Maswali na majibu kuhusu Uhamiaji

Maswali na majibu kuhusu Uhamiaji

Mimi Nina passport ya East Africa je naweza safiria kwenda msumbiji ?

Hapana huwezi kusafiria kwenda msumbiji kwa kuwa sio mojawapo ya nchi zinazounda east africa.

Waweza kusafiria kwenda kenya uganda burundi rwanda bila kusahau Tanzania

Kama unataka kwenda msumbiji omba passport ya kimataifa ambayo inakuruhusu kusafiri kwenda nchi yoyote duniani ukijumlisha nchi za afrika mashariki
 
up date wadau jamaa wana achia lini majina mbona kimya kuna taarifa zilikuwepo humu kua tar 21 mwezi huu but bila bila na leo 22 embu wazee wa vyeti tupeni vyeti za hawa jamaa
 
Mambo yameisha iva jikon yanasubil kupakuliw tu,tuvut subila
 
mmh,marumbano ya nini? nadhani jamaa kafafanua vizuri,hawa jamaa wametuletea matatizo sana kiukweli uhamiaji inahitaji watu makini na waadilifu,kama mlikiuka kiapo,hapa katu hatuwaamini,thanks mkuu kwa kutoa majibu ya uhakika,chanzo ni kilekile ulichopatia tangazo la kwanza,huyu jamaa ni mtendaji wa ukweli wengine acheni ubabaishaji hata kama jf ni mtandao wa updates,na updates zenyewe ndo hizi.........
 
Mkuu vuta subira
tarehe 21 mwezi
wa 4 Batch ya kwanza inatoka.

Wiki ya pili ya tarehe 28 inatoka batch ya pili

wiki ya tatu ya tarehe 7 mwezi wa 5 inatoka ya Tatu


kweli naanza kuamini kuwa watajitokeza manabii wa uongo leo trh 22/4/14 nasubiri batch ya kwanza mbona hailetwi au ndio hadithi zile zile hatarudi hatarudi
 
Kaeni mkao wa kula wadau...kuna mdau amedokeza kuwa jumatano mambo yote mwake


Ndugu mtendaji wenzako wakina Tmajuto walitabiri kuwa itakuwa tarehe 21/4 na wewe umeongeza siku mbili yaani uhakika ni tarehe 23 sasa mimi naamua kuwa THOMASO wa kwenye biblia siamini hadi nifike mezani ya usaili.

hata ivyo nashukuru ingawa hii vita inaenda kuwa ngumu sana ila naona watu wanaichukulia simple sana,
 
Duh inshu ya leaving certificate ndo naiona Leo!!! Shame upon me....

sio wewe tu wengi ilo litawaponza, nakuombea mungu uitwe ila hakikisha izo leaving zipo home siku ya usaili unakuja nazo kibishi. kuna wadau walipanic sana na tangazo la kazi wakiamini pale uhamiaji ndo mdebwedo subiri siku wakitoka kwa usaili au shortlist wasiwepo wataleta midongo humu utacheka ufe
 
sio wewe tu wengi ilo litawaponza, nakuombea mungu uitwe ila hakikisha izo leaving zipo home siku ya usaili unakuja nazo kibishi. kuna wadau walipanic sana na tangazo la kazi wakiamini pale uhamiaji ndo mdebwedo subiri siku wakitoka kwa usaili au shortlist wasiwepo wataleta midongo humu utacheka ufe

Hilo tangazo sio la mwaka huu coz nilirudi tovuti ya uhamiaji kujirishisha. Hakuna sharti la leaving certificates. Asante sana kwa dua njema. Mungu atatenda kwa mapenzi yake. Mzigo ninao kamili.
 
wewe jpya lako ni lipi?

kama una uhakika wa kuitwa nakupa ushauri wa anza kujisomea civics ya form one. Wenzako wa zimamoto nilishauli wapitie chemistry ya form one topic za fire &fire extuinguisher waliofatilia wana uhakika walioyakuta wakashindwa kujibu walinipigia hodi kwa PM.

akili za kuambiwa changanya na zako
J.Kikwete
 
Hilo tangazo sio la mwaka huu coz nilirudi tovuti ya uhamiaji kujirishisha. Hakuna sharti la leaving certificates. Asante sana kwa dua njema. Mungu atatenda kwa mapenzi yake. Mzigo ninao kamili.


bahati mbaya sina ujuzi wa kulink ila kuna mdau aliliweka hapa katika uzi huuhuu unaweza ukacheki page ya 3 au 4
 
lazima afanyiwe vipimo na aende depo, depo ni miezi tisa au mwaka mmoja. ukiwa depo ama jeshini kama unavyoita hupewi mshahara Bali unapewa posho kila mwisho wa Mwezi


hapa nimepapenda, vipimo vya nini magonjwa au urefu na ufupi. samahani sitanii nauliza seriuos ndugu yangu, na je vipimo ivyo kabla ujaenda depo au ukiwa depo na kama wanapima magonjwa je ni magonjwa gani hayatakiwi?
 
