Marafiki wa Nape: Kwanini Nape hakutulia?

Marafiki wa Nape: Kwanini Nape hakutulia?

Hlafu ujue jambo moja. Nape alifanya uchunguzi na kujua ni nini hasa kilichotekea ndipo akatoa maamuzi. Yeye Magufuli alitoa maamuzi bila kufanya uchunguzi na kujua undani wa scandal yenyewe ulikuwaje! Hivyo Nape alitumia nafasi yake kama waziri kumsaidia rais kutekeleza majukumu yake!
unahisi vyanzo vya taarifa vya nape ni vingi kuliko vya pombe?
 
Huyu ni kiongozi mkubwa katika nchi na amepitia katika kipindi cha presha

Kwa nini hakutulia??? au kulikuwa na ulazima wa yeye kusema kitu? what if kama Magufuli alikuwa anataka ampe nafasi ingine ya serikalini?

Nyuma ya pazia kuna nini ambacho Nape anahisi kachukiwa sana wakati kitu alichofanya is obvious ilikuwa lazima ajiuzulu yeye , bila hata kuondolewa. Hakukuwa na haja ya Kamati wakati mwisho wa matokeo ya kamati ni kupeleka report kwa Rais ambaye aliishaamua na kusema pale ubungo

Naamini rais sio malaika, wala sio kuwa Nape hana namba ya simu ya Magu kiasi ambacho wangeongea kuhusu hili swala na kupata baraka zake, kufanya jambo kama lile au kuendelea nalo likiwa linakinzana na bosi wako lina maana gani?? (tuache mihemko wengi tuna mabosi hapa)

Namna ya kudeal na lile swala ilikuwa lazima kuwe na kamati? au angebadili methodology? what was the mission behind? tuwaze nje ya box

Nape inaonekana alijua anafanya nini, na alijua outcome ya mission ilikuwa aidha

1. Rais awe kwenye wakati mgumu wa maamuzi
2. au Nape aondoke yeye

mkuu kamuwahi

ila siamini kama kwa level ya Nape hakujua kuwa kuna kitu kinaendelea..(?????) Yes unaweza kuwa hero, unaweza kuwa na malengo mema na mazuri kabisa ( kutimiza wajibu wako) ila kufanikisha kazi yako kwa ufanisi kunahitaji akili pia na approach kufikia lengo

mimi mtu wa chini niliona kabisa Nape anakinzana na rais, yeye hakuona? au yeye anafanya kazi kama msaidizi wa nani? kama sio msaidizi wa rais....naona Logic inagoma kuona kama Nape alikuwa yeye kama yeye na hana affiliation na Magufuli ambaye ni bosi wake

Imani yangu na msimamo wangu, Makonda ataondoka kupitia mahakama kwa sasa, kuvamia clouds was the best opportunity ya kumuweka kwenye majengo ya mahakama....ingemlazimisha rais kumuondoa
Na wewe ungetulia tu si lazima upost.
 
MZEE WA BAO LA MKONO, MZEE WA BUNGE LIVE.
WAKATI WABUNGE WANATOKA BUNGENI KUDAI BUNGE LIVE YEYE ALIKUWA ANAWACHEKA.
NGOJA AONJE MACHUNGU YA HASIYETAKA KOSOLEWA.
 
Magufuli kaumizwa sana na magazeti ya leo kumpa kiki Nape,amekuwa akiumizwa na magazeti yanayomuandika vibaya makonda!Leo kaweka wazi
 
Nape iilkuwa ni lazima angeondoka tu...mmeona wenyewe tone ya rais leo ni wazi alikuwa mmoja wa mawaziri asiowapenda ......,na waliobaki huo ni ujumbe kwako kuwa nao wataondoka tu !!

Ukitazama leo ukawaona breed ya wasomi wetu kama Kabudi na hotuba za kulamba miguu walizozitoa pale basi utajuwa he was dying to be the minister .....na ukiona namna Mwakyembe alivyokuwa anaamrishwa akaendelee kujinajisi basi utasema BORA USIWE MSOMI!!
 
Waberoya,

..JPM ameharibu ku-side na Makonda wakati kashfa yake ina ushahidi mpaka video.

..mimi nilidhani Nape alikuwa anamsaidia JPM kuona ni jinsi gani jumuiya ya wanahabari na wananchi kwa ujumla wanakichukulia kitendo cha Makonda kuvamia studio za clouds tv.

