Maskini Tanzania!

Maskini Tanzania!

Ninakupenda sana Tanzania pia ninakuwazia utakaporudi tena kwa watu walewale wanaokutesa miaka minne na kukubembeleza miezi mitatu

Tanzania ninakufananisha na yule Jamaa ambaye alitekwa na kuteswa sana akapata nafasi ya kutoroka ila alitoka nje na kurudi tena ndani kisa anaogopa Waliomteka na kumtesa labda watamuona

Tanzania upo kwenye mikono ya watu ambao hawataki kujifunza kutokana na makosa nakupenda Tanzania

Tanzania upo kwenye mikono ya watu ambao hawana sifa kuu ya mjasiriamali ambayo ni (risk taker)

Narudia tena chozi litanitoka kusikia unarudi au unafunga tena ndoa ya miaka mitano na Mume ambaye anakutesa kwa miaka minne na kukufariji kwa miezi mitatu nawe unasahau mateso ya miaka minne

Tufanye Urais upinzani ulikosea, yaani hata ubunge bado tu Watanzania wanawaamini watu waliokaa majimboni miaka 10 na zaidi???

Kuna gharama ya mabadiliko, watu wakiendelea kuwa waoga tutabaki hapa hapa...

Uchaguzi wa mwaka huu nilitegemea bunge liwe na uwiano mzuri lakini inavyoelekea tunarudi kulekule kwenye wanaosema Ndiooo waseme ndiooooo....
Nyie watu watu wawili mmeandika mambo ya msingi sana, mbarikiwe.

Binafsi kama Mtanzania najisikia aibu sana kwa maamuzi ambayo Watanzania tumeyafanya hasa kwa kurudisha wabunge wengi ambao miaka kumi au mitano nyuma tuliwaona kabisa wakiwa ni wapinga maendeleo kwa kutetea hoja za serikali ambazo zilikuwa hazina TIJA kwa wananchi.

Ila imani yangu ni kuwa kila mtu ataadhibiwa kwa makosa yake, sitegemei tena kusikia watanzania wakilia lia na huduma mbovu za afya, maji, sheria mbovu za kusimamia maliasili ya nchi.

Sitegemei tena kusikia watanzania wakilia kwa umaskini kwakuwa maamuzi yaliyofanyika na wao wenyewe ndio yatakayowagharimu. :angry:
 
Jamani, lets be serious. Hivi kweli kuna mtu serious aliyedhani kuwa Tanzania itakabidhiwa kwa UKAWA? No way. Mimi sina tatizo na LOWASSA. Lakini ukweli ni kuwa hawezi kuwa rais mzuri wa Tanzania tunayoitaka. Yaani kweli watu kweli mlitegemea Mbowe awe waziri wa Fedha na Tundu Lissu Waziri Mkuu? Watanzania wana akili... Na kinachofuatia sasa ni mwanzo wa anguko kuu la CHADEMA.
 
Ninakupenda sana Tanzania pia ninakuwazia utakaporudi tena kwa watu walewale wanaokutesa miaka minne na kukubembeleza miezi mitatu

Tanzania ninakufananisha na yule Jamaa ambaye alitekwa na kuteswa sana akapata nafasi ya kutoroka ila alitoka nje na kurudi tena ndani kisa anaogopa Waliomteka na kumtesa labda watamuona

Tanzania upo kwenye mikono ya watu ambao hawataki kujifunza kutokana na makosa nakupenda Tanzania

Tanzania upo kwenye mikono ya watu ambao hawana sifa kuu ya mjasiriamali ambayo ni (risk taker)

Narudia tena chozi litanitoka kusikia unarudi au unafunga tena ndoa ya miaka mitano na Mume ambaye anakutesa kwa miaka minne na kukufariji kwa miezi mitatu nawe unasahau mateso ya miaka minne

Hapana. wtz wameona mbali mkuu taifa hili hatuwezi wakabidhi genge la wahuni.
 
Soma "allegory of the cave by Plato"
Allegory of the cave eeh? Toeni elimu ya uraia kwa wananchi na muwe na strategy nzuri na mikakati ya kudumu. Mmepoteza muda mwingi kumsafisha Lowassa badala ya kuelezea sera zenu. Haya mambo ya Plato na pango lake na waogopa mwanga hazitawasaidia. Jitathminini kwanza badala ya kukimbilia kusema kuwa wapiga kura ni wajinga. Inawezekana nyinyi mlioko nje ya pango ndo wajinga japo hamjielewi!
 
