alubati
JF-Expert Member
- May 29, 2016
- 5,717
- 12,237
Twende kazi...Bila kuamini kilichotokea alipofika kama hatua tatu tu toka tulipokuwepo aliniitaja jina langu huku akitabasamu na kutukaribia, alitusalimia kwa tabasamu kubwa..huku aliweka mikono yake mabegani kwetu kulia na kushoto huku tukitembea kuelekea nyumbani kwake. Alitutambulisha kwa mkeo na watoto wake 2, Huyu CEO hakuna mzee hapana ni kijana tusema wa miaka 35 - 40 hivi nafikiri alipata cheo hiki kwa werevu wake alionao.
Alituomba tupate bites kidogo na drinks ila tulikataa tukamwambia tuna jambo kidogo tumekuja kushare na yeye na si wakaaji - lakini wapi alitushawishi hadi tukapata hizo bites na soft drinks... so wakati nataka kuanza kumweleza jambo letu lilolotupeka hapo yeye akadaikia akasema " I know what you want to tell me, please come to my office tomorrow morning 9 am", akakataa kata kata tusimwambie kitu bali tufike ofisini kwake hiyo kesho.
Tulimazia bites zetu na vinywaji na kisha tukaaga na kuondoka, alitusindikiza kadi nje, akamwambia dereva wake atufikishe hadi makwetu...akatuaga kwa kutumbia " Ok we meet tommorow" cheers!!
Ndani ya gari mawazo mengi, hiyo kesho anakwenda kutuambia nini ambacho asingetuambia hapa hapa, nikakumbuka tunakwenda tena kukutana na line manager wetu maana huwezi kuingia ofisini mule bila wao kujua. nikafiri namna wafanyakazi wenzetu wanakavyotuchukulia maana wote sasa washajua kwamba tumeshatimuliwa kazi. Mawazo haya yalinizunguka kwenye fikra zangu nafikiiri hata mwenzangu alikuwa akiwaza hivyo hivyo kwamba huenda tukawa tumelikorogoa zaidi kwenda kuaibika huko. Nikakumbua wazo na mwenzangu kwamba tungeamua kuachana na haya mambo ya msamaha tukajali maisha yetu.
Gari ikafika mitaa ya sinza tukashuka, tukamshukuru dereva - hapo tukaagana na mwenzangu pia ili sasa kesho tukutane ofisini kwa CEO saa tatu asubuhi... Kwangu usiku ulikuwa mfupi, sikutana asubuhi ifike mapema maana nilihofu ni nini kinakwenda kutokea hiyo kesho, wazo la kutokwenda tuliona halitakuwa na uungwana cha msingi twende tu tukajue ni nini hasa. Tulijua kwamba kama kufukuzwa tumefukuzwa sasa kinachokwenda kutokea yawezekana ikawa ni kudhalilishwa mbele ya staff wote wa kampuni.. Usingizi ulinipitia kama kipanga.. nafikiri kwa sababu ya uchovu wa mawazo..