Maswahibu yanayomkuta Halima Mdee yalinikuta na Mimi, tofauti tu yeye ni Senior Mimi nilikuwa Junior

Yes, NBA huwa wana categories za mishahara, basing on performance, age, accomplishments, markets nk.

Nadhani hiyo aliyosaini LBJ ni maximum kwa category yake.

AD pia kasign ya miaka 5, USD 190m.
Hivi hzo pesa zote zinaingia kwnye account au ndo kuna mapayee, load board, nssf, na kodi ya kitanda?
 
Ni story nzuri sana ila iko na evil intention subirin mwisho wake
 
...tunaendelea tulipoishia...

Jamaa yangu alifika asubuhi saa tatu, tulianza mjadala moja kwa moja - mjadala ulikuwa mgumu na fikirishi mno - Hoja mezani zilikuwa Je twenda kuomba msamaha au lah? Je kuna uhumimu gani au faida gani tutapata endapo tutaomba msamaha? Je ni hasara ama faida endpo hatutakwenda kuomba msamaha ? Je msamaha wenyewe ni wa kurejeshwa kazini ama ni wa kutusafisihia tu CV zetu zilizochafuka? Je ni nani tunakwenda kumwomba msamaha huo, ni CEO ama ni line manager wetu?

Tulivutana mno, mwenzangu alishauri tuachane nao na maisha yaendelee kwamba hakuna haja ya kumpigia magoti mwanadamu, sisi bado vijana na tuna future kubwa mbele yatu ukizingatia kozi tulizo soma zina uhitaji (market) kubwa. Mimi nani nilisimamia msimamo kwamba ni sawa anavyopendekeza ila umuhimu wa kusafisha majina yetu ni mkubwa mno kwa maana kokote tukakapokwenda tutaulizwa previous job reference, tumefanya kazi wapi na wale watu wanaotaka kutuajiri watahitaji kupata fununu juu ya tabia zetu na utendaji wetu wa kazi.

Mjadala ulikwenda hadi alasiri, tunasikia njaa tukaamua tutoke kwende pale Rose Garden, si mbali sababu wote tulikuwa tunaishi Sinza na kwa wakati huo kiwanja hicho kilikuwa ndiyo makutano ya hasa vijana kubadilishana mawazo huku walipata chakula... Tulikaa wenyewe tu ili tumalizie mjadala wetu na kabla ya siku kuisha tuwe na msimamo mmoja.

Baada ya chakula tuliendelea na mjadala huku tukigonga glass moja moja tukipeana matuamani ambayo ki ukweli hayakuwepo, mwishoni tukaafikiana twende tukaombe msamaha kwa CEO kesho yake na si kwa line Manager wetu sababu kuu kwamba yeye ndiye aliyelishughulikia jambo letu toka mwanzo - na msamaha tunaokwenda kuomba si wa kurudishwa kazini hapana ila tu ni wa kusafisha CV zetu ili tupate reference nzuri endapo zitahitajika na waajiri wengine. Hoja ya mwisho ilikuwa tunakwenda kwa CEO ofisini kwake ama nyumbani kwake? hapa napo tulivunata mno, kwa kauli moja tukaafikiana twenda nyumbani kwake badala ya ofisini - twende kama vijana wake..tuliona ni rahisi kumpigia magoti CEO kuliko line manager wetu. Tuliagana pale mida ya saa mbili usiku kila mmoja akienda getoni kwake kupumzika.

Inaendelea.......
 
Mkuu unatusumbua

Sasa kuandika vipande vifupi hivyo ni kutesena,
Ukizingatia story tamu

Sasa ni bora umalize yote watu tupate mkate mzima???
 
Kesho ikafika na jioni ya saa 11 mwenzangu alifika kwangu, tulipanga tuondoka mida hii ili walau tuwahi kufika kwa CEO mida ya saa 12 na nusu ama saa moja moja hivi - CEO alikuwa anaishi Upanga kwa hiyo tukaanza safari yetu toka sinza mida hiyo. Tulifika Upanga karibu na nyumbani kwake saa 12 kasoro, tukawa pale nje kwa mbali kidogo tukipiga soga ili tuhakikishe kafika then ndiyo twende. Kufika saa 12 unusu tulianza safari ya kwenda getini kwake, kuna walinzi pale lakini tukajipa matumaini hawawezi kutuzuia maana tutasema sisi ni wafanyakazi wa ofisini na tuna jambo la muhimu la binafsi la kumwambia (Personal issue).

