Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,265
- 17,135
Tunaweza lakini kwa uchumi tulionao kwa hivi sasa, kuweza kuumaliza mradi kama huo kwa pesa zetu wenyewe inaweza kutuchukua miaka kadhaa... kwa uchache kumi! Sasa wakati tunajitia kiburi cha kwamba, hata kama itatuchukua miaka 15 kumaliza potelea mbali ili mradi tu tuujenge kwa pesa zetu wenyewe, kwa upande mwingine tunatakiwa kujiuliza, je katika kipindi hicho cha miaka 10+ tutakuwa tumepoteza kiasi gani? I mean, assume Wachina wanamaliza mradi ndani ya miaka 3 na sisi kwa kutumia pesa yetu tunamaliza ndani ya miaka 15... hapa kati kati kuna miaka 12... tufanye miaka kumi ambayo hakutakuwa na mzigo wowote umeingia na kwa maana hiyo hakutakuwa na kodi yoyote iliyokusanywa! Aidha, wakati sie tunataka kujikongoja kwa kuonesha jeuri ya kujitegemea, wapo ambao wata-opt kutumia njia ya PPP kama tunayofanya hivi sasa! Mathalani, Kenya nao wana mradi unaofanana na huu na wao wanatafuta mwekezaji vile vile ambae ataachiwa miaka kadhaa a-operate bandari husika! Hii maana yake ni kwamba, wakati sie tutakuwa tunajikongoja ili kuonesha jeuri ya kujitegemea, baada ya miaka 3-5 competitors wetu watakuwa tayari kwenye game... hadi wewe unamaliza ujenzi, mwenzako tayari ameshajenga credibility kwenye industry... wale ambao ulitaraji wangekuwa wateja wa kwanza kutumia your new port, watakuwa tayari wameshaanza kutumia ya mshindani wako zaidi ya miaka 5 iliyopita!!Kwa maana hiyo sisi watanzania hatuwezi kujenga hiyo bandari yaaani kumpa contract hata mchina akafanya kazi ya kujenga tu hiyo bandari?
Shida inakuwa ni nini hapo?
Huu mradi haujaelekezwa kwenye bandari ya Mtwara coz' lengo ni kuifanya bandari ya Mtwara i-accommodate meli za mafuta na gas! Ikiwa issue za mafuta na gas zitafanikiwa basi bandari ya Mtwara itakuwa busy na shughuli za mafuta na gas! Usisahau kwamba mimeli ya mafuta na gasi ni mikubwa mno... sasa pakishachangamka pale (Mtwara) itakuwa ni vurugu kutaka mizigo mingine nayo ipitie pale pale wakati kuna mimeli ya mafuta na gas imetinga nanga ikichukua mzigo kwa siku kadhaa!!kwanini wasiendeleze bandari ya Mtwara na kuipunguzia mzigo bandari ya Dar, bandari ya Mtwara ndiyo bandari yenye kina cha asili kwa Afrika mashariki mpaka pembe ya Afrika tofauti na bandari ya Dar ambayo kila baada ya muda inachimbwa ili kuongeza kina. Bandari ya Mtwara ni ya asili haihitaji kuchimbwa ili kuongeza kina, waiboreshe hii halafu wajenge barabara yenye urefu wa KM 654 ya kutoka Mtwara kwenda Songea kwa kiwango cha lami. Ni kitu cha kushangaza gari inatoka bandari Dar kwenda Msumbiji ila inapita Custom TRA iliyopo ndani bandari ya Mtwara au ufuta kulimwa Mtwara halafu unapelekwa bandari ya Dar kusafirishwa.
Kwa maana hiyo sisi watanzania hatuwezi kujenga hiyo bandari yaaani kumpa contract hata mchina akafanya kazi ya kujenga tu hiyo bandari?
Shida inakuwa ni nini hapo?
Ndugu, unaijua $10B au unaisikia tu?
Jua kuwa hatuna uwezo huo,hasa kwa sasa hivi, ni pesa nyingi sana.
Hiivi unaweza kumuambia mtu mwenye kipato cha chini,let's say anayelipwa laki 5 kwa mwezi ajenge gorofa la bilioni moja?Jibu ni haiwezekani.
Uchumi wetu hauturuhusu kufanya commitment za $10B. Actually ni faida kwetu wakijenga wachina, na kumiliki kwa kipindi flani, kwani wao ndio kiwanda cha dunia, Meli zote lazima ziende china at one point in time. Sisi kuwa sehemu muhimu ya stratergy yao kunatusaidia kupata market share ya usafirishaji wa maji kwa urahisi zaidi. Kumbuka bandari ni meli.