..JPM alipaswa kutulia, kuipokea na kuifanyia kazi ripoti ya Tume iliyoundwa na Nape.
 
Hivi nape aliunda tume ili iweje labda? kwa sababu alishahukumu kabisa kwamba Tasnia imebakwa, sasa hiyo tume ingekuja na majibu tofauti na mtizamo wake angekubali? Yeye alitakiwa kuwa neutral kwanza asubiri majibu ya tume ili achukue hatua au kushauri. Kwa jinsi alivyolishughulikia tatizo inaonesha wazi alikuwa na lake moyoni kabla. Alitumia mihemko badala ya busara,
 
Huyu ni kiongozi mkubwa katika nchi na amepitia katika kipindi cha presha

Kwa nini hakutulia??? au kulikuwa na ulazima wa yeye kusema kitu? what if kama Magufuli alikuwa anataka ampe nafasi ingine ya serikalini?

Nyuma ya pazia kuna nini ambacho Nape anahisi kachukiwa sana wakati kitu alichofanya is obvious ilikuwa lazima ajiuzulu yeye , bila hata kuondolewa. Hakukuwa na haja ya Kamati wakati mwisho wa matokeo ya kamati ni kupeleka report kwa Rais ambaye aliishaamua na kusema pale ubungo

Naamini rais sio malaika, wala sio kuwa Nape hana namba ya simu ya Magu kiasi ambacho wangeongea kuhusu hili swala na kupata baraka zake, kufanya jambo kama lile au kuendelea nalo likiwa linakinzana na bosi wako lina maana gani?? (tuache mihemko wengi tuna mabosi hapa)

Namna ya kudeal na lile swala ilikuwa lazima kuwe na kamati? au angebadili methodology? what was the mission behind? tuwaze nje ya box

Nape inaonekana alijua anafanya nini, na alijua outcome ya mission ilikuwa aidha

1. Rais awe kwenye wakati mgumu wa maamuzi
2. au Nape aondoke yeye

mkuu kamuwahi

ila siamini kama kwa level ya Nape hakujua kuwa kuna kitu kinaendelea..(?????) Yes unaweza kuwa hero, unaweza kuwa na malengo mema na mazuri kabisa ( kutimiza wajibu wako) ila kufanikisha kazi yako kwa ufanisi kunahitaji akili pia na approach kufikia lengo

mimi mtu wa chini niliona kabisa Nape anakinzana na rais, yeye hakuona? au yeye anafanya kazi kama msaidizi wa nani? kama sio msaidizi wa rais....naona Logic inagoma kuona kama Nape alikuwa yeye kama yeye na hana affiliation na Magufuli ambaye ni bosi wake

Imani yangu na msimamo wangu, Makonda ataondoka kupitia mahakama kwa sasa, kuvamia clouds was the best opportunity ya kumuweka kwenye majengo ya mahakama....ingemlazimisha rais kumuondoa
Kwaiyo km bosi anakosea umfuate tu hii n nnchi na ina sheria ndo zinazo muongoza hata Huyo bosi
 
Ishu ya Nape sio bahati mbaya, wamejipanga, anayefuata ni Mwigulu atamkosoa Mkulu hadharani naye atakaa au atawekwa pembeni, atafuatia January Makamba...baadae kuna orodha ya wabunge hasa wa kanda ya ziwa ambao ni Tibaijuka,Kamala,Lugola,Mkono,Ahmed(Solwa),Nchambi,Chegeni,Salum(Meatu),Bukwimba na Musukuma.
 
Nadhani hapa tatizo ni mipaka ya kazi baina ya mkuu na msaidizi wake, alichokifanya Nape kama mwenye wizara ni sahihi lakini pia alichokifanya JPM kubadilisha na kuteua waziri ni sawa pia kwani kilichoangaliwa hapo nani alianza, tayari Rais alishalizungumzia hilo na kusema "huyo mtu wake" afanye kazi na hawezi kufanya kazi kwa maelekezo ya mitandaoni which means pamoja na makosa aliyofanya huyo dogo bado yeye aliona sawa na ndio maana akazidi kumwambia aendelee kufanya kazi (kwa kauli ile maana yake amefunga mjadala).......na kwa Nape kufanya kazi ile kama Waziri ili kujua kiini cha tatizo nae alikuwa yupo sawa tatizo hapo kwa kuwa tayari rais alishalizungumzia hilo ilibidi afanye mawasiliano na mkuu wake kabla ya kwenda frontline (hapo ni protokali za kiuongozi tusiangalie kosa la Makonda ambalo kimsingi lipo wazi tu halina ubishi). Kinachoonekana hapo tayari kuna tofauti katika ku-deal na tatizo alilolifanya Makonda wakati wote wawili ni sehemu ya serikali na kilichotokea ni yule mkubwa kumlamba mkono yule mdogo.
 
