Marekani yaifungua iPhone ya Mlipuaji

Acha kutangaza biashara zako za kitapeli hapa kiujanja ujanja ili watu waingie kingi uwatapeli na hao matapeli wenzako wa Sijui k/koo. Niletee hata simu moja hapa ambayo mmeishaitoa icloud hapo k/koo?
k.koo android tu zinawapa shida
 
Mkuu mbona covert operation nying tu zinapigwa na watu tunajua ingawa mamlaka husika hazijawah comment? hata china wandukua american firms daily lakin hawasemi?ulitegemea FBI waje hazaran waseme hivyo? kitu unachotaka ww kwe issue za ki intelligent km hcho hakiwez tokea lakin watu tunasoma habari kupitia third part...yaan unachotaka wewe chombo cha habari kitangaze kwamba iran imesema inahusika kulipua waisrael pale ujeruma wakati wa olimpic? au iran kulipua wayahudi kule argentina?haiwezekan mkuu
 

Basi jifunze ku qualify kauli zako.

Huwezi kutumia declarative statement kuelezea speculations zako na za wengine.

Hakuna, mpaka sasa, yeyote yule mwenye mamlaka aliyesema kuwa Muisrael ndo kaifungua hiyo simu.

Bali, kilichopo ni speculation tu.
 
Basi jifunze ku qualify kauli zako.

Huwezi kutumia declarative statement kuelezea speculations zako na za wengine.

Hakuna, mpaka sasa, yeyote yule mwenye mamlaka aliyesema kuwa Muisrael ndo kaifungua hiyo simu.

Bali, kilichopo ni speculation tu.
dah mkuu kama na hapo juu hujanielewa ntakua nmeshndwa hoja yako mkuu...but kuna vitu mkuu mamlaka husika haziwez comment hata cku moja....usitegemee kuwa iran watakiri kuwapa silaha waasi wa houth yemen...usitegemee mamlaka za russia zitasema kuwa russia inawapa silaha waasi wa ukraine wanaisumbua serikali ya ukraine lakin vtu hivi vipo na watu wanajua kuwa vinatokea..lakin sasa ukisema upewe source ya mamlaka husika inayothibitisha haya mkuu hutapata
 

Sasa kama mamlaka husika hawawezi kusema, wewe mamlaka ya kutoa declarative statement unayatoa wapi?

Hivi unajua hata maana ya declarative statement ni nini?

Unajua kwa nini, kwa mfano, hata kile chanzo ulichonipa hakikusema moja kwa moja kuwa Muisrael ndo kaifungua?

Wewe kubali tu kuwa, kilichopo ni speculation kuwa huenda kampuni ya Kiisrael ndo inasadikiwa ilihusika katika ufunguaji huo.

Unajua maana ya speculation ni nini? Maana nisije kuwa natumia misamiati ambayo labda hata huijui au huielewi!
 
hahahaa nna wasiwasi ushakuwa brainwashed sana mkuu kama kila kitu huwa unasubiri official statement, maana hata ZEC walituambia uchaguzi wa marudio ulikua fresh coz ulishirikisha vyama vyote na wananchi wakamchagua muheshimiwa kwa asilimia tisini na........
 

Kama unadhani nimekuwa brainwashed [sijui hata na nini], basi unakosea sana.

Kwangu ni suala la umakini tu.

Umakini wa kutambua mambo au vitu kama vilivyo na si visivyo.

Kama ni tetesi, basi acha na ziwe tetesi.

Lakini si kuzifanya tetesi ziwe ukweli.

Hivi unaelewa hata tofauti ya tetesi na ukweli?
 
fresh mkuu,we had a good conversation sema bahati mbaya tumetofautiana mawazo ni kitu cha kawaida broo
 
Binafsi naipongeza sana apple kwa kutokubali kuifungua hiyo simu. kazi kwako Invisible na JF kwa ujumla kulinda na kutetea yetu humu ndani
 
FBI wamejidharirisha sana! Kweli wanashindwa kutengeneza software za ku-track hizo iphone! Haikua ishu ya kuwasumbua apple hii! Naanza kutowaamini hawa jamaa kwenye ushushu wa kitecnokojia. Kuna hila hapa.
 
