Marekani kuitikisa Tanzania kwa vikwazo

Marekani kuitikisa Tanzania kwa vikwazo

Taifa la Marekani linatarajia kushusha rungu la aina yake kwa serikali ya Tanzania kufuatia hali ya sintofahamu inayoendelea nchini kutokana na sakata la uchaguzi mkuu wa Zanzibar.

Habari zinadokeza kuwa taifa hilo kubwa duniani litaweka vikwazo vya kiuchumi kwa Tanzania hali itakayopelekea Tanzania kuandika historia nyingine mbaya mbele ya uso wa dunia.
Serikali ya Marekani tayari imezuia misaada mbalimbali kwa Tanzania na pia ndiyo iliyoshinikiza Tanzania kunyimwa fedha za MCC. Hata hivyo serikali ya Tanzania bado haijatilia maanani jambo hilo huku ikioneknana kupuuza juhudi za kimataifa kuitaka kuumaliza kwa haraka mgogoro wa Zanzibar unaofukuta kwa kuacha haki ichukue mkondo wake.
Habari zinadokeza kuwa balozi wa Marekani nchini atatoa msimamo unaoelezwa kuwa 'mkali' ili kuishinikiza serikali ya Tanzania kuheshimu maamuzi ya wananchi kwenye uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika mwezi october mwaka jana ambao ulielezwa kuwa huru na wa haki.
Zimbabwe hadi leo bado ina survive na vikwazo bado vnaendelea,,,viva jpm!!
 
kama nchi za scandinavia na japan ndio wangeweka vikwazo ningeshituka kwani marekani msaada wao huwa hauna nguvu pesa nyingi zinarudi kwao na kwa kasi ya kukusanya mapato ya tra sioni tishio lolote kama maji yakizidi unga itabidi tubane matumizi yasiyo ya lazima kama posho za wabunge,ruzuku za vyama na mifuko ya jimbo nawashukuru sana wakizuia misaada kwani ndio tutaona uwezo wa watendaji wetu
Hii misaada ni mbinu ya kuwatengenezea ajira wazungu wenyewe....uliza madirector wa hizo program utaambiwa ni kina nani.

Ukisaidiwa flash ya buku kumi inapigwa chata kwa msaada wa watu flani....

Halafu chama kikubwa cha upinzani kinakimbilia kuwalilia....wakipewa nchi kwa style ya kutetewa na muzungu unategemea watarudisha fadhila gani??

Shame!
 
Kawaulize wa Iran, watakupa jibu zuri mno

Mkuu naona baadhi yetu tunajitia kuwa ng'ang'ari kwa kuwa hatujawahi kuonja joto la jiwe la kuwekewa vikwazo!

Mataifa ya magharibi yakihamua kufanya kweli tutajuta kuzaliwa,mambo mengi ya kimaendeleo yatakwana - hata mafuta tutakosa labda yatoke Iran na Angola lakini na wao wanaweza kuwekewa shinikizo na Merikani especially Angola, masuala ya Zanzibar tusiyafanyie mchezo, tutakuja juta siku si nyingi kuanzia sasa.
 
Huna chako hapo ulipo hiyo bandari itabakia na stori tu vikwazo vikianza, hiyo dhahabu hutauza, hiyo Tanzanite utapopolea ndege... Hiyo Pamba utakula mwenyewe hakuna kiwanda kitacho survive hapo

Mnajipa matumaini kama wagonjwa wa ukimwi lakufikiria la muhimu ni kudai haki hapo Zanzibar... Hii kujitia ujuaji itawatokea puani
Unauza dhahabu,Tanzanite na Pamba kiasi gani kwa sasa??unaingiza kiasi gani ??
 
Unauza dhahabu,Tanzanite na Pamba kiasi gani kwa sasa??unaingiza kiasi gani ??
Sasa ni bora kuuza kiasi gani na kuingiza kiasi gani au bora kutokuuza kabisa

So unakubali kwamba CCM imeshindwa kusimamia hizo biashara ikiwemo ya Utalii pia?
 
Again jaribu kutulia mkuu!!

Labda unanijibu kwa kunifananisha na YEOHADA...ndio maana unajibu vitu visivyoeleweka.
...Usijikunekune unaponijibu. Tulia!

...Ulipo quote majibu yangu kwa YEHODAYA kuhusu REA, ulikuwa unajua context yake, au ulidandia mbele tu? Uliyasoma ukaelewa?

...Mie si mjinga mwenzako! Tujadili mambo kwa hoja, tafadhali.

Kwa hiyo leo nikikuwekea umeme shida zako zitakuwa zimeisha na utaanza kuishi kwa raha??
...Umeme unaleta maendeleo, popote pale unapofika kwa uhakika, bei nafuu na wakutosha. Maendeleo hupunguza shida, na kuboresha maisha.

...Umeme ni kitu cha muhimu katika jamii yeyote duniani. Maendeleo ya viwanda, yataletwa bila umeme? Maendeleo ya kilimo, yatapatikana bila umeme?
 
