Masimulizi ya John Perkins na hatima ya Magufuli

Masimulizi ya John Perkins na hatima ya Magufuli

John Perkins, kachero wa National Security Agancey (NSA) ya U. S anasimulia jinsi ambavyo US huzifanyia nchi masikini duniani ili kuweza kuzinyonya na kupata rasilimali zake. Katika kitabu chake cha Economic Hit Men, Perkins anaeleza mbinu mbalimbali hasa kupitia mitambo ya umeme na uzalishaji nishati kuzipa madeni makubwa na tozo kubwa nchi hizo kama njia ya kuzifilisi na kuzifanya tegemezi huku wakiongeza shida kwa wananchi. Richmond na Escrow vinawea kuwa mfano, jisomee!

resistir.info/livros/john_perkins_confessions_of_an_economic_hit_man.pdf

Zaidi ya hapo John Perkins ameelezea namna ambavyo Economic Hit Men (EHM) hutumwa na serikali yao kupitia mashirika na makampuni mbalimbali makubwa kuwatapeli viongozi wa nci masikini waingie mikataba hiyo ya kitapeli. Perkins anasema wakishindwa kuwashawishi viongozi 'wagumu' mbinu ya kuwaua hutumika. Perkins ametoa mifano ya viongozi waliowahi kuliwa kwa njia mbalimbali na hata kupinduliwa.

Perkins anasema jaribio la kumuua likishindikana basi nchi husika hupelekewa vita. Mfano anaoutoa hapa ni wa Iraq kwa Saddam Hussein.

Ukisoma kitabu hicho cha Economic Hitman utakuta kabisa MCC ni moja ya mpango ulioandaliwa na Economic Hit Men. Perkins anasema nini hutokea endapo Economic Hit Men wakishindwa?

I wrote that in 1982, as the beginning of a book with the working title, Conscience of an Economic Hit Man . The book was dedicated to the presidents of two countries, men who had been my clients , whom I respected and thought of as kindred spirits -- Jaime Roldos , president of Ecuador, and Omar Torrijos, president of Panama . Both had just died in fiery crashes. Their deaths were not accidental. They were assassinated because they opposed that fraternity of corporate , government, and banking heads whose goal is global empire . We EHMs failed to bring Roldos and Torrijos around, and the other typ e of hit men, the CIA-sanctioned jackals who were always right behin d us, stepped in.

Perkins anaeleza wao ni akina nani, wanafanya nini na sababu iliyompelekea kuhatarisha maisha yake kuandika hiki kitabu.


That is what we EHMs do best: we build a global empire. We are an elite group of men and women who utilize international financia l organizations to foment conditions that make other nations subservient to the corporatocracy running our biggest corporations, ou r government, and our banks. Like our counterparts in the Mafia, EHMs provide favors. These take the form of loans to develop infrastructure — electric generating plants, highways, ports, airports, or industrial parks. A condition of such loans is that engineering an d construction companies from our own country must build all thes e projects. In essence, most of the money never leaves the United States; it is simply transferred from banking offices in Washington to engineering offices in New York, Houston, or San Francisco.

Najaribu kutafakari haya masimulizi ya Perkins kama yana ukweli na hatima ya msimamo wa rais Magufuli kwa U.S. Japo wengi wetu ni wavivu wa kusoma, kitabu hiki che Economic Hit Man kinafaa sana kusomwa hasa na watu wanaopenda kufikiri
Ulichosema ni kweli. Hata sera za kima cha chini cha mshahara/mifuko ya akiba za uzeeni/riba kubwa za mikopo vs riba ndogo kwa akiba yako benki, makodi kedekede nk. Lengo ni kumfukarisha mwananchi, azidi kuwa mnyonge na mjinga ili watawala wajineemeshe. Ndio mana unaona wanaongeza idadi ya mikoa na wilaya, wananunua magari ya washawasha na kuvuruga uchaguzi na kuzima mabadiliko kikatiba.
 
I see what a wonderful argument! Then support it with evidence, say why do you think so rather than giving empty words
There is no doubt you might be a devout follower of staunch "conspiracy theory" believers . Utakuwa muumini mzuri wa Ponda, mtashinda ktk mitandao kutafuta theories kibao za kuonyesha jinsi mnaibiwa, mnakandamizwa, kuliko kuangalia nini mnaweza fanya muende mbele haraka.
 
