Marekani kuitikisa Tanzania kwa vikwazo

Marekani kuitikisa Tanzania kwa vikwazo

Kenya ilipigwa vikwazo na kuzuiwa kukopa kwa zaidi ya miaka 25 Kilichofanyika Kenya walijenga uwezo wao wa kujitegemea sasa hivi asilimia 99 ya bajeti hawategemei msaada wa mtu.Vikwazo vinasaidia kujenga nationalism tutarudi kwenye siasa ya ujamaa ndilo suluhisho pekee la kupambana na ubeberu wa kimataifa

Sera hizo za vikwazo kwa Africa zitawawakia wenyewe wanaoweka.Tutahamia moja kwa moja kwa wachina wasiopenda upuuzi wa kushirikisha mambo ya siasa kwenye mambo ya uchumi.
Unajua tofauti ya VIKWAZO na kunyimwa MISAADA?
 
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!

Hatuwezi kuishi kwa misaada pekee ....na inatakiwa kuulinda uhuru wetu kiukweli!!
nchi masikini ambayo imeshindwa kutengeneza hata pamba ya kuoshea vidonda japo inalimwa kanda ya ziwa ina uhuru gani ?
 
hao wanamambo yao tuu wana uchungu na gesi kwa kua kapewa mchina sehemu kubwa
 
nchi masikini ambayo imeshindwa kutengeneza hata pamba ya kuoshea vidonda japo inalimwa kanda ya ziwa ina uhuru gani ?
Huna taarifa kwamba pamba na gauze zinatengenezwa hapa hapa bongo ....halafu unajiita jina kubwa la ki-medic...NYUMBU MNA SHIDA SANA
 
W
kwan bila marekani tutakufa njaa
japo siafik ubakaji wa demokrasia uko ZNZ lkn shobo za kuwashobokea WHITE FORKS sizipendi kinoma mbna KOREAKASKAZINI wameweza bila marekani japo wakati wanaanza kukaza uzi walibezwa sana najua HATUWEZI KUJIFANANISHA NA KOREA KASKAZINI ila zama za sasa tujitengenezee mazingila ya kujitegemea wenyewe muda ndo huu wa kujenga nchi yetu TANZANIA afrca kwa ujumla tufufuke tuache uchu wa MADALAKA wangapi wababe walikuwapo leo awapo duniani
koba
MOBUTU SESESEKO JONAS SAVIMBI SANKARA wako wapi wamefukiwa na Bado maisha yanaendelea dunia tunapita tu



White focks ni kiswahili ?
Mbona tayari ume shoboka na lugha yao.
 
Na
HESHMA YA NCHI INALINDWA KWA KUSIMAMIA UHURU NA TARATIBU ZAKE. IFIKE MAHALI TUACHANE KUSHABIKIA MISAADA NA TUJIJENGEE UTANADUNI WA KULIPA KODI NA KUKUSANYA MAPATO KWA UADILIFU. TAKWIMU ZA MAPATO YA NOVEMBA NA DESEMBA 2015 ZINAONYESHA TUNAWEZA KUSANYA MAPATO YATAKAYOTOSHELEZA KUTEKELEZA BAJETI YOTE. JINAMIZI MISAADA NI WAKALA WA UMASKINI NA UTUMWA WA KIFIKRA. TUNA KILA KITU NA MH. RAIS ANADHAMIRA YA DHATI. TUULINDE UHURU WA TANZANIA NA TUULINDE MUUNGANO WETU KWA NGUVU ZOTE. MAPINDUZI YA ZANZIBAR HAYANA BUDI KULINDWA NA KUHESHIMIWA KWA GHARAMA YOYOTE MAANA NDIO FAHARI YA KILA MZANZIBARI NA ISHARA YA UHURU WAO NA VYOMBO VYAO VYA MAAMUZI.
Baada ya hapo tutaweza kufuta uchaguzi kwa raha zetu!!akishinda flani tunafuta!!!itakuwa hakuna WA kutuuliza,safi sana
 
Wakiweka vikwazo na sisi itabidi tukakamae nao uwekezaji wao nchini kwetu .Ni heri tuwape wachina kuliko kuwapa wanaotusumbua na ujinga wa vikwazo mara sijui hamruhusu mashoga mtatukoma ujinga mtupu kila kona.Tuachane nao biashara iishie hapo.Kila mtu aende akaendeshe siasa kwake
Hizi nchi zote za Ulaya na Marekani nani wanatoa misaada mingi zaidi?

