Rooney
JF-Expert Member
- Jan 16, 2015
- 3,782
- 3,909
Congrats mkuu na usimuliaji mzuri sana.Hitimisho:
Tulitembea hadi ofisi ya Finance Mananger huku yeye akiwa katangulia - alikuwa mzee wa hekima wa age kama 55 - 60 hivi, tuliingia tukaketi pia baada ya muda Operation Manager na yeye akaingia ndani, hatukuwa na wasiwasi tena maana kama msahama tulishapata toka CEO haya yanayofuata si ya hatari tena.
Finance akaanza - Kama mlivyosikia kwa CEO wetu, leo asubuhi kabla hamjafika tulikuwa na kikao cha uongozi kwa hiyo haya yote ntakayoyasema tulishayafanyia maamuzi tayari ila tulisubiri mfike ili tuyabariki.. sasa sitaki kurudia hayo yote yaliyotokea kwenu tangu mwanzo hapana, waungwana na wasomi huwa wana focus yaliyo mbele yao na hii ndiyo kazi yangu mimi na mwenzangu hapa.
Kwanza kabisa PONGEZI nyingi sana nazitoa kwenu toka kwa kampuni yetu kwa kutuletea mteja ambaye kwa tetesi tulizopata alikuwa afunge mkataba na kampuni nyingine siku chache kabla ya ninyi kufanya mazungumzo na yeye, ila kwa weredi wenu mmeweza kumshawishi na mmetuletea project kubwa kama hii Big Up kwenu. Muda huo nilikuwa naendeea kuchekea tumboni...
Akaendelea Pili kampuni yetu pamoja na hayo yote imeamuwa kuwazawaidia ajira MPYA...... kwa muda mrefu tulikuwa tuna mpango wa kufungua tawi letu Arusha, ila tulikuwa tunakwamba kidogo kwa hiyo tukawa tunaendelea kuwatumia mawakala - sasa napenda kuwajulisha kwamba mmechaguliwa ninyi wawili kwenda kufungua tawi hilo ambalo kwa kuanza litashughulika na kazi za Sales / Marketing pamoja na Technical na viongozi mtakuwa ni ninyi.
Akanitaja mimi ( nitakuwa Head wa Marketing / Sales) na mwenzangu atakuwa upande wa Technical. Kwa sababu position hizi ni kubwa na ninyi hamna uzoefu mkubwa basi mtafanya orientation kwa wiki mbili na mabosi wenu wa zamani yaani Operation Manager na Sales Manager na mkiwa huko Arusha mtatimiza majukumu yenu na kuriport moja kwa moja kwa CEO. Kwa hiyo kwa wiki mbili hizi mtafanya kazi hapa bega kwa bega na hawa watu ili mjue nini majukumu yenu mapya... Sambamba na hilo kikao cha leo kimeamua kuwapa 5% ya thamani ya projet nzima kama asante kwenu.
Muda huo nilibakia nimeduwaa siamini kinachoendelea pale, jamaa yangu ndiyo kabisaa alikuwa mbali, nilishtuka wakati anasema " I think your comfortable with these positions in front of you right? nikashtuka kidogo nikasema Yes, na mwenzangu Yes.
Operation Manager naye akasema kuwa kwa wiki hizi mbili zijazo tutafanya kazi naye pamoja na yule wa Sales (Building capacity) kabla hatujasafiri kwenda kwenye majukumu mapya.. Pia pamoja ya yeye tutasimalia hii Project nzima kuhakikisha inafanya kazi kama ilivyotazamiawa. Walisimama wote wakatupa hage la nguvu la Hongera na kututakia mafanikio mema... Tulisimama na kuondoka, ili kesho yake tuanze rasmi majukumu hayo mapya ya orientation.
Tulitoka, wakati natoka nilihisi miguu nyepesi sana, yaani siamini kama kweli yametukuta haya, tulifika reception tukaaga - dada aka smie na kutumbia Hongera... tulitabasabu sababu tunamjua. Tulifika nje ya office pale wawili wote tuliangaliana na kukumbatiana wa furaha kubwa, tukaagana ili tukapumzike baada ya kazi ngumu ya siku tatu mfululizo. Nilifika nyumbani nilipiga magoti kumshukuru Mungu wangu kama kawaida yangu kwa yote mema aliyonitendea kwa kutujaza Hekima mpaka kumelimaliza jambo letu salama.
Tulianza orientaion yetu vizuri, tukawa tunaingia kwenye Management meeting..., kule tukaanza kujua na kujadili future focus ya kampuni, financial, Sales na Technical strategies etc... Baada ya wiki mbili tulipata ile 5% yetu - pesa nyingii sana... tuliaga na kwenda Arusha kuanza kazi. Tulifanya kazi yetu vizuri kule Arusha huku tukireport moja kwa moja kwa CEO, na huko ndipo nikakomaa kwenye idara zote za mauzo na ufundi - pamoja na mwenzangu tukajifunza kufuata MISINGI ya kazi - Taratibu zilizopo na kutii mamlaka na kufuata itifaki.
Poleni kina Mdee, mimi nilivuka kwa style hii - ninyi nafikiri bado mna nafasi kubwa ya kusamehewa kama kweli mlikuwa na dhamira ya kweli ya KUJENGA badala ya KUBOMOA, Sisi mlango ulifungwa ila ukafunguliwa tena kwa stle hii ya kipekee - bado naamini mna NAFASI.
-------------------------------- END ---------------------------------
Be blessed.