Mimi ni dispora lakini matatizo yangu ni matatizo ya wengi hata kaka yangu ambaye yuko Tanzania anapata matatizo hayo hayo.
Naomba niweke utangulizi kwamba nayoyasema hapa sio kwa 100% ya Watanzania lakini ni utamaduni ambao unaturudisha nyuma
Najua kama jamii tuna mikasa mingi sana na mimi badala ya kusema ya watu niseme yale ambayo nina uhakika nao
Diaspora tufauti wa wengi wanavyo amini ni wengi wetu ni Watanzania wa kawaida ambao tunatafuta pesa na kuinua maisha yetu. Mimi mfano nimepigika sana kwanza nimekaa hapa US kwa miaka 25. Ilinichukuwa miaka 12 bila kumuona baba yangu mzazi kuanzia 1997 mpaka 2009.
Tena bahati mbaya nimeshanunua ticket ya kwenda Tanzania miaka ile kaka yangu akafariki hivyo baada ya miaka 12 nilimkuta mzee wangu kwa masikitiko makubwa. Nimejipiga ndugu zangu sana nikafanikiwa kumaliza mpaka degee ingawa kwasababu ya kufanya kazi ilinichukuwa mpaka 2006 kukamilisha na kupata shahada ya fedha.
Nimefanya kazi za mabox za kila aina mpaka sasa nimekuwa consultant kwenye kampuni kubwa sana na nafanya kazi na hospital. Naelezea hili ili ujue kwamba watu wanatokea mbali na sio kwa kujionyesha au kulalamika. Naomba nitoe mifano michache jinsi gani uaminifu wa wetu unaturudisha nyuma:
1. Nina shamba Bagamoyo kubwa wale watu ambao wameniuzia shamba ndiyo haohao wanarudi tena na kujaribu kuwauzia wengine. Kibaya zaidi hawana uoga na wanaona ni sawa tu.
2. Kuna mzee nilimweka shambani kwangu nikamjengea nyumba, nika ajiri watu watu wamlimie eka 4, nikamnunulia pikipiki ili aweze kufanya shughuli zake lakini kwanza amekuwa akiiba bati za nyumba ambayo anakaa yeye anauza halafu anasingizia wezi. Nilikubali kutengeneza nyumba mara ya kwanza, ya pili, ya tatu na ya ya nne. Baada ya kuuza mabati mara nne nikaweka mtego na polisi wa kule bagamoyo bahati nzuri OCD alikuwa classmate watu wakamshika yule mzee akiiba mabati. Pikipiki yangu ambayo nilimpa nikakuta ameenda kuweka rehani na kapewa 100,000 wakati nilitumia 900,000 kununua.
3. Kuna fundi ambaye wamenipa nyumbani uninio anisaidie na wakaniambia ni mwaminifu lakini cha ajabu kazi ambayo ilikuwa inahitaji bati 13 aliweka bati 22 mpaka nilipouliza ndiyo akajirudi na kusema kazi inahitaji bati 13.
4. Tusisema watu wa chini tu nilipeleka kontena 2013 kwa mpango wa kufungua clinic ndogo thamani ya vitu ilikuwa $98,000 lakini nilipata kwa $20,000. Basi nikatuma list Tanzania ili nijue gharama zote za kodi kabla ya kupeleka vitu nikaambiwa hakuna kodi ni usafiri tu na storage ya siiku moja. Mzigo ukatuma ukafika Tanzania ghafla TRA haohao wakaja na kunitaka nilipe tsh 15M au wataifishe vitu vyote.
5. Mwaka jana Oct 2022 nimeenda Tanzania na nilihitaji NIDA. Yaani kwasababu jamaa nilimpa pesa kidogo ya kuifanya haraka nilipata card yangu ndani ya wiki wakati wazazi wangu nikaja kugundua walikuwa hawajapata card zao kwa zaidi ya miaka 2. Wazazi wangu ambao wanahitaji NIDA zaidi yangu walizungushwa miaka zaidi ya miwili mpaka nilivyofika Tanzania na baada ya mimi nao walipewa lakini kwasababu ya uwezo na kujuana.
Jamii yetu haitakiwi kuwa hivi. Kuna pesa nyingi sana vitu vingi sana hatuwezi kufanya au hata kusaidia kutokana na uaminifu. Rafiki yangu Professor youko Mississippi alitaka kuleta wanafunzi wa udaktari wa chuo kikuu muhimbili kwa semina akashidwa kwasababu Professor wa muhimbili mkuu wa kitengo alimuomba pesa ambayo hakuwa nayo. Mimi hapa mwenyewe nashidwa hata kupeleka vitu tena kwasababu vitu vikifika Tanzania ni maneno mengine.
Yaani kwa ushauri wangu kusaidia nchi nunua bond/TRESURY BILLS za Tanzania na hiyo pesa itaenda kwenye miradi ya serikali na utapata 10%-12% kwa mwaka lakini kufanya miradi nchini Tanzania ni ngumu sana sana kutokana na utamaduni wa wizi na udanganyifu