jouneGwalu
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 2,687
- 1,782
Ili tuondokane na miji holela
lazima kuwepo na nyumba za bei nafuu
watu wawe discouraged kujenga wawe encouraged kununua au kukopeshwa cheap houses..
na serikali iache kupimia watu viwanja,badala yake ipimie makampuni maeneo yajenge nyumba kwa wingi...
Labda swali la Msingi, tunahitaji kufanya Land reclamation Tanzania?
Kwa nini wameenda kujifunza reclamation kama hatuihitaji?
Anna Tibaijuka mbona uko kimya kuhusu mpango wako wa kuiendeleza Kigamboni?
Una lipi la kutuambia sisi wakazi wa Kigamboni, maana kimya kimetanda sasa na hatujui kinachoendelea.
WanaJF
... WaSingapore wamehaidi kutusaidia katika ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni. ......
View attachment 97055
Mama Tibaijuka
Mhe,
Naumia sana napoona uwezo wako wa utendaji,matarajio yangu yamekuwa tofauti.
Ipo kazi kubwa ya mipango mji inayotakiwa kufanyika Tanzania,wewe umeona hilo tu,ili mradi upate kibali cha mji mpya kigamboni.
Tafadhali nitakuona wa maana japo ukizungumzia master plan ya mwabupande
Tengeneza City in the forest,academic city,tourist city na kadhalika......
Acha ushabiki wa kisiasa,kuwa mtendaji wa fani yako.
kama atakujibu hizi nondo nitaomba nipigwe ban ya 24 hours
Hongera mama, kazi ya mikono yako tunaiona.! Jitahidi kwa nafasi yako watanzania wote tuko nyuma yako..!
WanaJF
Nilikuwa mmojawapo wa viongozi tulioandamana na Mhe Rais katika ziara yake ya majuzi nchini Singapore. Ninawaletea sehemu ya Master Plan ya mji wao mpya unaojengwa kutokana na kuokoa ardhi baharini (reclamation). Unaona kila kipande cha ardhi mpya kimeshapangiwa matumizi yake na kuwekewa malengo ya majengo yanayotakiwa.
Kupanga ni kuchagua. Kunahitaji nidhamu na hakuna mchezo wala utani. Huwezi kuwa na mji uliopangwa kama unapenda na kuendekeza uholela na vurugu (chaos). Kinachotakiwa ni kushirikisha wadau wote kupanga malengo na viwango baada ya kupata maoni ya wataalam. Wanaoarithirika na kulazimisha kuhama kupisha maendelezo mapya wanalipw fidia stahiki na endelevu.
Anayedai vinginevyo si msema kweli. WaSingapore wamehaidi kutusaidia katika ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni. Ninakaribisha maoni yenu hasa nyie mlio nje na mnaishi katika miji iliyopangwa? Je uholela unavumiliwa au kuendekezwa? Tupe habari.
View attachment 97055
Mama Tibaijuka
na hii ndio plani ya miji ya Tanzania, sasa mama kwa nini angalau usiunde vikosi jamii kwenye kila kata kama mfano inavyoanzishwa vikundi vya polisi jamii vitavyohakikisha kuwa kila kiwanja kina access the barabara na kuweka kipimo cha chini cha kiwanja. hamuwezi kukaa mnajivunia miji ya wenzenu huku yakwetu inazidi kuhabirika
Land reclamation ni kwa wale wasio na ardhi kama hao Singapore na Uholanzi, sijui ina apply vipi kwa nchi kama Tanzania ambapo Makazi na Kilimo havifiki hata 30% ya nchi nzima!!