Wanaoaamini huu upuuzi na kutafsiri kipuuzi km tulivyoona wajinga wengi. NI wazi kwamba hawa jamaa ni rahisi sana kugeuzwa kuwa magaidi.
 
Tatizo bado ni tafsiri, ni kutokana na malezi na fikra ulizojengewa. Huwezi kataa ni tafsiri ya mwandishi au nia yake ya kuandika hicho kitabu ndio unaiamini na si lazima iwe ndio ukweli wa mambo.
...Kuna vitu vilivyoongelewa, ambavyo ni facts. Lakini, haimaanishi kwamba mwandishi yuko sahihi kwenye tafsiri ya kila jambo lililofanywa na US Govt.

Hapo ndipo nakuambia shida ipo kwako zaidi kuliko ambaye hakukisoma kabisa. Hivi unajua hao waandishi pia huandika vitabu kwa style fulani ili kutafuta hela ya kustaafia, kwa kuuza habari wajinga wanazopenda ili kuzidi waharibu zaidi na kuwatisha kabisa? Wajamaa ni wajinga sana, kiasi cha kuweza wageuza soko, ktk furaha yao au ktk huzuni yao.
...Huyo jamaa amekiri aliyoyafanya. Hayo mengine ni tafsiri yake ya what drives US foreign policy and development aid, overseas.

...Actually, kuna faida kukisoma. Unless, unasema kwamba wewe baada ya kukisoma hukujifunza chochote.
 
Ningumu sana watz na waafrica wengine kujitoa ktk ujinga wa CCM. CCM wanajilisha ujinga sana ,sasa wanaamini huo ujinga.
...Epuka kutumia vijembe na kejeli za kisiasa kwenye mijadala kama hii. Una blunt umuhimu wa hoja zako.

...Hoja zako nyingi zinajitosheleza, usiziharibu kwa kuingiza mihemko ya kisiasa.
 
...Epuka kutumia vijembe na kejeli za kisiasa kwenye mijadala kama hii. Una blunt umuhimu wa hoja zako.

...Hoja zako nyingi zinajitosheleza, usiziharibu kwa kuingiza mihemko ya kisiasa.
Haha.sidhani km ulicho quote mimi ndio nipo wrong. Au kwa vile nimeitaja ccm? huo ni mfano hai sana kweli pengine usiyo taka isikia. nikusaidie . UNAFAHAMU NENO BACKFIRE? Sasa litumie katika propaganda za CCM(ambazo ni uongo) dhidi ya wengine, halafu angalia zinadhuru nani ktk kuziamini.
 
RedDevil, baada ya kumsoma huyu Perkins na pia kupata nafasi ya kupitia "Economic Development" kama model mpya ya uchumi baada ya kushindwa kwa model uchumi wa soko, nikapata hisia hawa watu wanataka kuiingiza hii model yao ya 'mixed economy' ambayo inataka kujikita katika kutoa social services na unafuu wa maisha wa aina fulani kwa watu wa nchi masikini. Yaani kama wanataka kukopa mambo fulani kutoka katika ujamaa na kuyaingiza katika ubepari. Nikifikiria zaidi naona kama lengo lao halichochowi na mapenzi yao kwa watu wa dunia ya tatu bali wanaona wakiendelea na unyonyaji wao wa namna ile watawachukiza watu wengi na kupata maadui wengi hivyo kupelekea ubepari na hasa nchi ya marekani kuanguka. Anyway, najaribu kufikiri na ningependa wengine wafikiri hawa jamaa wana mpango gani hasa!
..."model ya uchumi wa soko" haijashindwa. Ila, inafahamika kwamba usoshalisti na ukomunisti umeshindwa, na almost nchi zote dunia zina uchumi wa soko.

...Unahitaji kusoma kuhusu New Deal, ili kujua historia ya US kwenye masuala ya social services.

...Lengo lao ni kuambukiza utamaduni wao wa maisha, siasa na uchumi duniani kote. Ili tufanane, wakiamini kuwa hilo ndio linafanya dunia kuwa sehemu salama zaidi.
 
