Masikini Ze Comedy Imekosa Legal Advice

Walikuwa wanapata sikatai lakini hata wewe hollo ukipata a better paying job you leave the old one and move to the new one.mbona christian ronaldo nalipwa mno and still anang'ang'ania better payments?
Yeah ni kweli lakini sasa mimi nikitapata sehemu ya dau kubwa naondoka ila si unajua tena kazi zinatofautiana kwa hili suala la kina Ze comedy ni lingine Manji hajawashawishi burebure lazima ni kwa manufaa yake pia!
Kuhusu Ronaldo wewe muache tu si anang'ang'ania kwenda Madrid atakoma maana huko kila mtu anacheza vizuri atalisugua benchi hadi atakoma!na asipoangalia itakuwa mwisho wake!
 
Hollo you dony make empty offers.you make an offer expecting something in return.
 
Hollo you dony make empty offers.you make an offer expecting something in return.
kwa kweli mimi ningekuwa wao nisingekubali mhindi afaidike kupitia mgongo wangu!Ukizingatia wahindi kazi yao ni kuiba tu na kutunyanyasa
sisi watz kwenye ardhi yetu!
Asante!
Hollo
 
....mimi Nafikiri Bora Ze Comedy ...na Mengi Waelewane ...warudi Eatv,....kitendo Cha Jana Tvt /tbc Kukataa Kuonesha Hotuba Ya Slaa Kimenipa Hisia Kuwa Hawa Vijana Watapokonywa Uhuru Wao Tbc Hata Kama Tido Ana Nia Njema Lakini...serikali Imeonesha Nia Ovu Ya Kutopenda Kukosolewa....na Inaonekana Vijana Hawatakuwa Na Uhuru Kamili....

Tunaomba Mzee Mengi Na Regina Wawarudishe Hawa Vijana ...wawape Mkataba Mnono...ili Watusaidie Kupambana Na Ufisadi
Kweli Bro Hawa Vijana Wamrudie Mengi Wakafanye Makubaliano Mkuu.unajua Kama Waliona Kitendo Cha Jana Wajue Wazi Hawataweza Kuact Chenge Akifanya Uchawi Bungeni.
 
Mbona Jambo imekuwa Jamii na bado inapeta? Watafute jina jipya waliache hilo lenye wenyewe. Kama kweli wanakubalika, watu watawafuata kama sisi tulivyoifuata Jamiiforums!
 
Once mtu anapotaka kuanzisha kitu its best kama unakuwa na legal counsel.mimi binafsi ni law student.befor nilikuwa hata still nina wasiwasi wa akina joti kuendeleza matimizi ya hili jina 'ze comedy'.wao kama comedians wanaweza ku go an extra mile and be creative watunge jina jipya and still they will make it.If before they made it why not know?
I believe they can fly and make it big.

Kwa ufupi njia walotumia EATV kuwakaba shingo hawa bwana hawatakuwa na pakutokea,the only solution sasa hivi wabadili jina,mbinu n.k kidogo tu.Hata hivyo ilifaa mkataba wao uwekwe wazi na EATV ili wapate msaada wa kisheria.Lililowakumba hawa ndilo linaloikumba serikali yetu nkila siku.Watu mnapoingia mikataba msiangalie maslahi ya wakati huo think of the future,think of the probable consequences,think of breach,damages,assignment,termination etc. Sasa wasanii wetu wakishaahidiwa pesa tu basi wanaanguka wino bila kusoma mkataba au kuomba japo siu mbili tatu wa usome kwa msaada wa legal counsel kabla ya kuusaini.

Sasa hivi wadau be very careful mnapoingia mikataba hasa ile ya kunegotiate,bora hata ile unilateral unaweza kuprove unfair contract,or undue influence hii mingine ni ngumu.
 
Hatuna cha kuwasaidia..hii sheria imewakalia pabaya..inawakata shingo hawa moja kwa moja. Ila wanavuna walichopanda.
 
