Marekani haitatamalaki katika utukufu tena

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,606
696,728
13b2a12da2198acc06b1491cae5f2595.jpg


Hii mada itawakera wale wenzangu na mimi wenye mapenzi yaliyopitiliza kwa taifa la Marekani! Lakini ukweli mchungu ni kwamba AMERICA WILL NEVER BE GREAT AGAIN...! what a painful truth!

Akiwa kwenye kampeni za kinyang'anyiro cha urais mgombea wa kiti hicho bwana Trump alirudiarudia maneno haya. '....I want to make America great again...'! Yaani ataifanya Marekani itamalaki katika utukufu tena! Ndoto za Alinacha hizi...!

Kanuni za maisha zinasema kwamba ni rahisi kuwa namba moja lakini ni vigumu kubakia kwenye nafasi hiyo....
Mmarekani kwa kulitambua hilo alifanya kila namna abaki kileleni lakini WAKATI SI MILELE...! Na kila jambo na majira yake...hii ni Kanuni ya kiasili kabisa

Ahadi ya bwana Trumph ya kutaka kuifanya marekani itamalaki tena katika utukufu ni ushahidi tosha kuwa marekani ya juzi na jana si ya Leo na hapo kesho!

Where is the American pride now? Zile tambo za ....we Americans kwenye kila jambo ziko wapi? Tulichoshuhudia kwa kiwango cha juu kabisa ni kukataliwa kwa bwana Trump kama rais wa marekani japo kura maarufu zimempa urais...tunachoendelea kushuhudia ni dhihaka kejeli matusi na hata tuhuma za udukuzi na kusaidiwa kushinda na mataifa adui!

Leo hii Marekani ndio inaongea lugha hizi kweli? Ule ufahari na kujikweza umepotelea wapi? Yale mambo yaliyozoeleka kusikika dunia ya tatu hasa Africa nyakati za chaguzi Leo hii ndio yanasikika marekani? Kweli...!!?

ac36854e0a3d7656dab9ede60aba2345.jpg


Itakuwa vigumu kukubaliwa na wengi lakini ukweli mchungu ni kwamba AMERICA WILL NEVER SHINE AGAIN...!!!!
 
Kwanza sitaki kuamini moja kwa moja hiyo kauli kutoka marekani.kwamba wamedukuliwa katika mfumo wa kumpata mshindi wa uraisi.mbwa mpe jina baya uendelee kumsimanga.

Hii ya utawala kufika kikomo, haliepukiki ila sio kizazi hiki cha karne 21.

China wanakuja kwa nguvu, walifurahi socialism ya urusi na ussr yao kuvunjika sasa wataisoma namba
Mfamaji kamwe haishi kutapatapa Marekani hatakubali kushindwa kirahisi lakini ndio hivyo tena wakati si milele
 
Sishangai madai ya ''kudukuliwa'' na Russia kwa DNC na Uchaguzi Mkuu kama ni kweli (conclusively) ama la.. Nachoshanga ni the so called ''Greatest Nation On Earth'' (Kama tunavyoaminishwa/hata kama ni uhalisia) kubaki kuwa crybaby... Hivi ka nchi kama Libya (enzi za Gadafi) wangefanya hivyo (kuhack) ... wangekuwa washafanyiwa kitu mbaya siku nyingi... Na hao Russia ''ubavu'' wanaupata wapi kuichokonoa Marekani kwenye sensitive issue kama uchaguzi wa Rais?
 
Mnajidanyanya nyingi....wapo watu Serikali ya America wanawaza baada ya miaka 50 america itakuwaje....mmekalia humu Jamiiforum porojoporojo hata hujui hatma yako Kesho itakuwaje....
Kuna wakati usione kila kitu ni porojo za mitandaoni labda tu kama hufuatilii nini kinaendelea marekani kuanzia marekani ya Bush Jr mpaka kufikia sass
Kama wenyewe wanakiri kuwa mambo si mambo....lakini wewe unasema ni porojo mmh!
 
Ila sikuandika ili watu waamini hilo sihusiki nayo...! Nimeandika uhalisia wa mambo kuamini au kutoamini hilo ni jambo lingine kabisa
Wewe ni mjuzi wa maandiko, umesoma biblia hata elimu dunia haijakupita, Je hukusoma wewe kuwa dunia na vyote vitapita?

Tusubiri hayo mabadiliko mtambuka.

Yaani Urusi itakuwa kimbilio la wanyonge?

MUNGU atufanyie wepesi katika aliyotupangia
 
Its like it was written ...... USA will fall the dollar will fall and Russia na China will rise... and then the war then the Jews control the world n bring the Ant-C.
 
Marekani ni taifa lililo pale juu kwa unafiki na umbea tu nothing else, kuchonganisha na kulaghai Marekani ndo kwao lengo likiwa moja tu, kuonekana wao ni great nation.
96404bea44206a0f3ddd1190bf512887.jpg

Its like it was written ......USA will fall the dollar will fall and Russia na China will rise...and then the war then the Jews control the world n bring the Ant-C.
f74dd4e4384ecf78bb1f23d8df6c5ee3.jpg
 
Ukiweka kando uchaguzi uliomalizika hivi karibuni, viashiria vya kuanguka kwa US kama super power ni vingi zaidi.
Mataifa ya mashariki yanainuka kwa kasi kubwa; kiuchumi, kijeshi, Technology n.k.

Washirika wake nchi za Ulaya kimsingi walishafilisika zamani. UK kwa mfano, ubabe wao umebakia library na si kwingineko.
Nadhani huu ni wakati wa nchi changa kusimama zenyewe ili wengine wakianguka pasiwepo na wafuasi wa kuwafuata shimoni.
 
36 Reactions
Reply
Back
Top Bottom