Marekani yamkamata alievujisha taarifa za siri za kijasusi

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
69803023-11969873-image-a-10_1681412962726.jpg

Kijana Jack Teixeira akielekezwa kwenda kwenye gari ya maofisa wa SWAT kutoka FBI. Picha na CNN

Jack Teixeira kijana mwenye umri wa miaka 21 ambae ni mwanajeshi katika jeshi la anga la Air National Guad ambalo lipo katika mji wa Masachusetts.

Kijana huyo tayari yupo mikononi mwa FBI na atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya Espionage.

Jack amekamatwa mchana huu nyumbani kwake kwenye kitongoji cha Swansea ambapo ameonakana akiwa amefungwa pingu.

Kukamatwa kwa Jack kwafuatia taarifa alozotoa kijana mwingine ambae walikuwa wakicheza pamoja mchezo wa computer na kuona Jack akisambaza taarifa hizo.

Hadi sasa imefahamika kuwa taaarifa hizo zilitokea katika mchezo wa computer yaani "online game" na zilikuwa katika vipande vipande yaani "slides", zikielezea mipango yote ya majeshi ya Ukraine dhidi ya Russia kuanzia mwishoni mwa mwezi March mwaka huu.

Lakini uthibitisho kuwa taarifa hizo ni za kweli bado haujawa wazi ingawa zaonesha udhaifu mkubwa wa majeshi ya Ukraine na matumizi ya hovyo ya silaha jambo linopelekea kumaliza akiba ya silaha walokuwa wakipewa na nchi za NATO.

Pia taarifa hizo zaonyesha idadi kubwa ya majeshi maalum yaani "special forces" kutoka nchi za NATO vikiwemo vikosi vya UK ambao Russia yawachukulia kuwa ndo wachagizaji wakuu wa vita hiyo.

Uvujaji wa taarifa hizo umewastua maofisa wengi wa serikali ya Marekani akiwemo mkuu wa Pentagona ambae nae amesema hafahamu imekuwaje na kudai kuwa taarifa hizo zilikuwa mahala fulani mtandaoni na "hata hata yule aliekuwa amezipata kwa wakati huo hajulikani", amedai waziri wa Ulinzi Llyod Austin.

Shirika la habari la AP lilidai kuwa taarifa hizo za siri huenda zilianikwa katika ukumbi wa mazungumzo au "Chart Room" utumiwao na wachezaji michezo ya computer ujulikano kama Discord na haijulikani idadi halisi ya taarifa hizo na yasadikiwa kuwa ni mamia kwa mamia.

Jack na wenzie wapatao 20 waliunda kikundi chao hicho cha kucheza game online wakati wa Pandemic na wakawa wameshibana.

Kikundi hicho kilikuwa chakutana katika channel maalum ya majadiliano iitwayo Discord na ilikuwa yatumia jina la "End of War Mao Zone" na kilikuwa kikijadili masuala mbalimbali ya historia na siasa.

Baadae kukatokea ubishani mkubwa baina ya wajumbe na kiongozi wa mjadala aitwae "wao mao" amesema baada ya kuhojiwa juzi kwamba mmoja wa Mods wa YT aliamua kusambaza hizo baada ya kuzikuta zimewekwa na Jack katika Server ya Discord.

Jack atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kuondoa nyaraka za siri kutoka zilipokuwepo, kuzihodhi na kuzisambaza kinyume cha sheria.
---
1681457120862.png
Kitengo cha upelelezi cha Marekani (FBI) kimemkamata mlinzi wa anga mwenye umri wa miaka 21 huko mjini Massachusetts kwa madai kuhusika kwenye uvujishaji wa nyaraka za siri za kijeshi (Wizara ya Ulinzi wa nchi hiyo, Pentagon). Soma: Nyaraka za siri za Marekani na mpango wa kumuua Putin zaanikwa

FBI walimkamata Jack Teixeira akiwa nyumbani kwake katika mji wa Dighton Kaskazini. Akifafanua tukio hilo, Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Merrick Garland, amethibitisha kukamatwa kwa mlinzi huyo, huku akieleza kuwa kwamba Teixeira, anashikiliwa kwa kuhifadhi na kusambaza taarifa za siri za Wizara ya Ulinzi wa taifa".

Inaelezwa kuwa Teixeira amekamatwa kutokana na kuongoza kundi sogozi mtandaoni (Online Chat Group) lililokuwa likiwekwa picha na nyaraka nyingi za siri. Kundi hilo lilijiita Thug Shaker Central lilianzishwa Machi, 2022 na mamia ya picha na taarifa nyingi za siri zimekuwa zikiwekwa hapo.

Kutokana na tukio hilo Teixeira atakabiliwa na mashtaka chini ya Sheria ya Ujasusi. Inaelezwa kuwa kila shtaka chini ya sheria hiyo linaweza kubeba hadi kifungo cha miaka 10, Waendesha mashtaka wanaweza kuchukulia kila hati iliyovuja kama hesabu tofauti katika mashtaka yake.
 
""Kumatwa kwa Jack kwafuatia taarifa alozotoa kijana mwingine ambae walikuwa wakicheza pamoja mchezo wa computer na kuona Jack akisambaza taarifa hizo""

Marafiki sio.

Always SNITCHING.

#YNWA
Ni marafiki hucheza michezo hiyo.

Yes, yule kijana mwingine ni chanzo cha New York Times hivyo amepata mshiko tayari.

Ndo dunia ilivyo.
 
Jack Teixeira kijana mwenye umri wa miaka 21 ambae ni mwanajeshi katika jeshi la anga la Air National Guad ambalo lipo katika mji wa Masachusetts.

Kijana huyo tayari yupo mikononi mwa FBI na atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya Espionage.

Jack amekamatwa mchana huu nyumbani kwake kwenye kitongoji cha Swansea ambapo ameonakana akiwa amefungwa pingu.

Kumatwa kwa Jack kwafuatia taarifa alozotoa kijana mwingine ambae walikuwa wakicheza pamoja mchezo wa computer na kuona Jack akisambaza taarifa hizo.
Dúh huyu analo kama assange. Sasa zilifike mikononi mwake wakati si top official ambaye anaweza kuwa certified kuwa na top secret docs
 
Yawezekana yeye kapewa na mhusika mkuu ambae huenda asijulikane.
Nimetoka kumsoma dogo, kazi aliyokuwa anafanya kwenye base ni pamoja na kupitia classified docs na lengo lake halikuwa kuvujisha alikuwa tu anajimwambafy kwenye group ambalo yeye alikuwa admin na baada ya docs kusambaa aliogopa sana na kaanza zipost toka mwaka jana ila zilikuwa hazijasambaa hadi mwaka huu.
 
Back
Top Bottom