Haha.sidhani km ulicho quote mimi ndio nipo wrong. Au kwa vile nimeitaja ccm? huo ni mfano hai sana kweli pengine usiyo taka isikia. nikusaidie . UNAFAHAMU NENO BACKFIRE? Sasa litumie katika propaganda za CCM(ambazo ni uongo) dhidi ya wengine, halafu angalia zinadhuru nani ktk kuziamini.
...Narudia tena. Una hoja za msingi katika mjadala huu, acha kuchomekea vijembe vya kisiasa.

...Uchaguzi ni wako, wangu ni ushauri tu.
 
..."model ya uchumi wa soko" haijashindwa. Ila, inafahamika kwamba usoshalisti na ukomunisti umeshindwa, na almost nchi zote dunia zina uchumi wa soko.

...Unahitaji kusoma kuhusu New Deal, ili kujua historia ya US kwenye masuala ya social services.

...Lengo lao ni kuambukiza utamaduni wao wa maisha, siasa na uchumi duniani kote. Ili tufanane, wakiamini kuwa hilo ndio linafanya dunia kuwa sehemu salama zaidi.
kwa ufupi ujamaa ulishindwa na utashindwa kwa vile haufai. Ujamaa huwa haufanyi kitu kinachofanyika au kuwa na faida,ila wanafanya kila kitu ili kujionyesha mbele ya wajamaa kuwa wanaweza zaidi. Ndio maana hata maonyesho ya wajamaa kila kitu ni cha kuonyesha tuu si cha kutumika.
 
Angalau hata katika wazo la mjinga mwerevu anaweza akapata kitu cha kujifunza. Arguement yako ni nini hasa? Wapi nilipotafsiri hicho kitabu zaidi ya kutaka tukitumie kujifikirisha zaidi? Generalization yako ya wajamaa ni wajinga sana imenishangaza. Wajamaa wote ni wajinga au baadhi ya wajamaa au wajamaa unaowafahamu wewe? Kitabu hiki wameandikiwa wajamaa? Hebu na wewe nisaidie tafsiri yako hapo
...Tuko pamoja!
 
Kimsingi kwa utegemezi wetu hatuwezi kuukimbia ubepari.Ukingalia sana ni kama ujamaa umeshakufa duniani.Sema uchumi wa soko huria tunaoufanya hapa Tanzania ni mbaya sana ambapo serikali imejitoa kabisa kwenye biashara.Lakini ukingalia USA wakati wa mdororo wa uchumi waliingilia Kati makampuni na kufanya maamuzi,mfano General Motors walilazimisha na kuweka menejimenti walioitaka.
Nafikiri hata sisi tunapaswa kuyathibiti makampuni yetu hata kama tunaamini kwenye uchumi wa soko.Mfano kwenye sakata la sukari serikali ilipaswa kuvibana viwanda na waagizaji
 
kwa ufupi ujamaa ulishindwa na utashindwa kwa vile haufai. Ujamaa huwa haufanyi kitu kinachofanyika au kuwa na faida,ila wanafanya kila kitu ili kujionyesha mbele ya wajamaa kuwa wanaweza zaidi. Ndio maana hata maonyesho ya wajamaa kila kitu ni cha kuonyesha tuu si cha kutumika.
...Unafahamu waFaransa ni wajamaa wa aina fulani?

...Kushindwa kwa mfumo fulani wa uchumi, hakumaanishi kwamba hauna kitu chenye manufaa. Au hauna faida.

...Acha uongo! Na epuka ku generalize vitu.
 
Kwa asili binadamu ni mbinafsi. Tazama jinsi ambavyo kwa miaka michache tu tayari kuna tabaka fulani limejengwa Tanzania. Ambalo ni wafaidikaji wa kile alichosema rais, serikali kufanya biashara na fedha zake zenyewe. Ubwana na utwana umeletwa na tabaka hilo, ni kazi ngumu kuweza kulikumbusha tabaka hili kwamba pamoja na uhuru wa mtu au taasisi katika kujitafutia maisha mema lakini ni lazima haki itendeke, kodi ilipwe, njia za panya kama vile uingizaji mafuta bandarini, zikomeshwe. Ni vita ngumu sana kulikumbusha tabaka hilo kwamba linachofanya ni kufaidika na ubepari wakati lenyewe ni likiwa ni tabaka linalokula kwa kutegema udalali wa kimataifa.
...Phillipo, tabaka lilikuwapo toka enzi zile mlipokuwa mna gate crush minuso ya washkaji O'bay. We mwenyewe ulifaidika na u tabaka enzi zile kwa kukaa mjini kwenye nyumba ya ghorofa, karibu na baharini.