Pale wananchi wanaposhabikia siasa kama ushabiki wa mpira ndio hapo utokea yote tunayoyaona leo.nitabaki kuamiani kwamba Upinzani ungeleta changamoto kubwa sana katika Taifa letu hili.hila njaa imetukost .tutaendelea kuwa maskini
 
Watanzania sio wajinga kama ulivyofikiria...!! Hatuwezi kumpa fisi atawale nchi..!! Mpaka upinzani utakapokua upinzani kweli na sio timu ya wasakatumbu ndo tutawachagua upinzani...:hand:

Huyu aliyetunyima elimu, uelewa, kujitambua ndiye aliyetumaliza kabisa. Fikra za aina hii ni tatizo kuliko ccm yenyewe
 
Kuna watu mnajiona mna akili sana kumbe ni wapumbavu tu.Wengine hawajawapigia kura upinzani kama salamu tu ya kwamba wao siyo wapumbavu wa aina hiyo.Huwezi kuwaimbia watu Lowassa fisadi kwa miaka saba halafu eti ndani ya miezi miwili tu uanze kuwaaminisha kwamba Lowassa siyo fisadi Mara oooh katubu.Mnao waona watanzania wapumbavu kisa hawakubaliani na upumbavu wenu basi nyie ndo wapumbavu hasa.Mbadala wa CCM ukipatikana,CCM itang'oka tu lakini kama wanaojitokeza ni hawa hawa mchwa watafuna ruzuku then CCM itaendelea tu.Heri ujue moja kuwa hiki ni kinyesi kuliko ulaghaiwe na kinyesi kilichopuliziwa perfume.
 
Usilaumu wapiga kura, laumu ukawa kumsimamisha mtu asiyeaminika hata kidogo.
Magufuli sasa kazi anayo kubwa sana maana akicheza hata kidogo atakua rais ambaye alikaa miaka mitano tu wakamsepesha.
 
Watanzania sio wajinga kama ulivyofikiria...!! Hatuwezi kumpa fisi atawale nchi..!! Mpaka upinzani utakapokua upinzani kweli na sio timu ya wasakatumbu ndo tutawachagua upinzani...:hand:

Aliyetunyima elimu, uelewa, kujitambua ndiye aliyetufikisha hapa. Huyu ndio adui namba moja. Fikra za namna hii zitaendelea kudumaza hii nchi forever. Then unakuta mtu kama huyu ni maskini wa kutupa. Problem kabisa
 
Kuna watu mnajiona mna akili sana kumbe ni wapumbavu tu.Wengine hawajawapigia kura upinzani kama salamu tu ya kwamba wao siyo wapumbavu wa aina hiyo.Huwezi kuwaimbia watu Lowassa fisadi kwa miaka saba halafu eti ndani ya miezi miwili tu uanze kuwaaminisha kwamba Lowassa siyo fisadi Mara oooh katubu.Mnao waona watanzania wapumbavu kisa hawakubaliani na upumbavu wenu basi nyie ndo wapumbavu hasa.Mbadala wa CCM ukipatikana,CCM itang'oka tu lakini kama wanaojitokeza ni hawa hawa mchwa watafuna ruzuku then CCM itaendelea tu.Heri ujue moja kuwa hiki ni kinyesi kuliko ulaghaiwe na kinyesi kilichopuliziwa perfume.

Uko sawa
 
kweli kabisa. Kama macho hayawahi kuona tofauti na kilicho zoeleka, kumbadilisha mwenye macho ni ndoto za alinacha.

Kweli Watanzania itatuchukua muda kupiga hatua ya maendeleo. Tumekuwa wanafiki lakini mioyoni ndani tunaongea kitu kingine. issue ya udini na ukabila vinatumaliza. tutaendelea kukosa watu wazuri wa kutuongoza kwa sababu zisizo na misingi.
 
Pale wananchi wanaposhabikia siasa kama ushabiki wa mpira ndio hapo utokea yote tunayoyaona leo.nitabaki kuamiani kwamba Upinzani ungeleta changamoto kubwa sana katika Taifa letu hili.hila njaa imetukost .tutaendelea kuwa maskini
broo upinzani hadi sasa una mafanikio makubwa sana haijawahi kutokea safari ya kubadilisha utawala katika jamii yenye elimu duni si kazi lele mama. hakuna sehemu iliyokuwa ikiniuma kama Dar es salaam lakini safari hii dar imebadilika na hii ni dalili njema sababu madudu na uozo mwingi ulikuwa unafanyikia hapo. hii ni dalili njema sana
 
Tufanye Urais upinzani ulikosea, yaani hata ubunge bado tu Watanzania wanawaamini watu waliokaa majimboni miaka 10 na zaidi???

Kuna gharama ya mabadiliko, watu wakiendelea kuwa waoga tutabaki hapa hapa...

Uchaguzi wa mwaka huu nilitegemea bunge liwe na uwiano mzuri lakini inavyoelekea tunarudi kulekule kwenye wanaosema Ndiooo waseme ndiooooo....

Tanzania ya sasa kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Kuoneana huruma hakuna tena.
Hatujajifunza bado.
 
Hamuwezi kumpa fisi atawale nchi?

Unaona sasa..huu ndo ujuha wenyewe ninaouzungumzia.

Hao CCM ni zaidi ya fisi maana wao ndo waliosababisha na watakaoendelea kusababisha hali tuliyonayo.

Kama hulioni hilo ni ama unanufaika na uwepo wao madarakani au u juha kama jiwe.

Usibishane na wapumbavu hao.
Tanzania ni zaidi ya majuha.
Tumelaaniwa.
 
Back
Top Bottom