Wana Jf habari ni kuwa wale vinara waliokamatwa na mzigo mkubwa wa sembe huko SA wenye thamani ya 6.8 bilion sasa wataachiwa huru kwani imeonekana kuwa mzigo huo haukuwa ni madawa ya kulevya bali ephedrine ambazo haziko kwenye kundi la dawa za kulevya
Habari zinasema ephedrine ambayo inasemekana ndiyo waliyoisafirisha akina dada hao inaangukia ktk kundi la vibashirifu yaani dawa ambazo malighafi yake inaweza kutumika kutengeneza dawa za kulevya.
Hivyo basi kesi yao haina nguvu tena na wanatarajiwa kupewa dhamana wakati wowote kutoka sasa.
Source:Gazeti la Raia Mwema Sep.18, 2013
Huu ni mweleka wa hali ya juu sana aliopigwa Dr.Mwakyembe!!
Hakika imeniacha na maswali mengi pasipo
majibu!!!
Ikumbukwe kabla ya taarifa hizo mkuu wa kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya Alfred Nzowa alienda SA kwa kile alichodai kwenda kuangalia kama watanzania hao wanatendewa haki ktk kesi yao!!!
Mimi nikajiuliza hivi wako watanzania wangapi wanaotuhumiwa na sembe China, Hong Kong na kwingineko, kwa nini huyu mkuu aende SA tu?????
Ni Nzowa huyo huyo baada ya kutoka SA alisema kuwa watuhumiwa wamewataja watu waliowatuma mzigo huo na ni mnyororo mrefu sana. Hivyo ataufanyia kazi. Ina maana watuhumiwa walitaja majina ya wauza apples!!!!
Lakini taarifa za nyuma zilisema kuwa watuhumiwa waliingizwa katika chumba cha mateso baada ya kutoonyesha ushirikiano kwa polisi SA wa kutaja wahusika wa mzigo. Lakini baada ya kuingizwa ndani ya chumba hicho walisema kila kitu!!!!!
Najiuliza, inamaana watuhumiwa waliteswa kabla ya kuthibitisha kwa uhakika mzigo walioubeba ndani kulikuwa na nini?
Hakika vita ya kupambana na madawa ya kulevya ni ngumu mno. Wampambanaji ndio wanaomiliki,wanaoratibu,wanaosafirisha,wanaosimamia na kuendesha biashara hiyo ya sembe.
Ni lini Tanzania italivalia njuga kwa dhati tatizo la dawa za kulevya????