Tulifika pale tukajieleza kwa mlizi, akatuambia tumsubiri huko huko nje .. alikwenda moja kwa moja ndani... sasa nikawa na na mawazo fikirishi kwamba hivi alimjibu hataki kuongea na sisi tutasemaje? ama akaja akatufokea mbele ya walinzi hawa? au akaamua kutuchukulia hatua kwamba tumekwenda kumsumbua nyumbani kwake? nikakumbuka wazo la mwenzengu kwamba tungeachana na haya mambo ya kuomba msamaha maana yanaweza kutuletea mambo mengine tena.

Wakati natafakari mara namuona CEO pamoja na mlinzi wanakuja main gate tulipokuwepo, aisee nikahisi sasa mbivu na mbichi ndiyo hiii - kwa sasa ningetumia jina la "Mwana kuli-find....." Kwa mbali tulijaribu kusoma sura ya CEO maana kwa mwanadamu unaweza kusoma sura ukajua lililomo moyoni kwako kabla....wakasonge karibu nasi......mwili wangu ni kama ulipata ganzi hivi..
 
Mkuu unatusumbua

Sasa kuandika vipande vifupi hivyo ni kutesena,
Ukizingatia story tamu

Sasa ni bora umalize yote watu tupate mkate mzima???
mkuu naandika huku nafanya kazi za wenyewe - kuwa mvumilivu.
 
Bila kuamini kilichotokea alipofika kama hatua tatu tu toka tulipokuwepo aliniitaja jina langu huku akitabasamu na kutukaribia, alitusalimia kwa tabasamu kubwa..huku aliweka mikono yake mabegani kwetu kulia na kushoto huku tukitembea kuelekea nyumbani kwake. Alitutambulisha kwa mkeo na watoto wake 2, Huyu CEO hakuna mzee hapana ni kijana tusema wa miaka 35 - 40 hivi nafikiri alipata cheo hiki kwa werevu wake alionao.

Alituomba tupate bites kidogo na drinks ila tulikataa tukamwambia tuna jambo kidogo tumekuja kushare na yeye na si wakaaji - lakini wapi alitushawishi hadi tukapata hizo bites na soft drinks... so wakati nataka kuanza kumweleza jambo letu lilolotupeka hapo yeye akadaikia akasema " I know what you want to tell me, please come to my office tomorrow morning 9 am", akakataa kata kata tusimwambie kitu bali tufike ofisini kwake hiyo kesho.

Tulimazia bites zetu na vinywaji na kisha tukaaga na kuondoka, alitusindikiza kadi nje, akamwambia dereva wake atufikishe hadi makwetu...akatuaga kwa kutumbia " Ok we meet tommorow" cheers!!

Ndani ya gari mawazo mengi, hiyo kesho anakwenda kutuambia nini ambacho asingetuambia hapa hapa, nikakumbuka tunakwenda tena kukutana na line manager wetu maana huwezi kuingia ofisini mule bila wao kujua. nikafiri namna wafanyakazi wenzetu wanakavyotuchukulia maana wote sasa washajua kwamba tumeshatimuliwa kazi. Mawazo haya yalinizunguka kwenye fikra zangu nafikiiri hata mwenzangu alikuwa akiwaza hivyo hivyo kwamba huenda tukawa tumelikorogoa zaidi kwenda kuaibika huko. Nikakumbua wazo na mwenzangu kwamba tungeamua kuachana na haya mambo ya msamaha tukajali maisha yetu.

Gari ikafika mitaa ya sinza tukashuka, tukamshukuru dereva - hapo tukaagana na mwenzangu pia ili sasa kesho tukutane ofisini kwa CEO saa tatu asubuhi... Kwangu usiku ulikuwa mfupi, sikutana asubuhi ifike mapema maana nilihofu ni nini kinakwenda kutokea hiyo kesho, wazo la kutokwenda tuliona halitakuwa na uungwana cha msingi twende tu tukajue ni nini hasa. Tulijua kwamba kama kufukuzwa tumefukuzwa sasa kinachokwenda kutokea yawezekana ikawa ni kudhalilishwa mbele ya staff wote wa kampuni.. Usingizi ulinipitia kama kipanga.. nafikiri kwa sababu ya uchovu wa mawazo..
 
Back
Top Bottom