Ruby: Nilikuwa nalala kwenye kibaraza cha Diamond

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
352
Reaction score
770
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ruby, kupitia kipindi cha wasafi fm (the switch) tarehe 24 august, amefunguka kuhusu maisha magumu aliyopitia wakati akipambana kutafuta kutoboa kwenye tasnia ya muziki, ikiwemo kufikia hatua ya kulala kwenye kibaraza cha nyumba ya msanii mwenzake, Diamond Platnumz.

Ilikuwa ni mahojiano maalum (interview) ambapo Ruby alikuwa akieleza safari ya maisha yake ya muziki, changamoto alizopitia, na jinsi alivyopambana kujiendeleza kabla ya kufanikiwa na kujulikana nchi nzima. Mahojiano haya yalikuwa katika vipindi vya hivi karibuni vya masuala ya burudani kwenye kituo hicho cha Wasafi.

Ruby alieleza kuwa baada ya kurejea jijini Dar es Salaam akitokea mkoani, alikumbana na pigo kubwa kutoka kwa ndugu na jamaa zake wa karibu waliokuwa wakiishi jijini hapa. Ndugu hao walimkataa na kumnyima hifadhi, jambo lililomfanya akose kabisa mahali pa kujistiri.

Baada ya kukataliwa na ndugu, msanii huyo alilazimika kutafuta hifadhi mbadala na kuamua kukimbilia kwenye nyumba moja ya kulala wageni (gesti) iliyopo maeneo ya Sinza, Dar es Salaam.

Katika gesti hiyo, alilazimika kulipia kiasi cha shilingi 5,000 kila siku ili kupata hifadhi ya usiku na kuepuka kuzurura mitaani.

Hata hivyo, kutokana na ukata na ukosefu wa kipato cha uhakika, kulikuwa na siku ambazo alikosa kabisa fedha za kulipia gesti hiyo. Siku yoyote alipokosa fedha hiyo, alilazimika kutoka na kwenda kulala kwenye kibaraza cha nyumba iliyokuwa inatazamana na gesti hiyo.

Ruby alibainisha kuwa wakati anatumia kibaraza hicho kama hifadhi yake ya dharura ya usiku, hakuwa na ufahamu wowote kwamba mjengo huo ulikuwa ni wa mwanamuziki Diamond Platnumz. Ndoto yake ya kutoka kimaisha na kufanya vizuri kwenye muziki ilikuwa ndio nguzo pekee iliyompa uvumilivu wa kupita kwenye changamoto hizo kabla ya kupata mafanikio anayojivunia hivi sasa.

"Nilivyorudi Dar es salaam ndugu zangu wote wa huku walinikataa hivyo nikakosa sehemu ya kulala, nilipata gest flani maeneo ya sinza kwa siku nilikuwa nalipa elfu 5, sasa kumbe ile gest ilikuwa inaangaliana na nyumba ya Diamond Platnumz."

“Sasa nilivyokuwa nakosa hela ya kulipia gest nikawa naenda kulala kwenye kibaraza cha nyumba ya Diamond bila kujua kuwa ni nyumba yake, kuna siku akanikuta akanisamilia. mimi na Diamond tumeanza kujuana mda mrefu sana" amesema hayo msanii ruby.

1787556796698.png

1787556566378.png
 
Wengine wanasema anguko lake lilianzia alipojaribu kuivimbia ile media iliyosifika enzi hizo kwa kuteka soko la burudani iliyokuwa na tamasha la kuzunguka mikoa yote nchi baada ya kukataa kupewa dau dogo.

Hapo ndipo wakaazimia kumpoteza mazima na kumpandisha yule binti ambaye kwasasa ni mke wa mtu na kwenye msiba alisimama kama mjane wa jamaa aliyefia nje ya nchi na kwenda kuzikwa kwenye migomba. Huyu binti kwa hakika alifanikiwa kuwasahaulisha kabisa mashabiki juu ya habari za Ruby.
 
Alipokataa kutoa tunda Kwa namfungulia dunia nafasi yake ikachukuluwa na yule ambaye baada ya msiba alimrudia x wake
 
Yeah system ili mfuck
 
Dj Majizo alifosi kuitafuna ikamgomea.
Ruby anamsimamo kama mlingoti wa chuma
Alipokataa kutoa tunda Kwa namfungulia dunia nafasi yake ikachukuluwa na yule ambaye baada ya msiba alimrudia x wake
Mbona mnaandika kama vile alifanya kitu kibaya na anatakiwa kujuta? Kama alikataa kujidhalilisha utu wake kwa kutumikishwa kingono kisa apate umaarufu, akalinda heshima yake na kusimamia haki ya kipaji chake basi huyu binti ni shujaa; na ni mfano wa kuigwa. Mungu Ambariki na Azidi kumwongoza 🙏🏿
 
Wengine wanasema anguko lake lilianzia alipojaribu kuivimbia ile media iliyosifika enzi hizo kwa kuteka soko la burudani iliyokuwa na tamasha la kuzunguka mikoa yote nchi baada ya kukataa kupewa dau dogo.

Hapo ndipo wakaazimia kumpoteza mazima na kumpandisha yule binti ambaye kwasasa ni mke wa mtu na kwenye msiba alisimama kama mjane wa jamaa aliyefia nje ya nchi na kwenda kuzikwa kwenye migomba. Huyu binti kwa hakika alifanikiwa kuwasahaulisha kabisa mashabiki juu ya habari za Ruby.

Kwani uongo? Ni kweli, Ruby alimkataa Ruge na hiyo yote kuogopa ukimwi.
 
Back
Top Bottom