Marekani kuitikisa Tanzania kwa vikwazo

Marekani kuitikisa Tanzania kwa vikwazo

Kumbuka ukiwekewa sanction nchi washirika na US nazo huunga mkono. Kiushabiki unaweza kuhisifu eti utakula mahindi. Usiombee ban, vifaa vyote unapigwa marufuku kununua, madawa vipuri vyote huwezi. Angalau nchi kama Iran walijitutumua kwa kuwa wenzetu wana wanasayansi kwa kiasi chake wale walioiba Technology walijizatiti, ingawa wananchi walipata na kiukweli wanapata hadi sasa. Kwa mtu anaefikiria maslahi ya Taifa hawezi kamwe kusema vikwazo viwekwe tu kisa maslahi ya chama. Ni upuuz uliopitiliza
pengine tukiwekewa sanction tutapata akili...ni kama maisha ya kawaida ukimchukua kijana anayejitegemea amepanga nyumba ni tofauti sana na kijana anayekaa kwa wazazi wake kimawazo na kimtazamo....
 
Aisee tutakosa visa magu na kampuni yenu msitutikie vitumbua vyetu mchanga
 
Kweli tutaisoma namba tutakapo anza kukosa ile misaada inayosemaga kwa hisani ya watu wa marekani.
 
Tupo tayari
maneno hayo unaongea ukiwa umeshika kiroba au bange mkononi au unaongea ukiwa umejitoa ufahamu ikiwa matangazo tu ya malaria ni kwa hisani ya watu wa marekani so kama mmeshindwa hata kugharamia matangazo hata kwenye tbc mpaka walipa kodi wa marekani wawalipie ikiwa bajeti yenu 60% ni misaada kwa waisani sasa ameanza us kesho utackia uk na eu mtakula pumba mwaka huu kwa sababu ya mijitu ya mtaa wa lumumba
 
maneno hayo unaongea ukiwa umeshika kiroba au badge mkononi au unaongea ukiwa umejitoa ufahamu ikiwa matangazo tu ya maralia ni kwa hisani ya watu wa marekani so kama mmeshindwa hata kugaramia matangazo hata kwenye tbc mpaka walipa kodi wa marekani wawalipie ikiwa bajeti yenu 60% ni misaada kwa waisani sasa ameanza us kesho utackia uk na eu mtakula pumba mwaka huu kwa sababu ya mijitu ya mtaa wa lumumba
Wewe ndio huna uhakika, jiandae kuishi kwa kutegemea wahisani, kwa taarifa yako hadi sasa kwa mwezi January mapato yameisha vuka lengo 2trions zishaingia hazina. Wewe wasubiri baba zako commonwealth na wamarekani wakubebe.
 
jamani ifikie hatua tuwe wakweli hivi mnavyoona tunalima tunakula ndo tujione tunaweza kujitosheleza? wale jamaa wakiamua tutakiona cha moto wenzetu wenye viburi wanauchumi mkubwa sisi je? kama madawa yalitushinda unstegemea tutaweza wenyewe? ARV's zenyewe msaada hakika bila US tutayumba
Kuna kiwanda cha ARV bongo...!
Na sijawahi sikia vikwazo kwenye madawa...ndio maana nawaita nyumbu!
 
REA ni katika miradi ambayo weananchi wamepandikiziwa vijjijini.Vijiji vingi wala havihitaji umeme na havina umeme.Vingi nyaya za umeme zinapita mbele ya nyumba zao wala hakuna anayehitaji.Mahitaji ya wananchi wala si umeme wanachohitaji ni masoko ya uhakika ya mazao yao.Hiyo REA hata waifute kesho hakuna atakayeingia barabarani kulalamika.
...Acha kukejeli miradi ya maendeleo, inayoboresha maisha ya wananchi vijijini. Vijiji vipi hivyo ambavyo havihitaji umeme? Hao ambao hawahitaji umeme wala hawatakuwa na uwezo wa kuhitaji masoko. Simply, those kinds would not be producing any surplus for trading.

...Au una maana ukali wa wabunge kugombania miradi ya umeme kufika maeneo yao, ni danganya toto?

...Ina maana kituo cha afya maeneo hayo hakina haja ya umeme? Shule zilizopo huko pia hazina haja ya umeme? Mashine za kukoboa na kusaga nafaka nazo hazihitaji umeme?

...Jambo la kwanza haitakuwa kuingia barabarani, hiyo REA ikisisimama. Wabunge wataichinja Serikali bungeni mchana kweupe!

...Acha hasira!
 
mkuu huwezi ifananisha Korea kaskazini na TZ, korea asilimia kubwa ya bidhaa zao wanazalisha wenyewee, ni vitu vichache sana wanaagiza toka nje.

Sisi chakula chenyewe tunacholima hakitoshi kutulisha wote.

Dola ikianza kupaa kwa hivi vikwazo ndipo utajua uchumi wa dunia umeshikiliwa na mataifa makubwaa
Mkuu tusiende Iran ni mbali sana, hapo Zimbabwe tu tujifunze, pesa yao hakuna mwananchi anae taka haina thamani, ni dola kwenda mbele, yule dicteta amejaribu kubadilisha pesa hoo, wananchi hawaitaki haina thamani
 
100% great thinker
REA ni katika miradi ambayo weananchi wamepandikiziwa vijjijini.Vijiji vingi wala havihitaji umeme na havina umeme.Vingi nyaya za umeme zinapita mbele ya nyumba zao wala hakuna anayehitaji.Mahitaji ya wananchi wala si umeme wanachohitaji ni masoko ya uhakika ya mazao yao.Hiyo REA hata waifute kesho hakuna atakayeingia barabarani kulalamika.
 
