Yaani ni watu wa ajabu sana hawa wajamaa mji wa dar wameuaribu vyakutosha pengine si chini ya huyu mama lakini kwakweli kero ni kila mahala sijui ni nani ambae yupo responsible kwenye mgao wa ardhi na kutoa vibali vya majengo.Mimi nilishagawahi kuuliza kazi ya wizara ya ardhi na makazi ni ipi kama tuna slums kama Mwananyamala Kisiwani na sehemu zingine kama hizo ambako watu wanaishi kwenye vijumba vya udongo.
Mimi mawazo na maoni yangu ni
1. Endelezeni huo mji wa Dar es Salaam kwanza uwe wa kisasa kwani unatia aibu hasa mvua ikinyesha.
2. Tumieni huo msaada kuendeleza miji mingine mipya kwani kigammboni tayari mna kila kitu in place.
Mengine naona ni siasa na ufujaji wa pesa tu hapo tutakuwa na mi masterplan kibao kwenye makabati.
Pole na kazi mama Tiba, lakini pia si vibaya ukajibu tuhuma zifuatazo kuondoa wingu juu ya mradi huu, Mnamo tarehe 7/December 2012 inasadikika wewe mheshimiwa waziri ulisafiri kwenda nchini Thailand ambako ulikutana na wakuu wa kampuni kutoka China kusaini mkataba wa ujenzi wa mji kisasa wa Kigamboni. Mheshimiwa kwa mujibu wa vyanzo mhimu wewe utapata 3% kama aksante kutoka kwenye kampuni hii kutoka nchini china?
Pia kuna lawama kutoka kwa wadau wakuu ikiwemo wabunge na madiwani ambao ni wawakirishi wa wananchi hukuwashirikisha katika maamuzi juu ya mkataba huu na mradi kwa ujumla.
Mwisho tungependa kujua ni lini zabuni ya ujenzi wa mji wa kigamboni ilitangazwa kwa mujibu wa Public Procurement Regularity Authority-PPRA, ni kwa kupitia mtandao gani au gazeti gani la hapa nchini au nje ya nchi ilitangazwa (International Competitive Procurement-ICP) ili tujirishe kuwa kulikuwa na uwazi katika diri hili. kwa mujibu wa PPRA thamani ya mradi huo hauwezi kuwa Single source au International shoping. Tunaomba kujua sisi wananchi wa kawaida.
Labda swali la Msingi, tunahitaji kufanya Land reclamation Tanzania?
Kwa nini wameenda kujifunza reclamation kama hatuihitaji?
Mji wa Dar es Salaam hauendelezeki, ulishaharibiwa na kuvunja nyumba ni kutakana ubaya. Ulimwenguni mwote miji ya zamani inaachwa kama ilivyo, kinachofanyika ni kujenga miji mipya. Wazo la kujenga mji mpya wa Kigamboni ni ni jambo jema, lakini tatizo ni ufisadi. Kuna watu pale watataka kujenga nyumba wanavyoona vema wao, na kwa sababu ya nguvu ya pesa, hawatafanywa lolote. Chezea hela wewe kwa viongozi wetu
Ni matumaini yangu kuwa huyu Mama atarudi hapa kufafanua masuala mbalimbali yaliyotokana na hoja aliyoileta hapa jukwaani. Vinginevyo, atakuwa hana tofauti na kina Mwigulu Nchemba na Juma Nkamia.
Tatizo moja kubwa la hawa viongozi wetu wakienda nje ya nchi wanakuwa kama watoto wadogo! Wameona mji wa Singapore ulivyojengeka wameupenda. Badala ya kukaa chini na kujiuliza ni nini haswa siri ya hayo maendeleo? Wanakimbilia kusema na sisi tunataka mtutengenezee master plan. Hawajajiuliza hawa tu wana taratibu au sheria gani zinazofanya miji yao ikue kwa mpangilio. Kusema ukweli, kitu anachopendekeza Mheshimiwa wetu ni tusi kubwa kwa wasomi wetu wa pale Ardhi. Kwani, huitaji watu wa Singapore wakutengenezee master plan. Na wakati mwingine watu local wanaweza kuwa wazuri zaidi kwa kazi hiyo kwani wanaijua culture yetu kwa undani.
Mwalimu Nyerere, aliwahi kusema ya kuwa maendeleo sio lele mama bali ni mapambano. Ni lazima viongozi wetu wajue ya kuwa maendeleo sio kitu cha siku moja, na kinahitaji mipango madhubuti ili kukifanikisha. Na wakati mwingine Kiongozi husika anaweza hasifaidike au kupata sifa kwa kile alichokianzisha. Kama kweli Mama Tibaigana anataka akukumbukwe basi inabidi afanye mabadiliko ya kweli katika wizara ya Ardhi. Kama watu na wafanyakazi wa wizara walidharau master plan ya Mbezi Beach na kuichakachua, nini kinachomfanya afikiri ya kuwa awataichakua ya Kivukoni?
Niliwahi kuongea na rafiki yangu mmoja ambaye nu muhandisi wa maji taka kwenye mji mmoja mkubwa huko Marekani. Aliwahi kuniambia kuhusu gharama za kujenga mabomba ya maji machafu (drainage system) zilivyo juu. Nilimwuliza kwa nini gharama zinakuwa juu kiasi hicho? Aliniambia wanapo-design ukubwa wa pipe wanajaribu kukadiria population ya hiyo sehemu miaka hamsini ijayo. Nikamwuliza kwa nini mnafanya hivyo? Alisema ni kweli gharama zinaweza kuonekana kubwa lakini ni rahisi kufanya hivyo kuliko kubadilisha hayo mabomba baada ya miaka kumi. Na huu ni mmoja wa mfano mdogo wa jinsi wenzetu wanavyofikiria mbali. Ni maswali kama haya inabidi tujiulize kabla ya kuomba master plan.