Hakuna cha uhasama kabisa EATV wana haki kabisa!Hao vijana si watafute jina jingine wanaweza wakajiita THE comedy na si ze comedy na hayo majina wanaweza wakayapindisha kidogo tu kazi inaendelea badala ya kuzidi kulalamika

Ndugu, hivi niulize, kuna mtu ana haki miliki ya kipaji cha mtu mwenyewe...?? Ndio kwenye jina wanaweza wakawa wana haki miliki. Ninavyojua na kwa jinsi wanasheria wengine (walio wataalamu wa sheria za haki miliki) manake wengine huwa wanakurupuka hali hawajui haki miliki, mtu huwezi kuwa na haki miliki kwenye talent ya mtu bila idhini yake tena ya kimaandishi..!! Yaani in other words, Asha baraka hana haki miliki na style maarufu ya Ally Choki, ndio maana hata alipokuwa anahama, hakuweza kumpiga stop kuitumia. Ukiongelea kipaji, the first beneficiary wa haki miliki (pale panapokuwa hapana makubaliano yaliyo halali na siyo ya kusurutishwa; kwa lugha ya kisheria pasipo na undue influence) huwa ni mtu mwenyewe. Sasa sielewi huyu jamaa wa COSOTA anakurupuka vipi, hali yeye mwenyewe akishirikiana na BASATA waliwahi kumtetea Mengi, Mhavile na Rita Paulsen pale walipowaibia haki miliki vijana wanyonge hali hawa madogo walikuwa na maandishi ya kuwa wamiliki halali wa copyright ya Bongo Star Search (kesi bado iko mahakamani). Wafuatiliaji wa maswala ya sheria mtakuwa mmeisikia. Hayo tuyaache, tu-concentrate kwenye Ze Comedy.

Kwa hiyo, hawa madogo wasinyanyaswe hata kidogo, na ninaomba wataalamu wa sheria za haki miliki wasimame na kuongea facts. Tuachane na hawa wanasheria waliopewa cha juu na kuanza kuwakandamiza vijana wa watu. Pia tukumbuke kuwa hawa vijana hivi sasa wanafadhiliwa na Manji, na kwa wafuatiliaji wa maswala ya kijamii, mtakumbuka ugomvi kati ya Mengi na Manji ulivyoleta gumzo hapa TZ kiasi cha kuburuzana. Kwa hiyo hii ni ishara tosha ya namna ambavyo Bwana Mengi na familia yake pamoja na washirika wake walivyoamua kuwaharibia vijana hawa bila kujua wakidhani wanamharibia Manji ambaye nahisi keshashiba utajiri. Ushauri wangu kwa Mengi na washirika wake ni kuwa, wasilete ugomvi wao na Manji katika maeneo yatakayoumiza wanyonge. Kama wanataka kupambana wakapambane kule BOT au Kempinski ambako ni kwa mapede wenzao. Au if possible wakapambane huku wakiwaumiza matajiri wengine kama kina Mkono, Bakhresa au Rostam kabisa.

Huu ni ukoloni mamboleo ndani ya nchi yetu wenyewe. EATV ningewashauri wakatae mambo mengine lakini sio matumizi ya talents za vijana wa watu ambao waliamua kujituma badala ya kujiingiza katika u-kibaka na matumizi ya madawa ya kulevya. Tumeona vipindi kibao vya TV vinarushwa leo kwenye SABC kesho kwenye channel nyingine kwa mwendo ule ule.
 
Na niongezee, watanzania wengi tuna tabia ya kuogopa na kufagilia watu matajiri kiasi kwamba kila anachofanya hata kama ni kinyesi kitaonekana ni pafyumu. Nawaona watu kibao wakiongea hapo juu kuwasapoti EATV. Mi nafikiri ingekuwa busara na hekima kama tungeangalia kama palikuwa na mkataba halali kabisa, wa vijana hawa kushift ownership ya talents zao (i.e. surrender of copyright) to EATV. If upo, then we can say EATV wana haki. Lakini isijeikawa EATV wanaleta janja ya nyani ili kutimiza adhma za pede wao (i.e. kupambana na Manji).

Tuwe waangalifu katika maneno yetu tutatia aibu..!!
 
Sina huruma kwa hao vijana wa Ze Comedy kwa kuwa wanachokipata hapo ni matunda ya ujuha wao. Makosa yao makubwa ni haya yafuatayo:

Moja, walianza kufanya mipango ya kuhama EATV bila kufanya uchunguzi wa kina na hivyo hawakuyatarajia haya yanayotokea hivi. Katika dunia ya ushindani, hakuna mfanyabiashara anaweza kukubali aharibu biashara yake kirahisi kwa kumwachia mpinzani wake atambe zaidi.