Ni nchi zipi zinaongiza kwa kuchangia bajeti yetu zaidi?

Wakati ule JK anaishi airport na angani alikuwa anenda nchi zipi zaidi na kwanini?

Nchi ikiwekewa vikwazo unafikiri China itatusaidia katika mambo gani hasa?

Je,Iran alipowekewa vikwazo je kwanini China haikumsaidia.

Je China nao wanadhamira ya dhati sana nasisi tujitegemee kwa kutupa misaada yao?
 
hiyo misada ya mcc wabaki nayo kwasasa tanzania hatuitaki hata hivyo sisi siyo vilema wa kusaidiwa,hiyo misaada wawape mashoga wa hukohuko


Kumbuka ukiwekewa sanction nchi washirika na US nazo huunga mkono. Kiushabiki unaweza kuhisifu eti utakula mahindi. Usiombee ban, vifaa vyote unapigwa marufuku kununua, madawa vipuri vyote huwezi. Angalau nchi kama Iran walijitutumua kwa kuwa wenzetu wana wanasayansi kwa kiasi chake wale walioiba Technology walijizatiti, ingawa wananchi walipata na kiukweli wanapata hadi sasa. Kwa mtu anaefikiria maslahi ya Taifa hawezi kamwe kusema vikwazo viwekwe tu kisa maslahi ya chama. Ni upuuz uliopitiliza
 
Mikataba inaweza kufilia mbali asikudanganye mtu.Uchukulie umenunua nyumba kijijini una hati zote.Halafu ukaanza kutukana wanakijiji kuwa uongozi wao haufai halafu kila siku wanakijiji wanakujia na mapanga na marungu kwamba funga virago uondoke.Utaondoka tu

Na ndivyo sultani wa Zanzibar alivyoondoka alikuwa na mikataba yote ya kisheria ya kutawala Zanzibar siku ya siku wakamwibukia alitimka mbio mikataba hata uulize iko wapi hajui.Alivyotembezewa kipigo na mikataba yake

Mkataba ukisaini wa kibiashara unasimamiwa na mahusiano mema.Si kwamba maadamu unao unafikiri waweza tu lindwa na mkataba tu lazima uchunge usijiingize kwenye mambo yanayoweza athiri biashara zako.
Tuambie serikali wanaweza wakaivunja vip hiyo mikataba...maana umeeleza vema kuhusu sultani lakini umekwepa kuhusu serikali itakavyovunja hiyo mikataba...au itavunjwa kama ilivyovunjwa ya sultani?una maana hiyo
 
kuna watu humu wanatetea uovu wa ccm badala ya kuangalia maslahi yetu kama taifa...tz tukiwekewa sanctions manayake sio tu kunyimwa misaada hata kufanya biashara na mashirika ya nje ya nchi hakuna......kampuni yoyote inayofanya kazi na Tanzania inapigwa ban marekani....iran baada ya sanctions kuisha juzi raisi wao bila kupoteza muda amekimbilia ulaya kutafuta wawekezaji na kununua ma ndege jinsi hali ilivokua ngumu, wana gesi nyngi walikua hawajui pa kuipeleka..leo hii kuna mburula humu wanakwambia sanctions sio tatizo tutarudi enzi za ujamaa yaani nchi badala ya kusonga mbele tunarudi nyuma kwenye ujamaa...ccm magufuli angalia maslahi ya nchi kwanza sio ccm
Acha hiyo wakibaniwa tu ARV mbona wataachia tu wenyewe
 
jamani ifikie hatua tuwe wakweli hivi mnavyoona tunalima tunakula ndo tujione tunaweza kujitosheleza? wale jamaa wakiamua tutakiona cha moto wenzetu wenye viburi wanauchumi mkubwa sisi je? kama madawa yalitushinda unstegemea tutaweza wenyewe? ARV's zenyewe msaada hakika bila US tutayumba
 
mnaodharau bado shule inawasumbuaa.

