Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,027
- 20,517
NINAVYO UTAZAMA MRADI WA REFINERY KENYA.
Jana Kenya na Dangote wamezindua mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta huko Lamu Kenya. Ni hatua muhimu sana, na ni mradi unaotazamwa kama alama ya uchumi imara wa Kenya wenye thamani ya dola Bilioni 20.
Lakini kwangu nautazama tofauti kidogo, Nafikiri ni haki kwamba Afrika Mashariki ielewe na kuufahamu kwa kina mkataba ulioingiwa kwa ajili ya Kiwanda hiki cha Kusafisha Mafuta cha Dangote kabla majirani hawajaanza kushangilia.
Hebu nikurejeshe nyuma hadi Lagos, Kiwanda cha Kusafisha Mafuta cha Dangote kule Lagos kilizinduliwa mwaka 2023 na kikaanza kuuza mafuta mwishoni mwa 2024. Kabla ya kiwanda hicho, huko Nigeria, mafuta yalikuwa yakiuzwa kwa bei ya N898 kwa lita (sawa na shilingi 87 za Kenya) nchi nzima ya Nigeria, lakini leo tunapozungumza mafuta (petroli) yanauzwa N1,450 kwa lita (Sawa na shingili 141 za Kenya).
Yaani Kiwanda hicho kimetengeneza Naira Bilioni 17.8 kwa miezi 6 (Sawa na shilingi Bilioni 1.74 za Kenya) huku Wanigeria wakilipa pesa nyingi kuliko wakati wowote. Hivyo ndivyo hutokea unaposhangilia kabla ya kusoma masharti na vigezo. Katika hili naona Dar es na Kampala zililing'amua.
Kabla Dangote hajakubali kujenga kiwanda Lamu aliweka masharti matatu magumu. Sharti la kwanza ni soko la uhakika. Kenya, Uganda na Tanzania lazima zikubali kununua mafuta yote yaliyosafishwa kutoka Lamu.
Nchi yoyote ambayo itajitoa kununua lazima isaini dhamana ya kulipa, yaani utalipa hata kama huchukui mafuta. Sharti la pili ni bomba la mafuta ghafi. Kenya lazima ijenga bomba kutoka Lamu hadi Turkana kwa gharama yake yenyewe ili kulisha kiwanda kwa mafuta ya Turkana pamoja na mafuta ghafi ya ziada kutoka Uganda na Sudan Kusini.
Sharti la tatu ni ardhi na mtaji wa awali. Ardhi ya Lamu tayari imeshapatikana na shingili Bilioni 21.5 za Kenya tayari zimekwishatengwa. Kwa ufupi Wakenya watalipia ardhi, watalipia bomba na bado watalipa Bilioni 64.7 za Kenya ili tu kumiliki asilimia 10. Ni nchi gani inayojitambua itakubali mkataba wa aina hiyo?.
Baada ya hapo Kenya na wadau wake walazimishwa kisheria kununua mafuta kutoka Lamu kwa miaka 20 hata kama mafuta ya bei rahisi yatapatikana Dubai au Urusi.
Ni katika eneo moja tu muhimu ambapo Mradi ni mzuri, kwa sababu utatoa ajira zaidi ya 60,000 lakini masharti haya ni mtego na maumivu zaidi kwa Kenya na wabia. Kiwanda kinachompatia mtu mmoja Bilioni 1.74 za Kenya kwa miezi 6 ni ukoloni wa kiuchumi, pamoja na kwamba mradi huu ni mzuri na nilitamani sana ujengwe Tanzania kama mazungumzo yangefikiwa na masharti hayo magumu kupunguzwa, Lakini Binafsi ningeishangaa Tanzania kukubali mradi ukiwa na masharti hayo mazito.
Tanzania na Uganda zilipendekeza kujadili upya masharti haya lakini Dangote na Nairobi wakahitaji utekelezwaji wa mradi kwa harakati. Na hivyo Tanzania na Uganda zikachagua kuanzisha mradi wake wa kujenga Refinery Tanga kwakutumia mbia mwingine kutoka Asia ya Mbali. Vinginevyo wakenya watakuwa wanapiga makofi kwa jela yeo wenyewe.
Na Yericko Nyerere