Mary Masanja Achangia Milioni 21 na Kugawa Mitungi ya Gesi 700 kwa Wanawake Wajasiliamali Wadogo wa Mkoa wa Mwanza

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

MBUNGE MARY MASANJA ACHANGIA MILIONI 21, AGAWA MAJIKO YA GESI 700 KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI WADOGO MKOA WA MWANZA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amechangia Shilingi Milioni 21 na amegawa mitungi ya gesi 700 kwa wanawake wajasiriamali wadogo 700 wa Mkoa wa Mwanza

Mary Masanja amesema lengo ni kuhamasisha wanawake hao kuacha matumizi ya nishati chafu (Kuni na Mkaa) na badala yake watumie nishati safi ili kuhifadhi Mazingira.

Hafla hiyo imefanyika Machi 27, 2023 katika Ukumbi wa Rocky City Mall jijini Mwanza, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Ndugu Reuben Sixbert Jichabu.

Akizungumza katika hafla hiyo, baada ya kukabidhi majiko kwa niaba ya Mhe. Masanja, Bw. Jichabu amewataka wanawake hao kutumia nishati ya gesi ya ORYX katika shughuli zao za ujasiriamali na kuepuka matumizi ya kuni.

Naye, Mary Masanja ameahidi kuendelea kuwaunga mkono wajasiriamali wanawake wa Mkoa wa Mwanza ili waweze kukuza uchumi wao.

Pia, Mary Masanja amezishukuru Kampuni za ORYX ENERGIES & FOMAC kwa udhamini na kufanikisha tukio hilo.
WhatsApp Image 2023-03-27 at 20.49.06.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-27 at 20.50.13.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-27 at 20.49.09.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-27 at 20.50.09.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-27 at 20.50.07.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-03-27 at 20.50.11.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-27 at 20.50.11.jpeg
    236.4 KB · Views: 3
Back
Top Bottom