Kikwete na CCM wanaliaibisha Taifa. Anatumia ikulu vibaya.
Iweje Rais atumwe na Mwanamke, ambaye siye mkewe kumuita msanii kwenda Marekani?
Mwezi wa sita mwaka huu, Mwanamke mmoja anayeitwa Loveness Mamuya, alikuja pale Bungeni Dodoma. Tukiwa wana CCM kadhaa, alituelezea jinsi Rais Kikwete alivyomteua kuwa mwenyekiti wa CCM-DMV huko Marekani. Vigezo, anajua yeye mwanamke na Kikwete. Mwanamke huyu aliendelea kuelezea ombi lake kwa Rais la kumlepeleka msanii Diamond marekani katika ufunguzi wa Tawi la CCM.
Mnakumbuka wiki jana, magazeti tofauti pamoja na ya UDAKU, yaliandika Rais alivyomwalika msanii huyo (Diamond) Ikulu na kumpa kazi maalum nje ya nchi. Je ni vibaya kuhoji ni kwanini Rais asifanye kazi za Kitaifa hadi kuingilia mambo mengine ya upromota? Mbona asingemwachia msaidizi wake? Kwani Waziri wa Michezo, Nape Nnauye wasifanye hizo kazi za U-promoter? Kwenda kufungua tawi la watu hamsini, wakati hata Matawi vijijini yenye watu 1000 na zaidi rais hahusiki?
Ikulu ni taasisi takatifu katika nchi. Ni taasisi inayostahili heshima zote. Ikulu yetu imegeuka kuwa pango la walanguzi, wanyang'anyi, wauaji wa Mabwepande, mapromoter, na wapokea suti. Ikulu imegeuka kuwa sehemu ya kuuzia rasilimali zetu n.k. Mbona taasisi ya Rais imeshuka hadhi kiasi hiki?
Hon: Member of Parliament (CCM)