Mashirika mengi ya Tanzania hayatekelezi ahadi zao na hayajali muda wa Vijana

Bi huu

Member
Aug 14, 2022
6
3
Naweza nikatumia lugha ya uongo maana ndio maana halisi endapo mtu atashindwa kutekeleza lile aliloliahidi.

Lengo la post hii sio kulichafua shirika lolote lile ila ni kuwakumbusha tu kuwa wasiwachukulie poa vijana wanaowapa kazi.

Mfano mzuri leo hii nitayazungumzia mashirika mawili WATUMISHI HOUSING COMPANY ( WHC) na TANZANIA PRIVATE SECTOR FOUNDATION ( TPSF).

Siku zote tunajua kuwa sanaa na ajira lakini pia ili sanaa ipatikane yenye mvuto vinaitajika vitu viwili ambavyo ni PESA na MUDA.

WATUMISHI HOUSING COMPANY
Tarehe 26 September 2018 walipost tangazo la logo competition na wakaweka mpaka na deadline cha ajabu huu ni mwaka watano (5) sasa wapo kimya hawajatoa feedback yoyote.

20230821_080216.jpg


Sasa kama vijana tunashindwa kuelewa kuwa walikosa logo yenye vigezo wanavyotaka wao au wameghairisha au wamepuuza mda na pesa tulizoweka katika kutengeneza logo.

TANZANIA PRIVATE SECTOR FOUNDATION ( TPSF)
Hawa jamaa nao pia ni wajanja wajanja sijui nini kuna wakutaga maana tarehe 20 September 2020 walitoa Tangazo la kuitaji logo cha ajabu hawajatoa feedback yoyote ile mpaka leo hii.

20230821_081957.jpg


Lakini pia ikafika 14 june 2023 wakapost tena wanataka logo wakatangaza deadline ni tarehe 31 June 2023 na la nyongeza wakasema Tarehe 31 July 2023 watatangaza.

20230821_082904.jpg
Mshindi cha ajabu mpaka leo hii unakimbilia mwezi wa 9 tena wapo kimya.

Nadhani kuna haja Wizara ya sanaa na Utamaduni kuingilia kati hizi inshu maana jamaa wanatupotezea mda sisi ma artist.

Sanaa inaumiza kichwa lakini pia watu tunawekeza pesa na mda wakati wenzetu wanafanya masihara hawatoi feedback yoyote ile.
 
Minafikiri, hili sio jambo la kugombana na hayo mashirika. Chamsingi hayo yote yatazame kama changamoto na endelea kuoambana hadi siku utakapo tusua.
 
Back
Top Bottom