Tatizo we mkuu Ibilisi inaelekea ni miongoni mwa watu wasiofuatilia mambo kwa karibu.
JPM anajenga Tanzania ya viwanda hivyo miaka kama miwili ijayo kama sio miezi sita kuanzia sasa, sisi tutakuwa main exporters kwenda kwa EU, USA na kwingineko na usije shangaa bandari ya Dar es Salaam itakuwa imejaa makontena ya export hata wezi wa makontena hawatakuwa na cha kuiba ndugu!
Ukishawekewa sanction hata hivyo viwanda ni kazi bure hutafanya biashara na washirika wa Marekani ambao ni wengi zaidi ya unavyofikiria

Juzi juzi tu meli za iran zilikamatwa imewekwa bendera ya Tanzania muulize Kikwete kilichomkuta

Inawezekana wengi humu hamjui madhara ya hiyo sanction la sivyo hakuna ambaye angefurahia hilo...
 
...Acha kukejeli miradi ya maendeleo, inayoboresha maisha ya wananchi vijijini. Vijiji vipi hivyo ambavyo havihitaji umeme? Hao ambao hawahitaji umeme wala hawatakuwa na uwezo wa kuhitaji masoko. Simply, those kinds would not be producing any surplus for trading.

...Au una maana ukali wa wabunge kugombania miradi ya umeme kufika maeneo yao, ni danganya toto?

...Ina maana kituo cha afya maeneo hayo hakina haja ya umeme? Shule zilizopo huko pia hazina haja ya umeme? Mashine za kukoboa na kusaga nafaka nazo hazihitaji umeme?

...Jambo la kwanza haitakuwa kuingia barabarani, hiyo REA ikisisimama. Wabunge wataichinja Serikali bungeni mchana kweupe!

...Acha hasira!
Kwa miaka mingapi wanavijiji wameishi bila huo umeme?

Hao wenye umeme kama Dar si lamu wana kipato zaidi ya kinachopendekezwa?

Uwezo wa kukusanya na kufinance hiyo miradi upo ni upuuzi tu wa tabia za wapuuzi mithili ya hawa wanaolilia mabwana wa kizungu.

Solar kwa ajili ya kituo cha afya inaweza kucost sh milioni 6 ...je kiasi hiki kinashindikana mpaka tusubiri msaada wa wazungu?
 
Mliona yaliyoikuta Zimbabwe?! Mkate kuuzwa elfu ishirini! Nyinyi fanyeni mzaha na kitu kinachoitwa vikwazo! At urusi na iran pamoja na ubabe wao wanaogopa vikwazo
 
Mkuu watu wengine sijui wanaishi Dunia gani? Haya mambo ya kujitia masikini jeuri hayatatufikisha popote!

Tusipokuwa makini suala la Zanzibar linaweza kufuta sifa zote nzuri za Taifa letu pamoja na Serikali ya JMT, may be Serikali ya Zanzibar inajiona hawana cha kupoteza ndio maana wanaonekana kutojali maoni ya International Community - lakini wakae wakijua kwamba stance ya Serikali ya Zanzibar kuhusu kurudiwa tena uchaguzi zitamwaribia sana Dk.Magufuli kimataifa.

Ni jambo lililo wazi wanataka kulazimisha mambo na kuiweka Tanzania kwenye hali tete, kama matokeo ya vituo karibu 30+ matokeo yake yalisha bandikwa ukutani kulikuwa na ulazima gani wa kufuta uchaguzi? Kwani kuna ulazima gani wa Chama tawala kushinda Bara na visiwani, Watanzania si wanabaki wale wale bila ya kujali itikadi ya vyama vyao, mbona manispaa za Ilala na Kinondoni zinaongozwa na Mameya wa vyama vya Upinzani - kwani kuna kitu gani kilicho haribika.

Tufike mahali tukomae kisiasi tusipalilie vurugu na machafuko yasiyo ya lazima - na ukiangalia kwa umakini wanao palilia sintofahamu wengi umri wao umekwenda wanategemea vijana watajifunza/rithi kitu gani cha maana kutoka kwao.

Narudia tena kusema kwamba wasitake kulingiza Taifa letu pamoja na Dk.Magufuli katika hali ngumu, tutakuja kutengwa Kimataifa na kuwekewa vikwazo tukaponzwa na misimamo yenu hisiyo eleweka/yenye utata mtupu, tukumbuke hasiye kubali kushindwa simshindani.
Kwa hiyo siku hizi ukitaka kushinda uchaguzi unawahi kujitangaza???

Hujui unachokipalilia wewe...kila mgombea akitumia technique ya kujitangaza kabla wenye mamlaka hawajatoa jina la mshindi kutakalika??

Kama mnapendwa hadi na jumuia ya kimataifa rudini kwenye uchaguzi mchaguliwe tena...mnachoogopa ni kipi kama hamkuchakachua?
 
Back
Top Bottom