Mashabiki wa Simba wamlilia Rais Samia awezeshe mchakato wa mabadiliko

Mashabiki wa Simba wamlilia Rais Samia awezeshe mchakato wa mabadiliko

Kila mmoja anaongea lake dadeki, kama genge la wauza vijora vile.
 
Yaani binadamu anakuwa na mama wangapi.

Bila shaka hao wameandaliwa na machawa wa Samia ili kumtafutia namna ya kurejea kwa wananchi baada ya mauaji ya halaiki aliyofanya Oktoba 29 mwaka jana.

Sasa anatafutiwa jukwaa kwa nguvu zote na hiyo kazi inafanywa na machawa kama inavyoonekana kwenye video hiyo.

Vilabu vya Simba na Yanga ndio hivyo vinakosa mvuto kila uchao baada ya kukubali vitumike kisiasa na wanasiasa maadui wa nchi.

Hivi vilabu kwa sasa vinaendeshwa na wafanyabishara mafisadi ambao hawalipi kodi ipasavyo kwa kisingizio cha kuvifadhili vilabu hivyo kwa masilahi ya serikali iliyoko madarakani.

Kwa sababu cha kujiuliza ni kwamba hawa wafadhili uchwara hizi fedha wanazotumia katika huu ufadhili kimahesabu zinawekwa kwenye akaunti ipi na maelezo yake kwenye ukaguzi auditing yanatolewaje...!!?? Hapo ndipo tunapogundua kwamba haya makampuni hayalipi kodi kwa idhini ya serikali iliyoko madarakani.

Ikija serikali sahihi iliyochaguliwa na wananchi hayo makampuni yatafirisika mara moja na vivyo hivyo kwa vilabu hivyo viwili.
 
Back
Top Bottom