Iran iliwekewa vikwazo pamoja na kwamba ni taifa kubwa lkn nchi ilitikisika kiuchumi, sasa sisi sijui kipi kinatupa kiburi.
Mkuu watu wengine sijui wanaishi Dunia gani? Haya mambo ya kujitia masikini jeuri hayatatufikisha popote!

Tusipokuwa makini suala la Zanzibar linaweza kufuta sifa zote nzuri za Taifa letu pamoja na Serikali ya JMT, may be Serikali ya Zanzibar inajiona hawana cha kupoteza ndio maana wanaonekana kutojali maoni ya International Community - lakini wakae wakijua kwamba stance ya Serikali ya Zanzibar kuhusu kurudiwa tena uchaguzi zitamwaribia sana Dk.Magufuli kimataifa.

Ni jambo lililo wazi wanataka kulazimisha mambo na kuiweka Tanzania kwenye hali tete, kama matokeo ya vituo karibu 30+ matokeo yake yalisha bandikwa ukutani kulikuwa na ulazima gani wa kufuta uchaguzi? Kwani kuna ulazima gani wa Chama tawala kushinda Bara na visiwani, Watanzania si wanabaki wale wale bila ya kujali itikadi ya vyama vyao, mbona manispaa za Ilala na Kinondoni zinaongozwa na Mameya wa vyama vya Upinzani - kwani kuna kitu gani kilicho haribika.

Tufike mahali tukomae kisiasi tusipalilie vurugu na machafuko yasiyo ya lazima - na ukiangalia kwa umakini wanao palilia sintofahamu wengi umri wao umekwenda wanategemea vijana watajifunza/rithi kitu gani cha maana kutoka kwao.

Narudia tena kusema kwamba wasitake kulingiza Taifa letu pamoja na Dk.Magufuli katika hali ngumu, tutakuja kutengwa Kimataifa na kuwekewa vikwazo tukaponzwa na misimamo yenu hisiyo eleweka/yenye utata mtupu, tukumbuke hasiye kubali kushindwa simshindani.
 
Taifa la Marekani linatarajia kushusha rungu la aina yake kwa serikali ya Tanzania kufuatia hali ya sintofahamu inayoendelea nchini kutokana na sakata la uchaguzi mkuu wa Zanzibar.

Habari zinadokeza kuwa taifa hilo kubwa duniani litaweka vikwazo vya kiuchumi kwa Tanzania hali itakayopelekea Tanzania kuandika historia nyingine mbaya mbele ya uso wa dunia.
Serikali ya Marekani tayari imezuia misaada mbalimbali kwa Tanzania na pia ndiyo iliyoshinikiza Tanzania kunyimwa fedha za MCC. Hata hivyo serikali ya Tanzania bado haijatilia maanani jambo hilo huku ikioneknana kupuuza juhudi za kimataifa kuitaka kuumaliza kwa haraka mgogoro wa Zanzibar unaofukuta kwa kuacha haki ichukue mkondo wake.
Habari zinadokeza kuwa balozi wa Marekani nchini atatoa msimamo unaoelezwa kuwa 'mkali' ili kuishinikiza serikali ya Tanzania kuheshimu maamuzi ya wananchi kwenye uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika mwezi october mwaka jana ambao ulielezwa kuwa huru na wa haki.
Sometime we should not fear superpower countries.
 
kwan bila marekani tutakufa njaa
japo siafik ubakaji wa demokrasia uko ZNZ lkn shobo za kuwashobokea WHITE FORKS sizipendi kinoma mbna KOREAKASKAZINI wameweza bila marekani japo wakati wanaanza kukaza uzi walibezwa sana najua HATUWEZI KUJIFANANISHA NA KOREA KASKAZINI ila zama za sasa tujitengenezee mazingila ya kujitegemea wenyewe muda ndo huu wa kujenga nchi yetu TANZANIA afrca kwa ujumla tufufuke tuache uchu wa MADALAKA wangapi wababe walikuwapo leo awapo duniani
koba
MOBUTU SESESEKO JONAS SAVIMBI SANKARA wako wapi wamefukiwa na Bado maisha yanaendelea dunia tunapita tu
Pitia ulichoandika wala haueleweki. Sijui Sankara umemuwekaje hapo?
 
Back
Top Bottom