Last Seen
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 223
- 549
Habari wana jamvi,
Msimu huu Arsenal tuna hali mbaya kuliko Misimu yote iliyopita, Emery alietegemewa kufanya makubwa na kikosi cha Arsenal akakibomoa kikosi kwa migogoro na wachezaji.
Alianza kwa mbwembwe za kufika fainali ya Europa hatimaye akala kipigo kitakatifu kutoka kwa timu iliyokuwa mbovu kwa kipindi hicho, nadhani wachezaji walijiamini sana kutokana na Chelsea haikuwa na wakati mzuri.
Baada ya hapo timu yetu imekuwa kimeo kupitiliza, tumepoteza asili ya mchezo wetu uliotupa heshima na mafanikio wa kupiga pasi nyingi na kumiliki mpira, hata tukifungwa unakuwa ume-enjoi mpira.
Baadhi ya makosa ya Unai Emery yaliogharimu Arsenal:
1. Kocha hakuwa na kikosi cha kwanza cha kudumu. Kwake hata mechi kubwa alikuwa akizitumia kama kufanya majaribio ya wachezaji wachanga.
2. Migogoro na wachezaji wake
3. Kuhamisha wachezaji namba walizozoea.
4. Kubadilisha mfumo wa uchezaji.
Emery ametugharimu sana hadi hatujui lini tutarudi kucheza UEFA. Enzi za Wenger timu ilikuwa mbovu lakini Top 4 lazima.
Sasa ni wakati sahihi wa Arsenal kutafuta kocha mzoefu ili nasi tuanze kupata furaha ya ubingwa!
Kocha gani unahisi ni sahihi kuifundisha Arsenal!?