Overgeneralization ni hatari katika kujenga hoja.Unaposema KILA MTU amebariki ukahaba,nashindwa kukuelewa.Labda useme baadhi ya watu (wengi au kidogo,inategemea mtazamo) wamebariki ukahaba kutokana na ushiriki wao kwenye shughuli hiyo (makahaba wenyewe,pimps,watumia huduma hiyo,etc).Na washiriki pia wanaweza kugawanywa katika makundi ya wanaofanya hivyo kutokana na sababu za kiuchumi na wale wanaofanya kwa starehe zao.
Ukisema "hata viongozi wa dini wanajua hilo" basi hata ufisadi,ujambazi,utumiaji madawa ya kulevya,ulawiti,na madhambi yooote tunayoyajua pia yanajulikana kwa viongozi wa dini.But,kujulikana hakumaanishi kuhalalisha.Kujua kwamba kuna ufisadi Tanzania hakumaanishi kuhalalisha ufisadi.Na kujua kuwa kuna kuna watu wanaua maalbino hakumaanishi kuhalalisha vifo vya maalbino.Kimsingi,viongozi wa dini wanapaswa kujua kuhusu madhambi kama ukahaba ili waweze kuwaongoza waumini wao ipasavyo.Kujua huko hakumaanishi kuhalalisha dhambi hiyo.Usafi au uchafu wa viongozi hao ni suala tofauti na halihusiani na sifa stahili za kiongozi wa dini.Baadhi ya viongozi wa dini kuwa wateja wa makahaba hakumaanishi kuwa dini inaruhusu ukahaba,just like kukithiri kwa rushwa Tanzania hakumaanishi kuwa rushwa ni halali.
Again,kuwepo kwa makahaba kila sehemu hakumaanishi kuwa ukahaba ni halali just like kuwepo kwa ukimwi duniani kote hakumaanishi kuwa ukiwmi sasa si ugonjwa.Au kuwepo wa biashara ya unga takriban kila kona ya dunia hakumaanishi kuwa biashara hiyo ni halali.Same could be saidi about kutapakaa kwa ujambazi,rushwa,ubaguzi wa rangi,utumikishwaji wa watoto,na maovu mengine katika jamii.Yapo takriban kila sehemu,lakini hiyo sio sababu ya maovu hayo kuwa halali.Uhalali wa kitu sio kutapakaa au kuenea kwake bali kuendana na mila,desturi,sheria na taratibu za jamii husika.
Ukahaba unawawezesha makahaba kutunza familia zao,lakini hata ufisadi nao unawawezesha watu kutunza familia zao,so does ujambazi,biashara ya madawa ya kulevya,utapeli,ukabaji,nk.Je hivyo navyo vihalalishwe kwa vile tu vinawawezesha watu kutunza familia zao?
Na tukishawatambua makahaba kisha tukawatoza kodi,what about hao watenda maovu wengine katika jamii?