Baba Wawili 2012
JF-Expert Member
- Mar 21, 2012
- 413
- 336
Natumai wote ni wazima.
Binafsi sijapendezwa na katuni iliyochorwa jana katika gazeti la Mwananchi kama ambavyo huwa inachorwa na Bwana Masoud.
Ki ukweli ukiiangalia kwa makini utagundua ina "Matusi" na waliochorwa katika katuni hiyo ni viongozi wa Taifa hili. Nadhani Mhariri wa gazeti la Mwananchi ni vyema wakaweka mipaka katika katuni zao. Ili kulinda heshima ya gazeti lao.
Mandla.
Masudi kipanya hii ya kidole cha kati haiko sawa, michoro yako daima ni ya busara anaeweza kutafisiri hata mtoto mdogo. Hapa ulikosea, binafsi sikuridhika!