Marekani kuanza kusitisha ufadhili wa fedha kwa WHO ndani ya siku 30 zijazo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Rais wa Marekani Donald Trump ambaye anakabiliwa na uchaguzi mkuu mwaka huu ambaye amekosolewa jinsi anavyotatua ugonjwa huo nchini Marekani , amelaumu China kwa kujaribu kuziba mlipuko huo na kuilaumu WHO kwa kushindwa kuiwajibisha China.

Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza kwamba usitishwaji wa mchango wa Marekani kwa Shirika la Afya Duniani, WHO, utaanza kutekelezwa mara moja ndani ya siku thelathini, ikiwa shirika hilo halitafanya "maboresho" makubwa.

Marekani imelishutumu Shirika la Afya Duniani kwa kuruhusu ugonjwa wa Covid -19 kushindwa kudhibitika na kuupuuzia hatari ya ugonjwa huo, ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu duniani.

Mlipuko wa Corona tayari umewauwa zaidi ya watu 316,000 ulimwenguni, na Merika ndio nchi iliyoathiriwa zaidi na vifo vya zaidi ya watu 90,000 na karibu watu milioni 1.5 wameambukizwa virusi vya Corona.

Rais Trump ambaye ameendelea kukosoa Shirika hilo la kimataida kwa usimamizi wake dhidi ya janga la Covid-19, ametoa mwezi mmoja kwa WHO kupata matokeo muhimu.

"Iwapo WHO haitafanya maboresho makubwa ndani ya siku 30, nitabadilisha uamuzi wa awali wa kusitisha kwa muda mchango wa fedha wa Marekani kwa shirika hilo na kuchukuwa hatu muhimu na kusitisha uanachama wetu kwa Shirika la Afya Duniani" , Bw. trump ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Rais wa Marekani Donald Trump , ambaye anakabiliwa na uchaguzi mkuu mwaka huu ambaye amekosolewa jinsi anavyotatua ugonjwa huo nchini Marekani , amelaumu China kwa kujaribu kuziba mlipuko huo na kuilaumu WHO kwa kushindwa kuiwajibisha China.

Wakati huo huo Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema tathmini huru ya jinsi janga la virusi vya Corona linavyoshughulikiwa itaanzishwa haraka iwezekanavyo na China imeunga mkono hatua hiyo.
 
Wakati huo huo Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema tathmini huru ya jinsi janga la virusi vya Corona linavyoshughulikiwa itaanzishwa haraka iwezekanavyo na China imeunga mkono hatua hiyo

Mzizi wafitna utakatwa hapa...

Sent using My COVID-19
 
Hahahaha hasira za kufa kwa raia wake anataka amalizie WHO
Wakati huo huo Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema tathmini huru ya jinsi janga la virusi vya Corona linavyoshughulikiwa itaanzishwa haraka iwezekanavyo na China imeunga mkono hatua hiyo

Mzizi wafitna utakatwa hapa...

Sent using My COVID-19

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Achana na Marekani, sasa hivi tunaye SuperPower wa ukweli, anaipa mapesa mengi zaidi WHO, zaidi ya asilimia 200 ya hizo pesa za Trump.

2020-05-19 10.53.42.png
 
Kufuatia mzozo unaoendelea juu ya namna ya kushughulikia janga la virusi vya corona, Rais Trump ameonya kwamba iwapo WHO, haitofanya maboresho muhimu katika kazi yake katika muda wa siku 30, Serikali yake itasitisha pia michango yake WHO kwa muda wa kudumu.

Trump ameonya kuwa Marekani pia itatafakari upya uanachama wake ndani ya Shirika hilo, tayari mwezi April Trump alitangaza usitishwaji wa muda wa malipo akidai WHO wamefeli kupambana na corona.

(via @dw_kiswahili )
 
RAKI BIG,
Marekani anachangia zaidi ya dola million 400,china anachangia dola million 40 (arobaini),kwanini WHO wasifyate mkia
 
Marekani raisi ni taasisi mkuu

Hivyo kama ni taasisi kwa kutumia twiti yake tu serikali inachukua maamuzi? Narudia tena, bila bunge na senate kuidhinisha Trump hawezi kujitoa WHO wala kuacha kupeleka michango kama kawaida.
 
Mkuu, hakuna cha veto power ya rais. Ila hawezi kujitoa WHO na michango atapeleka tu. Hizo statement ni mwendelezo wa ku inflict fear kwa jamii.

Mjadala ni ishu ya WHO, pata time pitia opinions za wanasiasa wa US kuhusu ishu hiyo.
Nshapitia saana lakin jua kwamba WHO wasipo toa ushirikiano matokeo yanayofuata ndio hayo, kwani alivyo freeze michango kwa muda aliomba kibal senete?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nshapitia saana lakin jua kwamba WHO wasipo toa ushirikiano matokeo yanayofuata ndio hayo, kwani alivyo freeze michango kwa muda aliomba kibal senete?

Sent using Jamii Forums mobile app

Haja freeze michango yoyote, zile ni siasa za jukwaani tu mkuu. Kumbuka bila UN hakuna US kama super power. Sio WHO tu, ni karibu mashirika yote chini ya UN Marekani ndio mchangiaji mkubwa, na hii ni kwa sababu anatumia UN organs kuonesha nguvu zake. Sasa kujitoa WHO ambayo ndio wanaitumia kwa tafiti zao sio rahisi.

Ni rahisi kwa Trump kutolewa madarakani kuliko yeye kujitoa WHO. World architect won`t allow that.
 
Haya niliokwambia na uliokua unabisha umeona sasa?? Haya mwanaume kaitoa america WHO bila senete unasemaje hapo?
 
Back
Top Bottom