Achana na hiyo...kuna body treatment moja ya ajabu sana ambayo itakufanya uonekane kama mtoto mchanga mwenye ngozi nyororo na isiyokuwa na makwinyanzi hata kama umri wako ni miaka 50 hadi 70.
Hii ni Kianty full body brushing stem bath. Hii ni body treatment ya kimataifa na inafanyika kwenye professional salon zote za Ulaya na America' na hapa Bongo ipo kwenye salon zisizozidi tatu au nne...mzee unaingia ndani ya beauty clinic room,unavua nguo zako zote au unaweza kubakia na under wear tu. Unapanda kitandani muhudumu wa kike anaingia akiwa kwenye uniform za unesi...anaanza kukubrush na kianty scrub mwili mzima,then analeta kianty steaming unapakwa mwili mzima (cream mzito) then anakuwashia double steamer mashine ambazo zitakupiga mwili mzima uku ukigeuzwa geuzwa kama kuku anechomwa kwenye oveni.
Baada ya hapo utaenda kuoga humo humo ndani...ukimaliza kuoga unapanda tena kitandani then dada muhudumu atachukuwa Kianty natural mask (mfano wa tope gumu lililo laini) alafu atakupaka mwili mzima kuanzia usoni hadi unyayoni...hii utaachwa nayo kama nusu saa au dk 45 hivi. Baadae itaondolewa yote kwa wewe kwenda kuoga tena au kwa muhudumu kuifuta yote kwa kutumia taulo laini lenye maji ya moto (kumbuka hatua hii ni ngumu kidogo kwani hiyo mask huwa inavuta ngozi yako balaa but for something good and not bad)
Baada ya hapo utalala tena kitandani,dada muhudumu atakusogelea tena mkononi akiwa na Natural Sea Salt ya Kianty atakupaka tena mwili mzima then utaingia kwenya Sauna steam bath na ndani ya hiyo Sauna steam bath kutakuwa na slace za matango kama pc 200...utakaa kwenye hiyo mashine kama dk 45 huku ukipigwa na mvuke mkali sana wa tiba. Baada ya dk zako kwisha utaoga humo humo kwenye hiyo mashine. Mwisho kabisa utapakwa finishing lotion na teyari kwa kuondoka.
Rafiki yangu, ukitoka hapo inaitwa Kantangaze huko uendako...kitu ngozi laani,ng'avu na isiyo na makwinyanzi...uvutaji wa hewa unausikia tafauti na mapigo ya moyo unayasikia tafauti. Ukiweza kuifanya huduma hii kwa mwaka mara tatu basi nakupa grantee miaka miaka mia moja...hakuna cha vipele,chunusi ndogo ndogo,ngozi kuwa na rangi mbili wala kuwa na ngozi ngumu kama ya kenge...yaani hii kitu ni kama mtoto mchanga.