Hizi ndizo akili nisizozitakaga. Eti $10B nchi haina wala haiwezi kuwa nayo, are you serious??
Kwahiyo unataka kuniambia hii nchi ni wataalam wa ufisadi TU, hatuwezi kujenga bandari wala kiwanda ??
Ukiwa na port nzuri yenye vigezo vyote meli zitakuja haijalishi una meli au huna.
Ndugu,
Usilete siasa, ingekuwa rahisi hivyo, bajeti yetu ya mwaka mzima isingekuwa $5-6B kwa mwaka, Hatuna uwezo huo usilazimishe mambo.
Una mengi ya kujifunza kuhusu uchumi, nakushauri usome vitabu vingi ili kuelewa vitu kama hivi vinavyokwenda na sio kurukia mambo na kutafuta majiibu mepesi kwa maswali magumu.
hizo $10B hatuna na hatujawahi kuwa nazo, unajua foreign reserve zetu zinachezea kiasi gani? purchasing power yetu ikoje?
Kwa uchumi wako huu wa kina makengeza jiridhishe tu kwamba Tanzania haiwezi na haitakaa iweze milele lkn kwa watu makini wanaojua nini wanatakiwa wafanye kama nchi that's not a big deal.
Miaka ya 1980 uchumi wetu ulikuwa sawa na hao wachina, sasa wao walimchinjia mungu mbuzi wakapata uchumi wao ukapaa au.
Hebu panua wigo wa ubongo wako zaidi
Shida yako unataka majibu mepesi kwa maswali magumu.
hizo make-wish thinking, sivyo uchumi au ukuaji wa uchumi unavyokwenda. sasa nani alikudanganya mwaka 1980 uchumi wa TZ ulikuwa sawa na uchumi wa china? Nadhani hii mada iko nje ya uwezo wako, nakushauri usome wanayoandika watu humu upate kujifunza zaidi, sio kila hadithi ya kijiweni inaweza kuandikwa humu.
999, Kimweri,
..mimi nadhani hiyo usd 10 billion inaweza kupatikana, ama kwa mkopo, au kwa kubanana humu ndani.
..lakini kwa upande mwingine nadhani kutumia kiasi kikubwa namna hiyo kwa ujenzi wa bandari peke yake inaweza isiwe busara.
..kwa nchi kama Tz hizo 10 billion inabidi tuzigawe kwenda kwenye umeme, reli, barabara, bandari, etc, na hapo ndipo uamuzi wa kutumia muwekezaji toka China kwenye ujenzi wa bandari unapokuwa na mantiki.
..Kenya wanajenga container terminal Mombasa na wamealika wawekezaji watakaojenga na kuendesha eneo hilo kwa miaka 25. Kwa hiyo tusione kwamba kilichotokea kwa Tanzania ni jambo la ajabu.
..Mimi kama mimi, ningependa wa-Tz tuwe na mradi mmoja mkubwa ambao tutaukamilisha kwa nguvu na fedha zetu wenyewe. Wenzetu wa Ethiopia wana mradi mkubwa wa bwawa la umeme ambao kwa sasa hivi ni fahari ya nchi yao.
cc NasDaz, Sangarara
..kwa nchi kama Tz hizo 10 billion inabidi tuzigawe kwenda kwenye umeme, reli, barabara, bandari, etc, na hapo ndipo uamuzi wa kutumia muwekezaji toka China kwenye ujenzi wa bandari unapokuwa na mantiki.
What Kenya is doing is a petty project not even worth $500M,we can do that anytime, we have actually done that with bomba la gesi at $1B na ushehe.Sio kila wakati Kenya wako Sahihi, na sie tunakosea. Hili la Bagamoyo, ni kitu pekee ninachoweza sema JK amefanya cha heri bila kumungunya maneno...Kenya wanajenga container terminal Mombasa na wamealika wawekezaji watakaojenga na kuendesha eneo hilo kwa miaka 25. Kwa hiyo tusione kwamba kilichotokea kwa Tanzania ni jambo la ajabu.
JokaKuu umeongea vizuri sana kwamba fedha zinapatikana either mkopo au hapa ndani au inaweza ikawa halfhalf(mkopo na hela ya ndani) vyovyote itakavyokuwa.999, Kimweri,
..mimi nadhani hiyo usd 10 billion inaweza kupatikana, ama kwa mkopo, au kwa kubanana humu ndani.
..lakini kwa upande mwingine nadhani kutumia kiasi kikubwa namna hiyo kwa ujenzi wa bandari peke yake inaweza isiwe busara.