Tetesi zilizoko ni FBI walishirikiana na engineer kutoka Jeshi la Israel wakafungua hyo simu.

Mkuu, usipende kushabikia tetesi maana hutakuja kuelimika.

Suala la uchunguzi wa kisayansi au forensic investigation ni la kawaida nchini Marekani, Ulaya, Australia, na baadhi ya nchi za kiarabu kama Saudia na Kuwait.

Sasa hivi katika uliwengu wa teknolojia, kuna masuala kama ya usalama na nyenzo za kusaidia uimarishaji wa usalama huo au utenguaji.

Kuna wahitimu wengi tu wenye shahada ya forensic and criminal investigations na polisi wa nchi nilizozitaja hapo juu wanawategemea watu hawa katika uchunguzi wao.

Siku hizi kuna kampuni ambazo zinaingia mikataba na polisi wa nchi hizo katika uchunguzi wa kesi za mauaji, utekaji watoto wa kike na wanawake ambao baadae wanauawa, makosa ya mitandao na mwisho udondoaji wa data kutpka kwenye vyombo kama simu za mkononi na tablets.

Moja ya kampuni hizo ni ya waisraeli inaitwa Cellebrite ambayo ndio wamewasaidia FBI kufungua simu ya Farouk.

Hii ni kampuni maarufu sana kwa kuwa na teknolojia ya kufungua simu za mkononi kwa kutumia advanced tools and technology.

Tarehe 19-20 mwezi wa 4 kutakuwa na maonyesho ya bidhaa za usalama na mitandao mjini London nchini Uingereza, maonyesho yanaitwa Forensic Euro Expo.

Lakini kabla ya hapo kutakuwa na maonyesho mjini Zagreb nchini Croatia tarehe 5/4/16 yanayoitwa DATA FOCUS 2016- Intrnational Conference On Digital Evidence.

Halafu tarehe 12-14 April 2016 maonyesho yatakuwa mjini Rio de Janeiro nchini Brazil.

Hivyo ndivyo mambo yanavyoendelea.
 
FBI wamejidharirisha sana! Kweli wanashindwa kutengeneza software za ku-track hizo iphone! Haikua ishu ya kuwasumbua apple hii! Naanza kutowaamini hawa jamaa kwenye ushushu wa kitecnokojia. Kuna hila hapa.

FBI hawajajidhalilisha kwa sababu wenzetu wanagawana majukumu ya kazi.

Hivyo wao wanawategemea wataalam wengine katika kufanikisha shughuli zao za uchunguzi.

FBI hawawezi kuhodhi kila utaalam maana kuna watu wanajifunza utaalam wa kila namna.
 
WAWADANGANYE WAJINGA !

Simu ilikua erased baada ya kujaribu kuweka wrong passcode zaid ya mara 10!

Na baada ya iPhone kua erased hata ukifanikiwa kuifungua hukuti chochote kwa hio wanajifagilia tu hakuna chochote walichosoma labda walifanikiwa kuifungua tu.
 
Ha ha ha...sio kila kitu cha ku comment bibie...we endelea kufuatilia habari za mtoto wa diamond na makalio ya wema huko ndo uko vizuri...hivi vitu technical tuachie tulioenda shule na kufaulu
[emoji1] [emoji1] [emoji1] umenifurahisha sana mkuu, eti endelea kufuatilia habari za mtt wa daimond na msambwanda wa sepenga huko ndo yuko vizuri,[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
hapo mwisho kwenye issue ya usalama ndo penye point kuu, ila mwanzo ulianza kwa porojo za kiswazi.
 
ndio maana nilisema ni tetesi,sikutaka kujiaminisha wala kumuaminisha mtu.Asante kwa maelezo yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…