Zimbabwe hadi leo bado ina survive na vikwazo bado vnaendelea,,,viva jpm!!
Zimbabwe hai survive inatembelea choke wala usitaketufikie alipofikia Zimbabwe haina uchumi wa kujivunia anagangamala kwasababu hataki kutoka madarakani

Wewe unafikiri akiingia Rais mwingine pale atang'ang'ania hayo?!
 
kama nchi za scandinavia na japan ndio wangeweka vikwazo ningeshituka kwani marekani msaada wao huwa hauna nguvu pesa nyingi zinarudi kwao na kwa kasi ya kukusanya mapato ya tra sioni tishio lolote kama maji yakizidi unga itabidi tubane matumizi yasiyo ya lazima kama posho za wabunge,ruzuku za vyama na mifuko ya jimbo nawashukuru sana wakizuia misaada kwani ndio tutaona uwezo wa watendaji wetu
...Kuwekewa vikwazo na yeyote yule si jambo zuri. Mara nyingi vikwazo huwekwa kwa ushirikiano. Tusifikirie wala kupenda kufika huko.
 
Hivi kuna kitu tunategemea wamarekani wasipotupa tutakufa? maana naona kama vyakula tunalima wenyewe na ndio tunavyoishi, biashara tunafanya za kwetu ndani ya afrika mashariki na tukikomaa zaidi tunakwenda kwa marafiki zetu china, tumeanza kuthibiti mapata yetu ya ndani , kama mbwai na iwe mbwai sema no 2 ombaomba. Kama ni neti za mbu wala hazikutusaidia lolote kwani tulibadilisha matumizi na kuwa nyavu za kuvulia samaki , fensi za bustani na vibanda vya kutunzia vifaranga vya kuku

Kama hujui, nenda karibia hospitali zote nchini asilimia kubwa ya mashine za maabara ni msaada toka marekani, bado ARV's na CTC clinic zote nchini zinaendeshwa kwa msaada wao.

Kumbuka blood bank zilikuwa na huduma nzuri zikiwa chini ya wamarekani baada tu ya kuzikabdhi serikani huduma zimesimama

Tafakari...
 
...Ukiwa hujatulia unao wote tuko sawa?

...Wewe na YEHODAYA ni mtu mmoja? maana hujatulia, unawashwa, unajikuna, hadi kusahau context ya hoja hii.


...Wanaishi kwa taabu. Nami pia!


...Unafahamu REA inachangiwa na kina nani?

...Unafahamu REA ni yetu wenyewe kwa fedha zetu wenyewe?

...We umezoea kuuza uhuru? Inaonekana humfahamu mzaziyo we!


...Tofauti ni kubwa! Unafikiri kwanini vijana wanakimbia huko kwenda Dar kutafuta maisha?


...Kama haujui. Kila siku tunakubali conditions!

...Issue hapa haikuwa kuwekewa hiki au kile! Issue ni REA kama mradi wa maendeleo, ambao wewe a.k.a YEHODAYA umeupondea!

On a side note, ina maana miradi yote hii ya umeme ambayo Serikali inawekeza, inapoteza muda na fedha?
SUPER - Well said, well done mkuu Dar-si-Lamu.
 
kwan bila marekani tutakufa njaa
japo siafik ubakaji wa demokrasia uko ZNZ lkn shobo za kuwashobokea WHITE FORKS sizipendi kinoma mbna KOREAKASKAZINI wameweza bila marekani japo wakati wanaanza kukaza uzi walibezwa sana najua HATUWEZI KUJIFANANISHA NA KOREA KASKAZINI ila zama za sasa tujitengenezee mazingila ya kujitegemea wenyewe muda ndo huu wa kujenga nchi yetu TANZANIA afrca kwa ujumla tufufuke tuache uchu wa MADALAKA wangapi wababe walikuwapo leo awapo duniani
koba
MOBUTU SESESEKO JONAS SAVIMBI SANKARA wako wapi wamefukiwa na Bado maisha yanaendelea dunia tunapita tu
ningekuona mjanja kama ungekua unajiweza lakini ujiwezi na kila uchwao unawapigia magoti kuomba msaada lazima wakuendeshe
 
Chini ya jembe Magufuli hatuhitaji misaada
...Chini yake, kama mambo yataenda vizuri, ndio tutapata misaada mingi, zaidi ikiwa katika kuboresha miundombinu.

...Tayari msaada toka watu wa Japan, unaenda kujenga barabara ya juu pale TAZARA kwenye junction ya Nyerere Road na Mandela Road.
 
Nasemaje, wafute tu misaada yote, tutafute kwa jasho letu... watu wanaitumia hiyo misaada vibaya sana... Kuna project nyingi sana chini ya USAID zinazotakiwa zilipe wafanyakazi mishahara mikubwa sana... lakini unakuja kupewa punje punje tu zote wanachukua hao wanaaojita wakubwa...
Jeuri hiyo mnayo na huu ufisadi? Miaka zaidi ya hamsini ya Uhuru bado hamjaweza kujitosheleza kwa neti za mbu wa malaria , hata matangazo ya kujikinga na malaria na ukimwi kwenye TV utasikia kwa udhamini wa Marekani, ndiyo mtaweza kujitosheleza kiuchumi kweli,? Kontena zipotee kwa maelfu, mapesa yabebwe kwa magunia benki na leo wahusika wanaingoza bunge ndiyo utegemee kujitosheleza kiuchumi?
 
Bavicha hivyo vikwazo vitatuhusu na kutuathiri wote sio mnashangilia tuu...angalieni zimbabwe..!

Kimsingi hakuna cha vikwazo wala nini..
 
Asiejua madhara ya kunyimwa misaada umuulize Salmin Amour rais wa Zanzibar wa awamu ya tano. kiwewe cha kukosa misaada kilimtumbuwa maradhi na sasa anakufa pole pole kitandani. Magufuli ajifunze kutoka kwake.
 
Back
Top Bottom