Mbili, vijana wamerubuniwa na Manji na ndiyo maana wamejikanyaga waliposema kwamba walimuomba Manji awe Mlezi wa Kikundi. Hivi Mlezi wa kikundi anawajibika kuwalipia nyumba, usafiri, masomo na mishahara? Huyu ni mlezi ama ni mwajiri? Nilitegemea kwamba TBC ndiyo ambao wangekuwa wanawalipa hao jamaa. Kilichofanyika ni kwamba vijana walisaini mkataba na Manji, na mojawapo ya vipengele vinatamka wazi kwamba maigizo yao lazima yawe approved na Manji (hilo peke yake linatosha kukujulisha lengo la Manji ni nini na kwamba ana ajenda mbaya na inawezekana katumwa na mafisadi).

Tatu, hawa vijana nao ninaona ni mafisadi kiaina kwa kuwa walitakiwa wawe makini na wasome between the lines kwenye huo mkataba walio usaini na kuusifia sana kwamba ni mnono wakati mimi ninaona ni kitanzi cha kuua sanaa yao kwa kuwa kuna mambo mazuri ya kuwapandisha chati ambayo wangeweza kuyaigiza lakini as long as yanagusa maslahi ya Mlezi wao na serikali ya mafisadi basi vitu kama hivyo hatutaviona tena. Tutegemee mambo mengine tofauti kabisa, hakuna cha waziri mkubwa wala nini ama tutarajie maigizo ya kuwapandisha chati mafisadi na kuwasifu viongozi na siyo kuwakosoa ama kuwafikishia ujumbe kwamba wajirekebishe.
 
Lets be frank with one another.Today money is everything.kama wewe unaona pesa si kitu kaa nyumbani ucheze kidali mpo uone mwisho wako ni nini.mnadhani hawataki kuendesha 'vogue' au 'lamborghin'?wanataka ndio maana wanatafuta penye maslahi.

pesa siyo kila kitu bro, unaweza ukawa na pesa hukakosa amani, sasa hiyo vogue ama lamborghin zikawa huwani tu.
 
Hakuna cha uhasama kabisa EATV wana haki kabisa!Hao vijana si watafute jina jingine wanaweza wakajiita THE comedy na si ze comedy na hayo majina wanaweza wakayapindisha kidogo tu kazi inaendelea badala ya kuzidi kulalamika

Haina shida sana waiweke tuu kama hivi THE COMEDY TV SHOW ili mradi wale wahusika wote wawepo kwa maana Joti, Mpoki, na wengineo.
 
Ndugu, hivi niulize, kuna mtu ana haki miliki ya kipaji cha mtu mwenyewe...?? Ndio kwenye jina wanaweza wakawa wana haki miliki. Ninavyojua na kwa jinsi wanasheria wengine (walio wataalamu wa sheria za haki miliki) manake wengine huwa wanakurupuka hali hawajui haki miliki, mtu huwezi kuwa na haki miliki kwenye talent ya mtu bila idhini yake tena ya kimaandishi..!! Yaani in other words, Asha baraka hana haki miliki na style maarufu ya Ally Choki, ndio maana hata alipokuwa anahama, hakuweza kumpiga stop kuitumia. Ukiongelea kipaji, the first beneficiary wa haki miliki (pale panapokuwa hapana makubaliano yaliyo halali na siyo ya kusurutishwa; kwa lugha ya kisheria pasipo na undue influence) huwa ni mtu mwenyewe. Sasa sielewi huyu jamaa wa COSOTA anakurupuka vipi, hali yeye mwenyewe akishirikiana na BASATA waliwahi kumtetea Mengi, Mhavile na Rita Paulsen pale walipowaibia haki miliki vijana wanyonge hali hawa madogo walikuwa na maandishi ya kuwa wamiliki halali wa copyright ya Bongo Star Search (kesi bado iko mahakamani). Wafuatiliaji wa maswala ya sheria mtakuwa mmeisikia. Hayo tuyaache, tu-concentrate kwenye Ze Comedy.

