Mfahamu Ole Gunnar Solkjaer kocha anaetunyima usingizi mashabiki wa Manchester United

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
INAWEZEKANA HATUMFAHAMU KOCHA OLE GUNNAR SOLKJAER . Tarehe 26 mwezi wa pili mwaka 1973 ndio siku rasmi aliyezaliwa Ole Gunnar Solkjaer kule nchini Norway .Maisha yake yote ya utotoni Solkjaer alikuwa anaupenda sana mpira na alikuwa na ndoto ya kuwa golikipa .

Wengi hawajui Ole Gunnar Solkjaer ni mshabiki mkubwa wa Liverpool tangu akiwa utotoni hii ni timu anayoipenda na kuihusudu moyoni kama unavyomuona happy kwenye picha enzi zake za utotoni akiwa ameshika mpira na uzi wake wa Liverpool. Usisahau kama Liverpool ndio mahasimu wakubwa wa Manchester United .

Sir Alex Ferguson ndie aliyemtambulisha kwenye ulimwengu wa soka ambapo mwaka 1996 alienda kumsajili kutoka kwenye timu ya Molde nchini kwao Norway akiwa na miaka 23 tu.Lengo kuu la Sir Alex Ferguson ni kumtafuta mshambuliaji wa akiba atakayewezesha kuwasaidia Andy Cole ,Dwight Yorke na Eric Cantona pale mbele kama siku wakiwa hawana siku nzuri uwanjani.Ole Gunnar Solkjaer alitumika kama super sub maisha yake yote ya mpira amecheza mechi 366 na kufunga magoli 123 mpaka pale alipoamua kustaafu soka mwaka 2007 baada ya kudumu Old Trafford miaka 11 .

Rekodi pekee anayekumbukwa Solkjaer akiwa mchezaji wa Manchester United ni goli lake alilofunga mwaka 1999 fainali ya Uefa dhidi ya Bayern Munich pale uwanja wa Nou Camp .Hana rekodi nyingine kubwa ya kukumbukwa na Manchester United .Christiano Ronaldo alikaa miaka 6 tu Manchester United na akaondoka hila juzijuzi tu karudi nyumbani na kuvunja hiyo rekodi ya Ole Gunnar Solkjaer ya mabao.

Wayne Rooney ,Paul Scholes ,David Beckam ,Eric Cantona ,Giggs,Roy Keane ,Dwight Yorke ,msaliti Paul Ince(aliyeamua kuichezea Liverpool ) ,Andy Cole ,Denis Irwins ,Garry Neville ,Steve Bruce (kocha wa zamani wa Newcastle ) hawa ni wachezaji waliofanya kazi kubwa kuipa heshima Manchester United ambayo inaharibiwa sasa hivi na huyo kocha anayeshabikia Liverpool tangu utotoni.

Hakuwa na mchango mkubwa enzi zake uchezaji Frank Lampard ana heshima kubwa Chelsea kwanza yeye ndie mfungaji bora wa muda wote pale darajani na amedumu miaka karibia 13 hila alipozingua kazi ya ukocha alifukuzwa.Koeman ana heshima kubwa Barcelona enzi zake za uchezaji mwaka 1992 ndie aliyewapa Barcelona Uefa yao ya kwanza baada ya kufunga goli pekee dhidi ya Dortmound fainali. Koeman anashikilia rekodi ya kuwa beki mwenye magoli mengi zaidi amefunga magoli 89 tena hapo akicheza kama nafasi ya beki wa kati.Alikuwa mzuri kwenye mipira ya faulo na hata ya juu hasa vichwa.

Koeman ameipa heshima kubwa Barcelona enzi zake za uchezaji hila alipopewa timu kama kocha na kazi ikamshinda akafukuzwa.Valverde alikuwa mchezaji mzuri enzi zake akiwa Barcelona kashinda mataji ya heshima kama Ligi kuu akiwa Barcelona hila alipokuwa kocha tu wa timu hii na kuleta ujinga akafukuzwa.Kumbuka hawa makocha wote wawili wameshinda mataji pale Barcelona .

Hila Manchester United wanamkumbatia Solkjaer ambaye anautafuta mwaka wa 4 bila taji lolote hata kombe la kuku.Mwenzake Arteta pale Arsenal amekuja muda mfupi tayari kanyanyua kwapa ,muangalie Brendan Rodgers ananyanyua makombe na Leicester City .Unafikiri Leicester City na Arsenal wana vikosi vizuri zaidi ya Manchester United ?Jibu ni hapana kinachowabeba wana makocha wanaojua nguvu na udhaifu wa wachezaji wao pamoja na mifumo sahihi ya kutumia kwenye vikosi.

