Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 40,033
- 61,934
Masikini wanatumia nguvu nyingi sana kutaka kuwaaminisha jamii kuwa ni matajiri, kwa kununua vitu vya anasa anasa visivyo zalisha; mfano, masikini atapambana sana kununua nguo za gharama, mikufu na micheni ya gharama, saa za gharama, magari ya gharama, kukodi usafiri binafsi kwa gharama n.k lengo ni kutaka kuwaaminisha jamii kuwa wao sio masikini; wakati kiuhalisia wao ni masikini.
Matajiri hufanya matumizi makubwa kwenye uwekezaji na hawataki kuwaaminisha watu wao ni matajiri; bali matendo yao tu ndio uwaonyesha wao ni matajiri.
Wao watawekeza kwenye mitambo ya uzalishaji, uchimbaji wa visima vya mafuta, uwekezaji kwenye uchimbaji wa gesi, ujengaji wa viwanda vya magari, vifaru, ndege, simu n.k na uvaaji wao huwa ni wa kawaida sana.
Masikini mwenzangu, unakubaliana na hii mada?