Kwa hiyo, hawa madogo wasinyanyaswe hata kidogo, na ninaomba wataalamu wa sheria za haki miliki wasimame na kuongea facts. Tuachane na hawa wanasheria waliopewa cha juu na kuanza kuwakandamiza vijana wa watu. Pia tukumbuke kuwa hawa vijana hivi sasa wanafadhiliwa na Manji, na kwa wafuatiliaji wa maswala ya kijamii, mtakumbuka ugomvi kati ya Mengi na Manji ulivyoleta gumzo hapa TZ kiasi cha kuburuzana. Kwa hiyo hii ni ishara tosha ya namna ambavyo Bwana Mengi na familia yake pamoja na washirika wake walivyoamua kuwaharibia vijana hawa bila kujua wakidhani wanamharibia Manji ambaye nahisi keshashiba utajiri. Ushauri wangu kwa Mengi na washirika wake ni kuwa, wasilete ugomvi wao na Manji katika maeneo yatakayoumiza wanyonge. Kama wanataka kupambana wakapambane kule BOT au Kempinski ambako ni kwa mapede wenzao. Au if possible wakapambane huku wakiwaumiza matajiri wengine kama kina Mkono, Bakhresa au Rostam kabisa.

Huu ni ukoloni mamboleo ndani ya nchi yetu wenyewe. EATV ningewashauri wakatae mambo mengine lakini sio matumizi ya talents za vijana wa watu ambao waliamua kujituma badala ya kujiingiza katika u-kibaka na matumizi ya madawa ya kulevya. Tumeona vipindi kibao vya TV vinarushwa leo kwenye SABC kesho kwenye channel nyingine kwa mwendo ule ule.

Kwani kuna mtu amewakataza kuendelea kuvuna kutokana na kipaji chao kwa kutumia jina lingine. Hata Jackson Five walipoondoka Motown ilibidi jina waliache! Hawa ni kama boy band. Mjanja amewakusanya, amewajenga, sasa wanataka kumkimbia. Waende lakini jina wamwachie. Hamna ukoloni mambo leo hapa.
 
Mimi nafikiri hatuwezi kutoa rational judgement as much as hatujui content ya mkataba wao na EATV uliku na content zipi na zipi...!!

Suala la haki miliki ni tatizo kubwa sana ktk ulimwengu wa wasanii sio tu wa dunia ya tatu akina Masanja lakini pia hadi akina Jay Z...!!

Kitu ambacho inabidi tujifunze ktk hili ni ''kukosa shule'' kwa wasanii wetu walio wengii nchini!!,its a real problem, mimi nafikiri inabidi wapate challenge kutokana na hili, walau wawe na-basic education, manake bila hiyo hata hiyo akili ya kumtafuta legal adviser wako/wenu uaipata wapi? kumbuka ya kina ''wanaume family/halisi''

Vile vile at the end of the day we should note that this felles are after better fringe benefits no matter where they are and what they are doing!, na hilo hata wewe msomaji wa hii thread inakusukuma ubadili bishara moja hadi nyingine, uende kusoma, uhame mtaa wabiashara, etc, sasa why not them?

Tumikia kafiri upate maji wako wahenga walinena!!
 
huu mtanange si mwepesi ni mtanange wa kukata shoka

ila mnonge mnyongeni haki yake mpeni.

baadhi ya wakati ni jambo la busara kumuacha maskini ajikombewe na kukosea ktk jambo kwa kutokjua akifanyacho isiwesababu ya kuadhibiwa.

vijana wanasaka riziki kwa njia ya halali na jamii inaburudika sasa eatv iwaachie isiwaekee biti na wakati huo huo wajifunze na vikundi vyengine

na sisi kama jamii tujitahidini kuwaelimisha jamii kuelewa sheria si hizi ziko nyingi wako wengi wandhulumiwa kwa kutojua sheria ndogo ndogo tu juu ya shughuli zao.

niliwahi kupendekeza na nitaendelea kufanya hivyo kuwa JF tuanzishe section ambayo itakuwa ikihusika na mambo ya kisheria kuanzia kuitambua katiba yetu haki za msingi za mwananchi na mpaka haya.

pia iwe ni sehemu ambayo watu wanaweza kuleta matatizo yao ambayo yanahitaji msaada wa kisheria au kuzungumzia issue ambazo zinajiri ulimwenguni na kutoa technicality za kisheria
 
Tatizo ze comedy wamekuso legal consuel mzuri wa kuwasaidia, hii issue inaonekana wazi ni kisa kinachondelea kati ya Manji na Mengi.
Ze comedy wanachotafuta ni kuwa na maisha mazuri kama ilivyo kuwa kwa mwanadamu yeyote yule kila mtu anapenda kuwa ktk maisha yaliokuwa kwenye mstari,
 
Na niongezee, watanzania wengi tuna tabia ya kuogopa na kufagilia watu matajiri kiasi kwamba kila anachofanya hata kama ni kinyesi kitaonekana ni pafyumu. Nawaona watu kibao wakiongea hapo juu kuwasapoti EATV. Mi nafikiri ingekuwa busara na hekima kama tungeangalia kama palikuwa na mkataba halali kabisa, wa vijana hawa kushift ownership ya talents zao (i.e. surrender of copyright) to EATV. If upo, then we can say EATV wana haki. Lakini isijeikawa EATV wanaleta janja ya nyani ili kutimiza adhma za pede wao (i.e. kupambana na Manji).