..kwa nchi kama Tz hizo 10 billion inabidi tuzigawe kwenda kwenye umeme, reli, barabara, bandari, etc, na hapo ndipo uamuzi wa kutumia muwekezaji toka China kwenye ujenzi wa bandari unapokuwa na mantiki.
..Kenya wanajenga container terminal Mombasa na wamealika wawekezaji watakaojenga na kuendesha eneo hilo kwa miaka 25. Kwa hiyo tusione kwamba kilichotokea kwa Tanzania ni jambo la ajabu.
..Mimi kama mimi, ningependa wa-Tz tuwe na mradi mmoja mkubwa ambao tutaukamilisha kwa nguvu na fedha zetu wenyewe. Wenzetu wa Ethiopia wana mradi mkubwa wa bwawa la umeme ambao kwa sasa hivi ni fahari ya nchi yao.
cc NasDaz, Sangarara
JokaKuu umeongea vizuri sana kwamba fedha zinapatikana either mkopo au hapa ndani au inaweza ikawa halfhalf(mkopo na hela ya ndani) vyovyote itakavyokuwa.
Na hizi zinakuwaga ni project za muda Mrefu may be 10yrs to come tutafanya kitu hiki so tunaanza kujiandaa mapema kwa hiyo mpaka muda huo unafika unakuta maandalizi yalishafanyika shughuli za utekelezaji zinaanza.
Wenzetu wanaplan project za miaka 20-30 ijayo na wanafanya yote hayo ni maandalizi mazuri yanafanyika lkn mwenzangu Kimweri hataki hilo.
Tukiwa na serikali makini hakuna linaloshindikana
Tatizo usichoelewa wewe ni kuwa sio kila project financing iko feasible. Ndio maana kuna ranking agencies. Ingekuwa rahisi hivyo kila maskini duniani angeplani 20-30 years halafu akaenda kukopa mabilioni benki. Kabla ya kukopa lazima uwe na capacity ya kurudisha mkopo, na uwezo wa kuhandle hiyo financing.
Nenda kesho CRDB waoneshe bank statement yako na collaterals zako, lets assume total portfolio yako iwe around 50M, halafu waambie wakupe mkopo wa bilioni 10 za kitanzania, ukimaliza hapo, waletee hadithi za plani za muda mrefu, n,k uone afisa mikopo atakujibu kitu gani.
Kuna uhalisia na ndoto za alinacha.
Simama kama NCHI ya TZ not an individual person.
Mimi nashindwa kukuelewa au sijui huelewi nini au labda unataka kuniambia TANZANIA hatuwezi lolote sisi tusubiri kufanyiwa tu na hao wazungu or wachina na wahindi?
Are we serious kweli??
Are you serious? Ni miaka ya 80 's ipi au ya karne gani ambayo uchumi wa Tanzania ulikuwa sawa na ule wa China? Hivi kweli unaifahamu vizuri historia ya uchumi wa Tanzania ndugu yangu? Hivi kuna wakati ambayo Tanzania ili-suffer kiuchumi kama hiyo miaka ya 80?Kwa uchumi wako huu wa kina makengeza jiridhishe tu kwamba Tanzania haiwezi na haitakaa iweze milele lkn kwa watu makini wanaojua nini wanatakiwa wafanye kama nchi that's not a big deal.
Miaka ya 1980 uchumi wetu ulikuwa sawa na hao wachina, sasa wao walimchinjia mungu mbuzi wakapata uchumi wao ukapaa au.
Hebu panua wigo wa ubongo wako zaidi
Kimweri tuko pamoja sana.Then Hiyo nchi yako ya Tanzania ni nchi maskini, huo mfano nimekupa ili uelewe kuna ndoto za mchana na uhalisia.get a grip.
Kama hatutaki mikopo na misaada, well, i support that stance, then hakuna sababu ya kuparamia au kulazimisha kufanya miradi iliyo nje ya uwezo wetu.
uwezo wa nchi kama Tanzania ni miradi midogo za zaidi hata ya hii iliyokuwepo. Miradi mikubwa mingi tunapigwa boost na hiyo misaada/grants.
Nyerere alipoleta siasa za kujitegemea alikuwa sahihi kabisa, lakini hakuanzisha project za mabilioni zilizo nje ya uwezo wa nchi. Waliko nchi tajiri tutafika siku moja, kama tukifanya kazi kwa bidii, na kuwa na nidhamu.
Ila hatuwezi kuamka siku moja na kutaka kujifannanisha na uchina au marekani.
Hata hizo nchi zenye uchumi mkubwa duniani kuna project hawawezi kuzifanya wao peke yao. ndio maana kuna internatinal financial institutions, private investors etc.
wewe unafikiri wamarekani wanaona raha kupunguza bajeti ya NASA n.k, uwezo.