Maswali kuhusu Bandari mpya ya Bagamoyo

Maswali kuhusu Bandari mpya ya Bagamoyo

Hapa ndio utaona watu wa Tanga na watu wanaotoka Tanga hawana influencetoka walipotaka kumpindua Nyerere

Pesa zilizopelekwa Bagamoyo zilikuwa ziende Tanga...project ilikuwa inaitwa MWAMBANI PORT PROJECT na ilikuwa ni project ya 40 billion usd.

feasibility na kila kitu kilikuwa tayari

wajanja frm BAGAMOYO wakawapiga bao hawa jamaa wa Tanga na wakapata hizo 10 billion usd toka kwa serikali ya china kupitia kitu kinachoitwa EPC na nadhani hawa jamaa walifanya DFBOOT ya mika 40

humu JF hamuwezi kupata habari zaidi kwa sababu watu hawana interest ya kumwaga data kwa kuwa mijadala ya jukwaa hili ni ya chadema na ccm na mangonda na ujunga wakusifiana. hakuna kukata issues wala nini

sioni sababu ya kupoteza muda kuelezea kitu ambacho wote mnajua hatutopata majibu kwa kuwa sirikali inasema ni siri

Timiza wajibu wako mkuu
 
Inasemekana ujenzi wa mradi huu utazinduliwa mwezi July.

Binafsi mpaka sasa hivi sijaweza kupata taarifa za kutosha kuhusu mradi huu mkubwa.

Inaonekana kuna mwekezaji anaitwa CHINA MERCHANTS HOLDINGS INTERNATIONAL ambao ndiyo wadau wakubwa ktk mradi huo.

So far taarifa zote ambazo nimekutana nazo zimeniacha na maswali mengi kuliko majibu.

Kwa mfano, kuna taarifa nimekutana nayo inaelekeza kwamba China Merchants Holdings wataendesha bandari hiyo kwa muda wa miaka 40.

Pia katika mradi huohuo kuna mwekezaji mwingine anaitwa OMAN STATE GENERAL RESERVE FUND ambaye atahusika na eneo huru la kibiashara.

Naomba wenye taarifa zaidi kuhusu mradi huu watueleze. zaidi ningependa kujua nafasi ya serikali ya tanzania, na mamlaka ya bandari TPA ktk mradi huu.

cc Sangarara, salaama, Kimweri, Zitto, laiza, limetumbuka, Nguruvi3, NasDaz, Mdondoaji, Fx Trader, Zitto, Tokyo40, Kibona

Mkuu about two weeks ago nilikua bagamoyo kimsingi maandalizi yapo maana kuna ujenzi wa barabara kutoka pale bandari pia inasemekana wanakijiji bado hawalipwa fidia mpaka leo hii
 
Taarifa niliyonayo mimi ni kwamba, mwambao wote huo inakozungumzwa kujengwa bandari hiyo unamilikiwa na Mtanzania mwenzetu na hao china nani sijui wanapanga hiyo ardhi kwake, na wameishaanza kulipia rent.

Mkataba wa pango uko complicated kidogo sababu uko governed na sharia za China.

watakuja hapa wataalamu wa PPP watakuelezea vizuri.
Hivi mtu unaruhusiwa kumiliki mwambao? ipo siku utasikia mtu anamiliki Mlima Kilimanjaro
 
Taarifa za ndani ni kwamba huo mradi haupo. Hivi sasa ni danadana tu zinapigwa halafu akishaondoka Kikwete au CCM Oktoba ndiyo ukweli utaelezwa.
 
..kwanza kuna wanaosema mradi haupo. kwa uelewa wangu mradi huu upo na serikali ya Tanzania, pamoja na wawekezaji toka Oman, na China, wamekubaliana kwamba July mambo yote yawe yamekamiliki.

..kwamba kuna "mwenzetu" anamiliki eneo litakapojengwa bandari hilo nalo sina uhakika nalo, ila nimepata kusoma mahali Raisi Kikwete akielekeza kwamba wananchi watakaochukuliwa ardhi yao walipwe pesa nzuri. sasa sina hakika kama ardhi aliyokuwa anaizungumzia Raisi ni eneo itakapojengwa bandari au eneo la ukanda wa biashara/viwanda.

cc Atukilia, mdawa, Sangarara
 
Last edited by a moderator:
Maswali ya nyongeza, kwa kuwa maelezo yako hayaja lifafanua hili, je bandari hii itakuwa chini ya TPA au Mamlaka ya Bandari China(MBC)?

Je bandari hii itakuwa mshirika wa bandari zilizoko au itakuwa mshindani?

Je kwa kuwa mizingo mingi ingiayo nchini ya wezekana inatoka China, Wachina hawata pendelea zaidi bandari yao hivyo kufifisha hizi zilizopo tayari?

Je baada ya miaka hii 40 ya uendeshaji wa Wachina Tanzania itakabidhiwa bandari yenye hali gani, miundo mbinu endelevu au magofu?

Je makuli wa Bandari hii watatoka China ua Tz? Maana kuna taarifa kuwa makuli wa China niwa gharama rahisi kuliko wa hapa.

Je....? Ok niache kwanza nitaendelea nikijibiwa haya.

..Thank u X 3.

..Na mimi nina maswali hayohayo ila wewe umeweza kuyaweka kwa ufasaha zaidi.

..KENYA wametangaza tender ya kujenga na kuendesha container terminal ktk bandari ya Mombasa, na wanatafuta mwekezaji atakayemiliki mradi huo kwa miaka 25.

cc Nguruvi3, salaama, Kimweri, Tokyo40, Pasco, Mchambuzi
 
Nyamgluu, share, respect wa boda, atheist, CHAZA,

..mahitaji ya bandari kubwa zaidi ya Dsm yapo.

..kuna utafiti ulifanywa na mamlaka ya bandari TPA ambao ulibainisha kwamba by 2017 au 2018 Tanzania itahitaji bandari kubwa zaidi na mpya.

..kwa hiyo wazo la kuwa na bandari Bagamoyo naamini limetokana na ripoti hiyo ya wataalamu.

..kuhusu Mwambao Port Project, habari zake niliwahi kukutano nazo kwenye mtandao. Nadhani bado mradi huo unatafutiwa wawekezaji. Ila sina uhakika kama utafanikiwa kutokana na ushindani toka bandari ya Bagamoyo. Zaidi, mradi huo unapata upinzani mkali toka kwa wanamazingira.

..Madai kwamba eneo la Bagamoyo linafaa kwa ujenzi wa bandari au la, kutokana na kina cha maji cha eneo hilo, nimekutana nayo hapa kwa mara ya kwanza. Lakini nadhani huyu mwekezaji wa Kichina hawezi kuwekeza pesa yake hapo bila kuwa na uhakika wa kuirudisha.
 
Last edited by a moderator:
Nasema tena huu mradi haupo lakini wahusika hawawezi kutangaza sasa.
China walitaka bandari hiyo kwa maslahi ya kijeshi pia wakakuta wanaingilia mipango ya muda mrefu ya Wamarekani kuweka kituo cha jeshi Tanzania. Wachina na wamarekani huwa hawashindani hivyo Mchina amebwaga manyanga.
Mtakuja kusimuliwa baadae.
 
..Thank u X 3.

..Na mimi nina maswali hayohayo ila wewe umeweza kuyaweka kwa ufasaha zaidi.

..KENYA wametangaza tender ya kujenga na kuendesha container terminal ktk bandari ya Mombasa, na wanatafuta mwekezaji atakayemiliki mradi huo kwa miaka 25.

cc Nguruvi3, salaama, Kimweri, Tokyo40, Pasco, Mchambuzi

Bandari ni meli, hivyo meli zitakazoenda bagamoyo ndio zitakazoamua wateja wake. meli ndogo hazitafaidika kwenda Bagamoyo, kwani ile itakuwa primarily transshipment port.

Bandari ya DSM itaongezeka ufanisi kwa kupunguziwa mizigo, kama vile bandari ya Zanzibar inavyotoa mizigo upesi kuliko Dar. Taifa halitapoteza lolote kwa Bandari ya Bagamoyo kutumika kuliko DSM kwani kote kutakuwa kunaliingizia mapato taifa kupitia kodi, kumbuka pia hata DSM kuna TICTS anaiendesha, na bado tunakusanya mapato ya kodi.

Uhusuiano wa waendeshaji wa Bagamoyo hautatofautiana na uhusiano wa TPA na TICTS. wachina wataamua nanin wamuajiri kama vile TICTS wanavyoamua nani awe staff wao.

Kuhusu kuhakikisha wazawa wanapata ajira zaidi, hili n ijukumu la wizara ya kazi na uhamiaji, na si mamlaka ya bandari.
 
Nasema tena huu mradi haupo lakini wahusika hawawezi kutangaza sasa.
China walitaka bandari hiyo kwa maslahi ya kijeshi pia wakakuta wanaingilia mipango ya muda mrefu ya Wamarekani kuweka kituo cha jeshi Tanzania. Wachina na wamarekani huwa hawashindani hivyo Mchina amebwaga manyanga.
Mtakuja kusimuliwa baadae.

..inasemekana eneo linalofaa kwa masuala ya kijeshi[jeshi la majini] liko ukanda wa kusini, kule ambako Jemedari wa Kijerumani, Von Lettow alikuwa ameficha meli zake za kivita wakati wa vita kuu ya kwanza.
 