Tuwe waangalifu katika maneno yetu tutatia aibu..!!

Sidhani kama COSOTA wanaweza kukurupuka tu na kuja na hayo maelezo kwamba Ze Comedy waharuhusiwi kuonyesha vipindi vyao TBC bila ya COSOTA kuona mkataba halali ambao una vipengele vinavyogusa hakimiliki. Kwa sasa ni vigumu kujua undani zaidi kwa kuwa wenye uwezo wa kuweka wazi mkataba ni Ze Comedy. EATV kazi yao imekwisha wanasubiri mtu akiuke then wakakutane mahakamani.

Kama Manji alikuwa na nia ya kuiua Ze Comedy basi kawamaliza, maana anaweza kusema alisaini mkataba na Ze Comedy na kama wao wanabadilisha jina then yeye anasitisha mkataba, period! Lengo la Manji siyo kuua biashara ya Mengi au EATV, lengo la Manji ni kulinda maslahi ya mafisadi ili wasije wakaanikwa zaidi na ndiyo maana aliweka kipengele cha ku-approve maigizo kabla hayajarushwa hewani.

Swali jingine, kwanini hakukuwa na mkataba kati ya TBC na Ze Comedy, na badala kuwe na mkataba kati ya Ze Comedy na Manji? Hiyo inaashiria nini?
 
lengo la Manji ni kulinda maslahi ya mafisadi ili wasije wakaanikwa zaidi na ndiyo maana aliweka kipengele cha ku-approve maigizo kabla hayajarushwa hewa
Sasa hapa ni balaa naona sasa hivi ze comedy itakuja na sura nyingine kabisa kama maigizo hadi Manji apitishe hii kali sasa!Umaskini huu tabu sana Fisadi anakutumia jinsi anavyotaka!Ila bora uwe maskini jeuri kwa kuworkhard pasipo shinikizo la fisadi kutaka ufanye anavyotaka yeye!kisa nyumba ?gari? kwani hata kubaki EATV hayo yote wangefanya tatizo ni Tamaa za kutaka utajiri wa fasta fasta!Suleimani alikuwa tajiri lakini yote aliona ni UBATILI mtupu!
Asante
Hollo
 
Au hao ze komedi waombe ETV na TBC wakae kwa pamoja mezani waweke mambo sawa ili kuondoa utata kuliko kila mtu kusema pembeni,( najisikia kucheka sababu wakati natype haya maoni naonaTBC wanawatangaza ze comedy coming soon)
 
Na niongezee, watanzania wengi tuna tabia ya kuogopa na kufagilia watu matajiri kiasi kwamba kila anachofanya hata kama ni kinyesi kitaonekana ni pafyumu. Nawaona watu kibao wakiongea hapo juu kuwasapoti EATV. Mi nafikiri ingekuwa busara na hekima kama tungeangalia kama palikuwa na mkataba halali kabisa, wa vijana hawa kushift ownership ya talents zao (i.e. surrender of copyright) to EATV. If upo, then we can say EATV wana haki. Lakini isijeikawa EATV wanaleta janja ya nyani ili kutimiza adhma za pede wao (i.e. kupambana na Manji).

Tuwe waangalifu katika maneno yetu tutatia aibu..!!

Hakuna aliyesema EATV wana haki miliki ya vipaji vya hao vijana waliokuwa kwenye kundi la Ze Comedy. Mfano Ali Choki alipoona maslahi kiduchu Twanga Pepeta aliondoka baada ya kuona amepatata umaarufu, lakini hakuweza kutumia jina la Twanga Pepeta kwa kuwa sio mmliki wa lebo hiyo. Ndo hivyo hivyo kwa hawa vijana. Kuna tofauti kati ya watu kuanzisha kundi lao la usanii na kulipa jina then kwenda kuomba ajira huko EATV, na EATV kuamua kuanzisha program na kuipa jina kisha kutafuta watu wenye kipaji cha kuigiza katika hiyo program.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom