DAWASA; Idara ya fedha iboreshwe (department of finance), kwakua inanyanyasa na kudhulumu Watumishi wa DSWASA katika malipo na stahiki zao

TOG

New Member
Nov 24, 2022
4
4
Nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

HII NI BARUA YA WAZI KWA DAWASA na KWA MAMLAKA HUSIKA.

IDARA YA FEDHA/Ofisi ya Finance (DEPARTMENT OF FINANCE) YA DAWASA Inayoongozwa na Mkurugenzi mhe. Sais Kyejo, ni Idara ambayo Inanyanyasa sana Watumishi wa Dawasa, Na kuwadhulumu Malipo ya watumishi hao.

Idara hii ya Fedha inabidi ifanyiwe Marekebisho na Maboresho ya kina, hasa katika system za Ulipaji wa Malipo na Stahiki za Watumishi wake.

Changamoto na Tatizo hilii, CEO aliyepita (Eng. Cyprian Luhemeja) na CEO wa sasa Hivi mhe. Kiula Kingu, wameshapeta taarifa ya Tatizo hili, lakini hadi leo, Tatizo hili la Malipo bado lipo pale pale.
Na Hatujui lini CEO wa sasa hivi ataanza kulifanyia kazi.

Watumishi wa DAWASA WANALALAMIKA saana kuhusu malipo na stahiki zao za malipo ambazo zinatakiwa kulipwa na office ya Finance, yaani kwa DF.

MATATIZO HAYO NI Kwamba;
1. Ofisi ya Finance hailipi malipo kwa wakatii, na ata kama wakifanya malipo hususani ya baadhi staffs wa DAWASA, Malipo na Stahiki zao yanacheleweshwa ata zaidi ya Miezi Kumi 10.

2. Ofisi ya Finance inafanya malipo kwa Upendeleo na mwa Ubaguzi sana.

Hapa unakuta Mkurugenzi wa Fedha anaamua kulipa malipo na Stahiki za Wafanyakazi kwa Upendeleo, aidha kwa Undugu, au kwa Kujuana. Haswa haswa unakuta, Mkurugenzi huyu ana fanya Malipo Mapema hasa ya Watumishi ambao Mkurugenzi huyu alikua anafanya nao kazi katika Shirika la Dawasa (kabla ya Dawasa halijaungana na Dawasco mwaka 2018).

Hii ina maana ya kwamba Mkurugenzi huyu wa Fedha, akigundua tu kua wewe ni Mtumishi ambae ulikua nae Dawasa, kabla ya kuungana na Dawasco, basi malipo yako atakufanyia mapeema saana bila ata Kumuomba omba na kumnyenyekea.

Swali kwa CEO wa DAWASA..
je, NI kwanini kuna upendeleo kama huo??
Je,, kundi la watumishi fulani ndio la Muhimu saana kuliko watumishi wengine??

Ifahamike ya kwamba, MALALAMIKO YA WAFANYAKAZI hawa wa Dawasa ni MEENGI MENGI SANA ndugu CEO. Please, elewa hilo.

Hivyo basi, wewe CEO ( mhe. Kiula Kingu) ndio kimbilio letu, wewe kama Accounting Officer. Tunaomba utusaidie na kuFacilitate haki za watumishiii, katika malipo yaoo ya Pending.

Ndugu CEO mhe. Kiula Kingu, wewe kama Accounting Officer, tunaomba ulisimamie Shirika hili na uwape maelekezo mahususii ofisi ya DF, kua ianze kufanya malipo ya watumishi woote ambao madokezo yao yapo pending zaidi ya Miezi Sita (6).

Aidha Madokezo yao yawe yamefika ofisi ya Finance aidha kwa njia ya hardcopies au kwa Njia ya mtandao uwe wa E-office, please TUNAOMBA uFacilitate kua yalipwe ontime na mapema, kwani tunaamini kila mtumishi ana haki sawa na anapaswa kulipwa Stahiki zake kwa Wakati.

Tunafahamu kua, Mkurugenzi wa Fedha anatabia ya kusema sababu ya kua labda.. i) Dokezo la Hardcopy halionekani, au ii) system ya e-Office ni mbovu.

Tafadhali mhe. CEO, usikubaliane na hizi sababu za huyu Mkurugenzi, kwani Watumishi tumechoka kuambiwa hizo sababu, huku ukiangalia watumishi wengine wanalipwa malipo na Stahiki zao mapema. Na huku watumishi wengine wakisubirishwa ata zaidi ya Miezi 6.

USHAURI;
1. DAWASA, tengenezeni mfumo mzuri wa malipo katika Ofisi ya Finance. Mfano, dokezo la malipo ya wafanyakazi likianza kuingia ndio hilo hilo lianze kua la kwanza kulipwa, yaani (FIRST IN - FIRST OUT) unless kuwe na emergencyyy katika mambo ya operations & Maintanance.

DAWASA, TENGENEZENI SYSTEM YA MALIPO VIZURI KAMA MNAVYOTENGENEZA SYSTEM ZINGINE KATIKA UTENDAJI KAZI. Na pia Muende Mkajifunze katika Taasisi zingine ambazo zipo katika Mfumo wa ISO.

2. Management, EXCOM ya DAWASA Na Bodi ya DAWASA, ikiongozwa na Rtd. Gen. D. Mwamunyange.
Sisi watumishi wa Dawasa, tunaomba muache kujipendelea wenyewe tuu, na bali Muanze kujali Pia Maslahi ya Watumishi wenu, haswa wale wa chini ambao hawana wa kuwasemea.

Tunaomba msimamie Usawa na Haki kwa Watumishi woote bila Upendeleo.

Tafadhalini saana, tunaomba hilo.
Mtusamehe sana kama tumewakwaza. Asanteni, na Mungu awabariki nyoote.
 
Back
Top Bottom