Naanza kwa maswali yafuatayo!Kwa kawaida mkaguzi msaidizi ni lazima aende jeshini? ni kwa muda gani na anapokuwa jeshini analipwa mshahara? Majibu wakuu pia mwenye maswali zaidi uliza

je albino wanaruhusiwa kuomba kazi izi za idara za usalama sababu sijawahi kuona polisi au mjeshi albino
 
NEWS AND EVENTS

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Kamishna Mkuu wa Uhamiaji anatangaza nafasi za kazi katika Idara ya Uhamiaji. Nafasi hizo ni Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Koplo wa Uhamiaji na Konstebo wa Uhamiaji.

A. MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI (Nafasi 70)


SIFA ZINAZOHITAJIKA
Awe na Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika fani zifuatazo:
Sheria, Uchumi, Biashara, Utawala, Uandishi wa Habari, Ualimu, Usafirishaji, Raslimali Watu, Sayansi ya Kompyuta, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Takwimu, Uchapaji, Uhandisi Majengo na Uhandisi Mitambo.

Awe na umri usiozidi miaka 35


MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
Kusimamia doria sehemu za Mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, Treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwemo vya majini
Kusimamia shughuli za upelelezi, kuandaa Hati ya Mashitaka na kuendesha mashitaka
Kutoa na kupokea fomu mbali mbali za maombi ya Hati za Uhamiaji
Kufanya Ukaguzi wa Mwanzo wa Maombi mbalimbali
Kuagiza ufunguaji wa Majalada ya watumiaji
Kupokea na kukagua Hati za Safari, Fomu za Kuingia na Kutoka Nchini
Kuidhinisha malipo mbalimbali ya huduma za Uhamiaji kwa wanaostahili
Kutunza kumbukumbu za ruhusa za watu wanaoingia na kutoka nchini
Kukusanya, kusimamia na kutunza takwimu za Uhamiaji na Uraia
Kuandaa majibu ya maombi yote ya huduma za uhamiaji yaliyokubaliwa au kukataliwa


B: KOPLO WA UHAMIAJI (Nafasi 100)

1. SIFA ZINAZOHITAJIKA:

Awe amehitimu Kidato cha Sita na kufaulu
Awe na umri usiozidi miaka 30
C. KONSTEBO WA UHAMIAJI (Nafasi 100)

1. SIFA ZINAZOHITAJIKA:

Awe amehitimu Kidato cha Nne na kufaulu
Awe na umri usiozidi miaka 25
D: SIFA ZA ZIADA: KOPLO/KONSTEBO WA UHAMIAJI

Cheti cha Ufundi Stadi (Full Technical Certificate) kwenye fani ya Umeme na Mitambo
Cheti au Stashahada ya Uhaziri (Certificate or Diploma in Secretarial Studies) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali
Cheti au Stashahada ya Kutunza Kumbukumbu (Certificate in Records Management) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali
Cheti au Stashahada ya Takwimu (Certificate or Diploma in Statatistics ) Kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali.
Cheti au Stashahada ya Vyombo vya Majini (Certificate or Diploma in Marine Transportation and Operations) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali
Cheti au Stashahada katika fani ya Uchapaji (Printing)
Ujuzi na Elimu ya Kompyuta na Uandishi mzuri utazingatiwa
Cheti cha Ufundi Makanika,Kozi ya juu ya Udereva na Leseni ya Udereva Daraja C


E. MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA

Kufungua, kupanga na kutunza majalada ya huduma mbalimbali za Uhamiaji
Kuandika Hati mbalimbali za Uhamiaji
Kufanya doria sehemu za Mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, Treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwemo vya majini.
Kusindikiza watuhumiwa wa kesi za Uhamiaji Mahakamani pamoja na wageni wanaofukuzwa nchini
Kufanya ukaguzi kwenye mahoteli, nyumba za kulala wageni na sehemu za biashara.
Kuchapa au kuandika kwa kompyuta barua au nyaraka mbalimbali zinazohusu kazi za kila siku za Uhamiaji.
Kufanya matengenezo/ukarabati wa mitambo na vitendea kazi vya Uhamiaji
Kuandaa na kutunza takwimu za huduma mbalimbali za uhamiaji
F. MAOMBI YOTE YAWE NA VIAMBATISHO VIFUATAVYO:

Nakala za vyeti vya kuhitimu masomo kwa mujibu wa sifa zilizotajwa
Nakala ya Cheti cha Kumaliza Elimu ya Msingi
Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa
Picha mbili (Passport Size)
Barua ya Utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa
G. UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yapitie posta na barua za maombi ziandikwe kwa mkono.

