Kukamatwa na kushitakiwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumeibua mjadala, ambapo nchi ya Marekani imeshauri kuwepo na majadiliano kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na vyama vya upinzani.
Hayo yameelezwa jana na Naibu Waziri wa Nchi wa Masuala ya Siasa wa Marekani, Victoria Nuland alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kufuatia mkutano wake na Rais Samia na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa hapo jana.
Waziri huyo alisema miongoni mwa mambo aliyozungumza na Rais Samia ni hofu ya Marekani kwenye utaratibu uliotumika kumkamata na kumshitaki Mbowe, huku akiomba Serikali ifuate misingi ya haki na sheria katika kesi hiyo.
“Ni muhimu kabisa kwamba hali hii itatuliwe kwa njia itakayofuata sheria kwa uharaka na uwazi. Hiyo ni muhimu katika kukuza nguvu ya demokrasia nchini Tanzania,” alisema.
Nuland alisema ana matumaini kuwa suala hilo litapatiwa ufumbuzi kwa majadiliano baina ya pande zote mbili, baada ya wote kuonyesha utayari wa kukutana na kulizungumza.
“Kwa mtazamo wangu pande zote mbili ni wazalendo na wana malengo mema, kwa hiyo ni vyema wakatumia nafasi hii ya utayari walionao kupata ufumbuzi wa kidemokrasia,” aliongeza.
Waziri huyo pia amemuomba Rais Samia kujenga kasi ya hatua zilizochukuliwa wakati wa siku za kwanza za urais wake ambako alijitahidi kuondoa vizuizi kwa vyombo vya habari na kutangaza mazungumzo makubwa na asasi za kiraia.
Pia alimsihi Rais Samia, kuhakikisha ulinzi wa haki za binadamu na raia wote watendewe haki chini ya sheria, bila kujali ushirika wao kisiasa.
“Wakati anaanza na matamanio makubwa kidemokrasia na wapinzani pia walionyesha utayari kumuunga mkono, hatua nzuri sana zilishachukuliwa mwanzoni,” alisema.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Balozi, Liberata Mulamula alisema Rais Samia alipanga kukutana na wapinzani lakini ratiba zikaingiliana.
Chanzo: MWANANCHI, 5 AUGUST 2021
My take:
Sarakasi za wahafidhina wanaomshinikiza Samia ndani ya CCM zinaelekea ukingoni. Soon
US waweke shinikizo ivyo ivyo..Mungu wabariki Wazungu
Siku zao zimekwishaUS waweke shinikizo ivyo ivyo..
Aibu sana kwa Siro na huyu mrembua macho.
Mwambie kama kweli ni iron lady akuze uchumi aache siasa za kishamba hazisaidii nchi.Kama una akili timamu hiyo ni kesi ya kubumba so usishabikie ujinga .Mbowe amekosea timing......huu sio muda wa Siasa za matusi na zilizokosa adabu. Cdm wasingatie sheria hakuna aliye juu ya sheria.
Never underestimate woman...she is iron lady in polite face. Siku Mia moja tu alibadili mfumo mzima wa mtawala mwenzake! She is who she is....watahitaji huruma sana ya mataifa ya nje. Watakuja,watasema,wataongea mwisho wataondoka.
Ubongo wako umejaa kamasi pole Sana.Mama asicheke na magaidi hata kidogo,aendelee kuwadhibiti washalegea wamekata tamaa kwa jinsi anavyowapiga pini.
Chadema ni nan ktk nchi hii acheni kuoverrate iko chamaJinsi Samia anavyozidi kujiweka mbali na upinzani hususan Chadema, ndio hali yake na serikali yake inazidi kuwa mbaya
Ujinga mtupu.Mambo ya usalama wa ndani ya nchi yatabaki kuwa ya nchi.
Tanzania is a sovereign coutry.
ila Chadema hakikufaa kabisaa kuwa chama cha upinzani nchini Tanzania kwa tabia ya mara kwa mara wanayo ionyesha inapo tokea jambo lolote basi wanaenda kuichongea Tanzania kwa mataifa makubwa wakitegemea Viongozi wetu wataogopa!! thubutu!!!! kamwe tusivumilie tabia hii ya kizandiki!!! labda wakafanye siasa zao Burundi lkn sio Tz..
Tunaomba viongozi wetu wasiyumbe kabisa, wawe imara kusimamia sheria za nchi.
Demokrasia sio kuvunja amani.
Usalama gani wa kubambikia watu kesi,kwa hiyo unashabikia watu kuonewa .Mimi nataka Kila raia wa Tanzania bila kujali chama chake awe na haki ,haya mambo ya kuoneana hayakubaliki kwa watu wanaojielewa .Mambo ya usalama wa ndani ya nchi yatabaki kuwa ya nchi.
Tanzania is a sovereign coutry.
ila Chadema hakikufaa kabisaa kuwa chama cha upinzani nchini Tanzania kwa tabia ya mara kwa mara wanayo ionyesha inapo tokea jambo lolote basi wanaenda kuichongea Tanzania kwa mataifa makubwa wakitegemea Viongozi wetu wataogopa!! thubutu!!!! kamwe tusivumilie tabia hii ya kizandiki!!! labda wakafanye siasa zao Burundi lkn sio Tz..
Tunaomba viongozi wetu wasiyumbe kabisa, wawe imara kusimamia sheria za nchi.
Demokrasia sio kuvunja amani.
Mbona Mandela na Nyerere ndio walikua wanaomba duniani kuwapiga vikwazo Afrika Kusini na S.Rhodesia? Ni kitu cha kawaida kuomba intervention ya Nchi washirika hata Burundi wakivurugana au Rwanda tunaona kina Mkapa wanaenda kusuluhisha unless haujui maana ya diplomasiaMambo ya usalama wa ndani ya nchi yatabaki kuwa ya nchi.
Tanzania is a sovereign coutry.
ila Chadema hakikufaa kabisaa kuwa chama cha upinzani nchini Tanzania kwa tabia ya mara kwa mara wanayo ionyesha inapo tokea jambo lolote basi wanaenda kuichongea Tanzania kwa mataifa makubwa wakitegemea Viongozi wetu wataogopa!! thubutu!!!! kamwe tusivumilie tabia hii ya kizandiki!!! labda wakafanye siasa zao Burundi lkn sio Tz..
Tunaomba viongozi wetu wasiyumbe kabisa, wawe imara kusimamia sheria za nchi.
Demokrasia sio kuvunja amani.
Hakuna mtu mwenye akili timamu na mawazo huru ataandika uliyoyaandika.Tusi tayari.....
Siri ni mpuuzi kama mwendakuzimuSiro sijui huko aliko anajiskiaje
Mbowe alimtukana Nani na wapi mbowe alifanya siasa za matusiMbowe amekosea timing......huu sio muda wa Siasa za matusi na zilizokosa adabu. Cdm wasingatie sheria hakuna aliye juu ya sheria.
Never underestimate woman...she is iron lady in polite face. Siku Mia moja tu alibadili mfumo mzima wa mtawala mwenzake! She is who she is....watahitaji huruma sana ya mataifa ya nje. Watakuja,watasema,wataongea mwisho wataondoka.
We mjinga kwa hiyo mnaona fahari kuonea wapinzani wenu kisa ni sovereign country acheni ushama nyie lumumba Ila ipo siku mtatamani kukaa na hao mnao waita magaidi lakini mtakuwa mmesha chelewa tendeni haki mtabalikiwaMambo ya usalama wa ndani ya nchi yatabaki kuwa ya nchi.