Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,632
- 697,796
Hii mada itawakera wale wenzangu na mimi wenye mapenzi yaliyopitiliza kwa taifa la Marekani! Lakini ukweli mchungu ni kwamba AMERICA WILL NEVER BE GREAT AGAIN...! what a painful truth!
Akiwa kwenye kampeni za kinyang'anyiro cha urais mgombea wa kiti hicho bwana Trump alirudiarudia maneno haya. '....I want to make America great again...'! Yaani ataifanya Marekani itamalaki katika utukufu tena! Ndoto za Alinacha hizi...!
Kanuni za maisha zinasema kwamba ni rahisi kuwa namba moja lakini ni vigumu kubakia kwenye nafasi hiyo....
Mmarekani kwa kulitambua hilo alifanya kila namna abaki kileleni lakini WAKATI SI MILELE...! Na kila jambo na majira yake...hii ni Kanuni ya kiasili kabisa
Ahadi ya bwana Trumph ya kutaka kuifanya marekani itamalaki tena katika utukufu ni ushahidi tosha kuwa marekani ya juzi na jana si ya Leo na hapo kesho!
Where is the American pride now? Zile tambo za ....we Americans kwenye kila jambo ziko wapi? Tulichoshuhudia kwa kiwango cha juu kabisa ni kukataliwa kwa bwana Trump kama rais wa marekani japo kura maarufu zimempa urais...tunachoendelea kushuhudia ni dhihaka kejeli matusi na hata tuhuma za udukuzi na kusaidiwa kushinda na mataifa adui!
Leo hii Marekani ndio inaongea lugha hizi kweli? Ule ufahari na kujikweza umepotelea wapi? Yale mambo yaliyozoeleka kusikika dunia ya tatu hasa Africa nyakati za chaguzi Leo hii ndio yanasikika marekani? Kweli...!!?
Itakuwa vigumu kukubaliwa na wengi lakini ukweli mchungu ni kwamba AMERICA WILL NEVER SHINE AGAIN...!!!!