Maombi ya nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji yatumwe kwa:


KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI,
S.L.P. 9223,
DAR ES SALAAM

Maombi ya nafasi ya Koplo wa Uhamiaji na Konstebo wa Uhamiaji yatumwe kwa:


KAMISHNA MKUU WA UHAMIAJI,
S.L.P. 512,
DAR ES SALAAM


Mwisho wa kutuma maombi kwa nafasi zote ni tarehe 27/02/2014





VACANCY ANNOUNCEMENT

The Principal Commissioner of Immigration Services announces vacant Posts in the Immigration Department. Any Tanzanian Citizen with minimum qualifications mentioned hereunder is encouraged to apply:

A. ASSISTANT INSPECTOR OF IMMIGRATION SERVICES (70 Posts)

Qualifications:
Tanzania Citizens aged not above 35 years
Holder of Bachelor Degree or Advanced Diploma from any University or Institution recognized by the Tanzania Government in the following disciplines:


Law, Economics, Business, Administration, Journalism, Education, Transportation, Human Resource, Computer Science, Information and Communication Technology, Statistics, Printing, Civil Engineering and Mechanical Engineering

Duties and Responsibilities:
To supervise patrols along the border areas, sea ports, bus stands, highways, railway stations, business centres and other entry points
To prepare charge sheets and prosecute in court all immigration related cases
To issue and receive various application forms for immigration services
To execute preliminary scrutinization of different application forms
To authorize opening of customers application files
To receive and scrutinize Passports and other travel documents
To authorise collection of government revenues for various immigration services
To keep records of all persons entering or leaving the country
To collect, organize and keep statistics of immigration and citizenship services
To notify customers in writing on the status of their applications


B. CORPORAL OF IMMIGRATION SERVICES (100 Posts)

Qualifications:
Tanzania Citizens not above 30 years of age
Holder of Advanced Certificate of Secondary Education


C. CONSTABLE OF IMMIGRATION SERVICES (100 Posts)

Qualifications:
Tanzania Citizens not above 25 years of age
Holder of Certificate of Secondary Education


D. ADDED ADVANTAGES:

Certificate or Diploma in Law
Computer knowledge and typing
Full Technician Certificate (FTC) in Electricity and Mechanical Engineering
Certificate or Diploma in Secretarial duties
Certificate or Diploma in Records Management
Certificate or Diploma in Statistics
Certificate or Diploma in Marine Transport and Operations
Certificate in Trade Test Grade II, Advanced Drivers Course Grade II and Driving License Class C
Certificate or Diploma in Printing
Certificate or Diploma in Civil Engineering
Certificate or Diploma in Statistics
Duties and Responsibilities:


To conduct patrols along the border areas, sea ports, bus stands, highways, railway stations, business centres and other entry points
To conduct inspections in the hotels, guest houses and other business premises
To issue Immigration forms and information on the requirements for the services sought
To escort immigration accused aliens/citizens in court
To escort deported aliens outside the country
To open and keep customers’ files in good order
To apprehend suspected immigration offenders
To make maintenance and regular service of equipment
To collect, organize and keep immigration related statistics
NOTE: Selected applicants for the posts must attend a one year Basic Immigration Course prior to employment

D. APPLICATION LETTERS MUST BE ACCOMPANIED WITH:

Two recent passport size photographs
Photocopy of Academic Certificates/Trainings
Photocopy of Birth Certificate
Letter of Introduction from Village/Ward Executive Officer or Sheha
Secondary/Advanced Secondary School Leaving Certificate
Primary school leaving Certificate
E. MODE OF SUBMISSION
All applications must be hand written and have to be submitted through Post Office

All applications for the post of Assistant Inspector of Immigration Services should be channeled to:


The Permanent Secretary,
Ministry of Home Affairs,
P.O. Box 9223,
DAR ES SALAAM

All applications for the post of Corporal and Constable of Immigration Services should be channeled to:


The Principal Commissioner of Immigration Services,
P.O. Box 512,
DAR ES SALAAM

Deadline for submission of applications: February 27, 2014.








Wednesday 16th Apr 2014
Others
News and Events
Acts and Regulations
Application Forms
Statistics
Prohibited Immigrants
Information Centre
Photo Gallery
Useful Links
Breaking News
Dear Visitors, Please keep on visiting this site for the Breaking News from the Ministry and Immigration Services Department!

mkuu nkungwe123 check toka kwa post ya vide2014 ambaye ni mdau mwenzetu
jioni njema shortlist kesho wanasema baadhi ya ndugu wa makamishina humu JF
 
Back
Top Bottom