...Kuna makosa yanafanyika. Lakini, siku zote jamii huwa na matabaka, watawala, wasomi, watendaji, wafanyabiashara, wakulima, n.k. Watu hawa hawatofanana maishani.

...Kazi kubwa ya Serikali ni kutekeleza mipango ya kiuchumi na kijamii itakayo punguza pengo kati ya matabaka, na kuboresha hali ya maskini.
 
...Phillipo, tabaka lilikuwapo toka enzi zile mlipokuwa mna gate crush minuso ya washkaji O'bay. We mwenyewe ulifaidika na u tabaka enzi zile kwa kukaa mjini kwenye nyumba ya ghorofa, karibu na baharini.

...Kuna makosa yanafanyika. Lakini, siku zote jamii huwa na matabaka, watawala, wasomi, watendaji, wafanyabiashara, wakulima, n.k. Watu hawa hawatofanana maishani.

...Kazi kubwa ya Serikali ni kutekeleza mipango ya kiuchumi na kijamii itakayo punguza pengo kati ya matabaka, na kuboresha hali ya maskini.
Mbona chupa tupu hiyo, mwambie mhudumu akuongezee kinywaji. Pamoja brother.
 
Hii ni thread ya maana sana kulinganisha na issues nyingine nyingi zinazoendelea humu JF. Lakini mtanzania mara nyingi hapendi kuumiza kichwa, anataka masuala mepesi ambayo hayahitaji kumfikirisha ili achangie kwa uhuru zaidi.
Very educative thread.
...Ndio maana nimemshauri Nico asiingize vijembe vya kisiasa.
 
...Ndio maana nimemshauri Nico asiingize vijembe vya kisiasa.
sawa mjamaa, ndio maana nawaambia huwa wajamaa wanapenda kufanya kazi zisizo na faida.Hamuwezi jiona . Sasa km huna practical thing kuhusisha ktk hizi story ,huu muda mnapoteza kuchambua mngefanya vitu vya maana.Hii habari itakuwa haina haja ya kuchambua. Practical failure ni hili CCM lenu na linaendelea, sasa unalijengea msingi wa kutoa sababu ktk vitu wasio wajamaa wanaona kabisa ni kupoteza muda na rasilimali.
 
Nakumbuka rais mstaafu Mkapa aliwahi kuagiza mawaziri wake wasome kitabu hicho. Pia aliagiza wasome na kile cha Prof Hernando De Soto, Dead Capital, na ndiyo akaja na MKURABITA.
...Moja ya project za maana kabisa katika nchi.
 
Unakataa ninachosema unarudi huko huko. Nakuuliza HIYO BURE UNATAKA KWA LIPI ULILO NALO?Hakuna rockettt science hapo , kupata bure km bure ni nadra sana na hiyo bure kwanini bure iwe kwako na si mwingine?. Sasa kwanini kuumiza vichwa kwa fikra za kugundua bure?
...Ndio maana wameuliza watu humu kama umekisoma, na umekielewa.

...Hoja sio bure, la. Kinachojadiliwa ni lengo la mkopo. Kwamba, unatolewa ili kukuingiza kwenye deni lisilolipika na kukutia matatizo ya kiuchumi. Si kwa ajili ya kufanikisha miradi ya maendeleo. Utakapokwama, unakuwa katika nafasi ya kutekeleza wanayotaka.
 
Bado sio shida wakuu ktk dili risky, ujue kulinda taifa kuna human cost. Sasa kutakuwa na shida gani kupokea hela zitakazookoa watu wengi kuliko watakaokufa wakilinda wengine.? mi sioni shida zaidi ya fikra zetu za kulala na kutoongeza weledi ktk deal breaking. Sasa unataka ktk deal mtu akupiganie wakati anataka best price?
...Deal hapo lilikuwa ni ku guarantee dominance ya dola kama trading currency.
 
Back
Top Bottom