Masikini kaka huyu

Masikini kaka huyu

Ila nilisikia sasa hivi vipimo si vya kuamini (na ilikuwa official statement kama niko sahihi)...anaweza jua yuko -ve kumbe vipimo ni vibovu...
 
Hapo penye rangi pananitia kichefuchefu. Naona makanisani hakuna masomo au miongozo ya wanandoa kabla ya harusi.Zaidi ya hapo inaonekana makanisani ni uwanja wa kufanya Uzinzi na uasherati chini ya upako wa shetani.Je serikali ya Yesu Kristo makanisani imepinduliwa??? Mungu tusaidie!!
Habari zenu wana Jf,

Ni moja ya rafiki zangu ni kijana mkimya, mpole, mcha Mungu, ana heshima na mpiganaji katika kutafuta maendeleo, katika pilika pilika zake Mungu akampa binti mzuri, mpole, msikivu na mwenye adabu hapa ndipo mwanzo wa misha yao mpaka ndoa. Kwa sasa wana mwaka mmoja ndani ya ndoa yao na Mungu kawamjalia mwanamke kwa sasa anaujauzito wa miezi miwili katika ile hali ya kuugua ugua akaenda hospital.

Kinachosikitisha na kuhuzunisha ni kijana mwezi huu kagundua mkewe ni muathirika (VVU). Huyu rafiki yangu huwa na mwita kaka ili kukata mzizi wa fitina si unajua mabinti tulivyo. Baada ya kugundua hivyo nikaanza kumuuliza je hawakupima wakati wa maandalizi ya ndoa.? Majibu aliyotoa kiukweli ni huzuni eti hawakuona haja ya kupima kisa wote aliona wametulia na hakukuwa na hisia yeyeote ya uchepukaji na pia walikutana Kanisani.

Nilivyo fyoko fyoko nikauliza vipi mlianza kuzini kabla ya ndoa na mlikuwa mnatumia Condom? akaijbu ndiyo ili kuzuia mimba kwa hiyo walivyofunga ndoa tu wakaanza kunjunjana bila Condom bila hata kujua afya ya kila mmoja.


Mungu si nanjilinji bwana wee kijana hajaathirika kapima zaidi ya mara 7 kila akipima anaona negative kawa kama chizi akipita mjini akiona hospital anashuka anapima aamini majibu anayopata.Lakini kutokana na vipimo inaonekana ajaathirika, kaenda hospital na mkewe doctor wamempa namna ya kuishi na mtu wa VVU lakini ameshindwa kinachotokea kijana analala sebuleni mwanamke chumbani.

Kinachotokea mke kawa na gubu anamlazimisha mwanaume mapenzi (ngono) mwanume hawezi, jamani mimi nimeshindwa mshauri zaidi nilimwambia alale sebuleni au Mzungu wa nne mwanamke amegeuka moto anataka ngono bila hata condom. Jamani naombeni anayeweza toa njia nyingine ya kumsaidia kijana ili waishi at least kwa amani mwenye suluhu

Karibuni, ushauri
 
Hapo penye rangi pananitia kichefuchefu. Naona makanisani hakuna masomo au miongozo ya wanandoa kabla ya harusi.Zaidi ya hapo inaonekana makanisani ni uwanja wa kufanya Uzinzi na uasherati chini ya upako wa shetani.Je serikali ya Yesu Kristo makanisani imepinduliwa??? Mungu tusaidie!!

Mungu atusamehe tu makanisa haya ya majina ya watu wamebadili utaratibu kabisa
 
hatari sasa na unachopanda kwa mwili ndio utavuna ,,,,,,,
 
MWanaNke uyo hana busara kabisa.Yaani yeye kaungua anataka waungue wote!Ningekuwa mi nnao ningeongeza heshima na mapenzi kwa mwenzangu na kushauriana naye kama yuko tayari tuduu kwa zana lakini si nimezama ,nizamishe jahazi tuangamie wote au hii ndo akili zenu miss chagga,masai dada et al?
 
Nawewe mgeni! ckuhizi hakuna cha ndoa ya kikiristo,inavunjwa vzr tu mahakamani kila mmoja anachukua 50 zake,
It seems binti aliupata mwenyewe huyu.

Ila hili kweli jaribu!!
mkuu christine ibrahim alichounganisha Mungu,mwanadamu hawezi kutenganisha! Km mahakani wanatengua ni kwa sheria za mahakama,lkn hawataweza tena kufunga ndoa na wenzi wao wapya kanuni za kikristu.
 
Last edited by a moderator:
Mimi si mtaalamu sana wa afya ila kuna scenario kama hizo nyingi tu. Hawa kitaalamu ni discordant couples ambapo mwanamume sio recipient wa VVU kulingana na blood group au aina ya kinga yake na aina ya HIV aliyonayo mkewe. ... hivyo ushauri wangu wapate ushauri wa kitabibu then goma liendelee,
atakuwa mpumbavu kumuacha mkewe... huenda ndo kipimo pekee cha ubinadamu na uwezo wake katika kuwafia wengine. Mungu hakupi mtihani asioweza kukupa mbinu za kuushinda. ...
 
We unataka kujua nini .? We toa ushauri kwa eafiki yangu

Ok nakushauri uwe rafiki yake katika kipindi hiki cha mpito, wakati huu anakuhitaji kuliko vipindi vingine, tazama sasa upo katika mtihani wa kupima urafiki wenu na unapaswa kuushinda....sema aaaamen!
 
Huyo mwanamke anataka wafe wote au ni nn sasa hicho atleast watumie kinga ili angalau mmoja apone!!ingawa ngumu kumeza

Yaani huyo Mwanamke anataka kuharibu sasa, inabidi amlinde mwenzie asipate maambukizi, waishi kama walivyoshauriwa na daktari
 
Ok nakushauri uwe rafiki yake katika kipindi hiki cha mpito, wakati huu anakuhitaji kuliko vipindi vingine, tazama sasa upo katika mtihani wa kupima urafiki wenu na unapaswa kuushinda....sema aaaamen!

ameeen
 
miss chagga pole sana na jela
Ashikilie msimamo wake bila condom hapana maana hapo mwanamke kashajijua anao anataka amwambukize na mwenzake waupate wote na hiyo ni mbaya sana.

Gubu haliwezi kuisha na wala halitamuua kijana ila akijifanya anafanya bila condom ajue tayari anaupata maana mwanamke inaonekana kadhamiria jamaa aupate na yeye

Asikilize ushauri wa wataalam na akiona yanazidi hapo ni kuwaita wazazi na kuwapa ukweli wa kinachoendelea. Mtoto anaweza kuzaliwa bila kuupata na hapo ajue hata maziwa ya mama hayanyonya

Kama ni mapenzi ampende na kumtimizia kama mke ila kushiriki tendo la ndoa bila mipira asijaribu hata siku moja maana hapo dhamiri ishamtoka huyo mama

Huyo Dada anaonekana sio mtu mzuri sasa, huyo kaka achunge hata mswaki wake, asije kuwa anashare naye kwa makusudi, sijui aliyemfanyia counselling aliwacounsel aje, wakafanyiwe counselling tena sehemu nyingine, na huyo Kaka sawa awe makini but aendelee kumwonyesha upendo, kuongea vizuri, kumtia moyo na kumjali Mkewe, la sivyo huyo Dada atakuwa hatari kwa familia yake na wageni pia humo ndani
 
Back
Top Bottom