Wakati sisi tukipigwa nguzo tano za kislamu na Liverpool pale Old Trafford juzi jumapili David Moyes na Westham yake walikuwa wanatupa darasa la bure jinsi ya kufunga Liverpool ya Jurgen Klopp.Unafikiri Westham wana kikosi bora zaidi ya Manchester United hapana hila wana kocha anayejua kutumia mifumo sahihi ya wachezaji.

Leo washabiki wa timu pinzani kila wakicheza na Manchester United wanaimba wimbo wa kejeli "Ole at the wheel "na wanatamani abaki maana wanajua hana mbinu .Mwaka 2014 huyu huyu Ole Gunnar Solkjaer aliwashusha Cardiff city daraja baada ya kucheza mechi 10 huku yeye akishinda 3 na kufungwa mechi 7 hila Glazers wanataka kuendelea kumpa nafasi huyu mshabiki wa Liverpool anayejificha kwenye kivuli cha ulegend kwenye timu yetu.

Wakati nikiwa Chuoni Profesa wangu Hella aliwahi kutupa stori kuwa kuna mtoto alikuwa anatabia ya kufanya makosa kila siku nyumbani ,kila akifanya kosa anakimbilia kuomba samahani .Bahati nzuri bibi yake alimpenda sana maana katika wajukuu zake huyu ndie mtoto zaidi.Ikawa ndio tabia yake ya kufanya makosa kila siku huku akijua akisema "samahani "atasamehewa".Hila siku moja alikuja kufanya kosa la mwaka akiwa nyumbani alisahau kuzima gesi jikoni kwa bahati mbaya nyumba ikaripuka na bibi yake akafariki .Mwishoe akawa hana mtu tena wa kumwambia "samahani akikosea.

Ndivyo alivyo Ole Gunnar Solkjaer anafanya makosa yaleyale Manchester United yanayojirudia kila siku na habadiliki kabisa huku akitumia mdomo wake na maneno matamu ya kuwafariji mabosi wa Manchester United .Wacha waendelee kumlea watakapokuja kushtuka atakuwa tayari ameshaipeleka Manchester United shimoni hata wakimfukuza kwa muda huo itakuwa tayari wamechelewa.Hapo ndipo watakapokumbuka kwa nini ng"ombe kanyimwa ndevu na Mwenyezi Mungu halafu mbuzi kapewa licha ya maumbile yao kuwa tofauti asante.
 
Huyu hapa taahira mmoja anaetuumiza mioyo yetu
IMG-20211110-WA0052.jpg
 
Atakuwa na damu ya baadhi ya wamasai wenye'Ole' kama aki na Ole S..b..ya aliyewakosesha watu usingizi akiwa mwenyekiti wa kamati fulani huko Kaskazini.
 
Mdumu na ole wenu naombea tu mechi na Chelsea awepo ole wenu na arsenal pia awepo yaani muishi naye mfunge naye ndoa ya kikirsto
 
Kwenye ukocha Ole anatakiwa apumzishwe ila kwenye enzi zake za uchezaji mashabiki wa kipindi hicho alitupa kitu roho inapenda. Itoshe kusema ukiwa mchezaji ulikua kipenzi cha old traford "baby face killing asasin" kwenye ukocha amepewa mda wa kutosha lakini hajapata fiest eleven team mpaka leo. Tumponde pale kwenye kumponda tulikupenda sana ukiwa mchezaji ila kwenye ukosha too much disapoitment.
 
Mbona nineandika huko juu??mashabiki wa Liverpool,Arsenal,Chelse na Man city wanamuhitaji Ole kuliko kipindi kingine chochote kwenye maisha yao
Nakazia mzidi kudumu na ole tuna waombea familia ya Glazers wamvumilie. Kwa maana mvumilivu hula mbivu atakua the next Sir Alex .
 
Unafiki mbaya huyu Rio ndiye alisema Man United are back Ole at the wheel na agewe mkataba aandika kiasi cha mshahara anachotaka.
Sawa alikuwa na matarajio nae makubwa sababu anaijua philosophy ya United lkn ka prove felia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom