ya mtu mmoja wanatudanganya wamefanya survey kumbe hamna lolote wanataka kuimpose kitu chochote wanachoamini wao kuwa ni sahihi, yaani ni njia ya kutuma meseji wanayotaka iwafikie wananchi...pamoja na kwamba inasaidia kwa namna fulani lakini.
 
kimsingi kwa taratibu za research haya maswali ya ITV hayawezi na hayakubaliki kuwa research questions because among other things are suggestive. Wanahitaji kutafuta mtaalamu awe akiwatungia maswali!
 
Kipimajoto ni pacha na kipimabaridi cha Ze Comedy.ZOTE NI COMEDY.
Ukitafakari utaona kuwa kipimajoto ni upuuzi mwingine unaojaza muda prime katika ITV maana hakuna mantiki yeyote kuuliza upate majibu ya NDIO, HAPANA au SIJUI halafu inaishia hapo.Toka kimeanza hatujaona matokeo ya hiyo poll ni nini.Ni afadhani wakifute tu.
 
Hii sio research, ni survey (becoz of sample size na ni swali moja tu). Lakini issue ni kwamba hata huo u-suggestive wake hautusaidii. Badala ya kuuliza kama mafisadi wapelekwe mahakamani, wangeweza hata kuuliza kama tunafikiri mafisadi wanashughulikiwa ipasavyo, au hata kama tunafikiri fedha za EPA kurudishwa sio changa la macho!
 
HATA SURVEYS inakuwa na objective...je objective ya Kipimajoto kwa mfano ..ni nini? watu 40% wakisema ndio..40% wakasema hapana na 20% wakasema hawajui..so what?..... TUNGEFAHAMISHWA HAYO MATOKEO YANAMAANISHA NINI ILI HATA WANAOSHIRIKI WAELEWE WALICHOKISEMA KINATAFSIRIWA VIPI.
 
Hii sio research, ni survey (becoz of sample size na ni swali moja tu). Lakini issue ni kwamba hata huo u-suggestive wake hautusaidii. Badala ya kuuliza kama mafisadi wapelekwe mahakamani, wangeweza hata kuuliza kama tunafikiri mafisadi wanashughulikiwa ipasavyo, au hata kama tunafikiri fedha za EPA kurudishwa sio changa la macho!
Best, if were are to define the events by their repercussions/ outcomes, then you must be in position to conclude that a research and a survey's difference is the same!
 
Ni kweli, afadhali umesema mwenzetu. Inafanya kipindi kisiwe na mvuto kabisa. Mara nyingi swali linakuwa katika msingi wa majibu kuliko kupata views za watu.
 
Mimi huwa sishangai maswali yao ya kipuuzi, huenda ndio kiwango chao kipoishia.

Huwa nawashangaa wanaopoteza fedha zao kujibu hayo maswali ya kipuuzi. Kwakweli wamepungukiwa kitu kichwani. Sisiti kuwaita wana ubongo wa kichina.
 
Halafu nilikuwa natafuta simu yao ili niwashirikishe mawazo yangu siku moja labda tutawachangamsha kidogo.
 
Hiyo tisa angalia sasa wanaojibu hayo maswali ana kwa ana hawana knowledge ndogo sana kuhusu swali husika so much so that hata haileti maana kuangalia na kusikiliza.
 
Nimefuatilia maswali ambayo yanaulizwa na ITV kwa kile kinachoitwa "Kipima Joto". Maswali haya ambayo yana lengo la kupoll kujua watu wana misimamo gani juu ya masuala mbalimbali ya kisiasa na kijamii. Naomba nikiri kuwa hadi hivi sasa maswali haya tayari yanaashiria wanataka jibu gani (suggestive questions) kiasi kwamba ni vigumu kweli kupata mtu anayepinga au mwenye msimamo tofauti.

Pendekezo: Jaribu kuuliza maswali ambayo hayaashirii jibu mnalolitaka.

Huwezi kumuuliza mtu "Je, mauaji ya Albino yalaaniwe?" au "Unafikiri wanaokula rushwa wafikishwe mahakamani?"!
Kipima joto, ni zuga tuu ili ionekane kama opinion poll, its not, the motive behind ni kamradi ka uchagishaji hivyo vijisenti vinavyokatwa kila unapotuma majibu kwa kutumia number hiyo.

Tena vipindi vingi tuu humu nchini, vinaendeshwa kinyume cha sheria, kisheria, walitakiwa waseme ujumbe unagharimu sh.ngapi ili watu wajue watakatwa.
 
Kipimajoto ni pacha na kipimabaridi cha Ze Comedy.ZOTE NI COMEDY.
Ukitafakari utaona kuwa kipimajoto ni upuuzi mwingine unaojaza muda prime katika ITV maana hakuna mantiki yeyote kuuliza upate majibu ya NDIO, HAPANA au SIJUI halafu inaishia hapo.Toka kimeanza hatujaona matokeo ya hiyo poll ni nini.Ni afadhani wakifute tu.
Hiyo ya ndiyo au siyo ipo kwenye research, ila mimi naungana na mtoa hoja,ni maswali ya aina gani hayo? ambayo tayari yamebeba jibu tayari?hilo ndo swali la kujiuliza,mi ninacho baadhi ya vyombo vyetu vya habari vinaajiri watu ambao bado ni wachanga
 
afadhari hata KIPIMA BARIDI cha ze comedy ya enzi zile kwani badala ya kuuliza kama swali wangeweza tu kutoa kama taarifa vilevile ilivyo na kuielimisha jamii zaidi..............hii inakuwa kama wanawafanya watu mbumbumbu kumbe sivyo.......la sivyo wabadilishe mfumo wa kutengeneza hivyo vipima joto.......
 
Back
Top Bottom