Bwana eeh...msinichoshe mimi na mihoja hoja yenu ya maana. Nchi hii mtu mwenye hoja anaonekana ni kundi la kukosa, mwenye husda na wivu.
Acha niende zangu bar nikalipe kodi miye.
 
Bandari ni meli, hivyo meli zitakazoenda bagamoyo ndio zitakazoamua wateja wake. meli ndogo hazitafaidika kwenda Bagamoyo, kwani ile itakuwa primarily transshipment port.

Bandari ya DSM itaongezeka ufanisi kwa kupunguziwa mizigo, kama vile bandari ya Zanzibar inavyotoa mizigo upesi kuliko Dar. Taifa halitapoteza lolote kwa Bandari ya Bagamoyo kutumika kuliko DSM kwani kote kutakuwa kunaliingizia mapato taifa kupitia kodi, kumbuka pia hata DSM kuna TICTS anaiendesha, na bado tunakusanya mapato ya kodi.

Uhusuiano wa waendeshaji wa Bagamoyo hautatofautiana na uhusiano wa TPA na TICTS. wachina wataamua nanin wamuajiri kama vile TICTS wanavyoamua nani awe staff wao.

Kuhusu kuhakikisha wazawa wanapata ajira zaidi, hili n ijukumu la wizara ya kazi na uhamiaji, na si mamlaka ya bandari.

..thanks.

..Kwa hiyo hapa kati ya Mamlaka ya Bandari Tanzania na China Merchants Holdings ni sawa na mahusiano yake na TICTS?

..Umesema Bagamoyo itakuwa transhipment port. Je, Dsm sasa hivi siyo transhipment port? Je, hapo baadaye Dsm itakuwa port ya aina gani? Naomba utupe elimu kidogo katika hili, mimi sina uelewa nalo.

..Mwisho, Je una information zozote zile kuhusu fedha za ujenzi wa mradi huu? Je, aliyekopa ni serikali ya Tanzania au China Merchants Holdings? Pia kulingana na jibu lako naomba utueleze faida na hasara zake. Vilevile utueleze bandari nyingine ambazo zimejengwa kwa mtindo huu utakaotumika hapo Bagamoyo.

..Tafadhali usichoke na maswali yetu.

cc NasDaz, MwanaDiwani
 
Bandari ya Dar es Salaam ni badnari ya kawaida. Transshipment ports ni zile zinazofaulisha mizigo kwenda bandari ndogo za karibu.mfano bandari ya singapore inafanya kazi hii. kwa nini transhipment?kuleta meli 20 africa sio economical kama kuleta meli moja kubwa yenye kubeba mizigo yenye ujazo sawa na meli ndogo 20. halafu vimeli vidogo vinachukulia hapo kwenye bandari kupeleka vibandari vyengine. ofcourse itafanya pia mambo mengine mengi.

Huo uhusiano uko sahihihi.

Hii ni bandari muhimu kuliko zote Africa inayojengwa miaka ya hivi karibuni, hizi ni one in a generation investments kama vile Suez Canal. The government did well to secure this investment. I think this is a BOT type of scheme. Wakirudisha fedha zao after 40 years bandari inakuwa ya kwetu 100%. wanaobeza wanasahau Suez Canal kwa mfano haijajengwa leo wala jana. Investment za aina hii hakuna anayeweza kuzirudisha in 5-10 years,kwa hivi vinchi vyetu maskini.

Ukimkopesha mwalimu wa msingi bilioni moja, jiandae kumdai yeye na wajukuu zake, ndio kilichotokea, hapa TZ ni kama mwalimu wa shule ya msingi, kinyume na hapo jua ni utapeli.

Bandari ya dar ina kazi za kutosha, kama kupokea mafuta,na bidhaa nyengine zinazoelekezwa kwa nchi kama Zambia n.k, infact ingekuwa vema kama Bandari ya dar ika-focus kwenye aina flani ya cargo ili kuongeza ufanisi. Bandari ya bagamoyo itakuwa kama Jalala, hakuna itakachoshindwa kupokea/kutuma.

Sina taarifa nyingi kuhusu financing structure.Ila nina uhakika wahusika wapo na wanafahamu zaidi.
 
Mkuu Kimweri heshima kwako. Wewe ni mmoja wa wanaJF ambao wana michango iliyonyoka kwelikweli. Hebu tunyoshee na hili;

Uwekezaji kama huu wa kampuni ya kichina utakao fanywa hapo bagamoyo port, share holders ni hao wachina peke yao au kuna wengine? Kama kuna wengine ni serikali ya Tanzania au kinanani hawa?
 
Uwekezaji kama huu wa kampuni ya kichina utakao fanywa hapo bagamoyo port, share holders ni hao wachina peke yao au kuna wengine? Kama kuna wengine ni serikali ya Tanzania au kina nani hawa?
 
Back
Top Bottom