Mleta mada umeona mbali sanaaaa....Bravo.
Hizi huwa zinaitwa " calculated moves". Mh Rais anahujumiwa dhahiri,halafu kuna watu wanatetea upuntunyu na kuhemka kwa mambo wasiyoyajua.

Kuna dots ukiweza kuziunganisha utamuelewa Mh Rais na kauli yake aliposema "CCM kuna Wasaliti".
Tatizo letu Watanzania huwa tunapenda kukurupuka na mihemko inayotuvuruga akili na kutuvua busara na UTU pale tunapoletewa jambo geni. Leo hii ikiletwa au ikitengenezwa habari ya "Nyama ya Nguruwe yakutwa ndani ya Msikiti wa Mtoro"...hiyo ndio itakuwa habari ya mjini na haya mengine yote yatasahaulika!

Tujifunze kutafakari na kufikiri nje ya boksi. Kuna mengi tunayajua na mengi hatuyajui....Mh Rais anapelekewa taarifa, sidhani Kama huwa anakurupuka kama Wanaharakati wanavyotaka kuuaminisha UMMA wa Tanzania. Muda ndio utaongea. Tuache kuishi kwa mazoea,tuishi kwa kufuata sheria,taratibu na kanuni za Nchi.

UZALENDO KWANZA VYAMA VYA SIASA BAADAE.
 
Nadhani hapa tatizo ni mipaka ya kazi baina ya mkuu na msaidizi wake, alichokifanya Nape kama mwenye wizara ni sahihi lakini pia alichokifanya JPM kubadilisha na kuteua waziri ni sawa pia kwani kilichoangaliwa hapo nani alianza, tayari Rais alishalizungumzia hilo na kusema "huyo mtu wake" afanye kazi na hawezi kufanya kazi kwa maelekezo ya mitandaoni which means pamoja na makosa aliyofanya huyo dogo bado yeye aliona sawa na ndio maana akazidi kumwambia aendelee kufanya kazi (kwa kauli ile maana yake amefunga mjadala).......na kwa Nape kufanya kazi ile kama Waziri ili kujua kiini cha tatizo nae alikuwa yupo sawa tatizo hapo kwa kuwa tayari rais alishalizungumzia hilo ilibidi afanye mawasiliano na mkuu wake kabla ya kwenda frontline (hapo ni protokali za kiuongozi tusiangalie kosa la Makonda ambalo kimsingi lipo wazi tu halina ubishi). Kinachoonekana hapo tayari kuna tofauti katika ku-deal na tatizo alilolifanya Makonda wakati wote wawili ni sehemu ya serikali na kilichotokea ni yule mkubwa kumlamba mkono yule mdogo.
Umenena vyema mkuu. Naomba unisaidie kujibu Swali hili "NAPE na RAIS wa JMT ni nani mwenye mamlaka katika Taifa hili" !!???
 
Nape sio material yakua Waziri, uwezo wake ni kuwa kiongozi ktka siasa za chama, a full cabinet minister u can't oppose yr boss openly nimchanga sana ktka nafasi ya uwaziri ndomaana laisi ameanza kuweka watu wazima na wenye uzoefu ktka fasi nyeti kama uwaziri nk. bado kuna kama wawili atawapiga chini warudi kwenye chama believe me He Will never trust younger men again imekuwa bonge la mistake ktk utawala wake.
 
Umenena vyema mkuu. Naomba unisaidie kujibu Swali hili "NAPE na RAIS wa JMT ni nani mwenye mamlaka katika Taifa hili" !!???
Mwenye mamlaka ni Rais mkuu, alichofanya Nape kama rais asingekizungumzia basi Nape kwa wakati alikuwa na mamlaka kwa muda ule wa utendaji kazi wa kamati na kuipokea baada ya hapo mamlaka yanabaki kuwa kwa rais baada ya kupokea mapendekezo. All in all mamlaka ni ya Rais kwa ujumla wake
 
Naona bado kuna uwoga katika kutimiza majukuu ya msingi kwa walio wengi na hili ndilo linalopelekea mtumbwi kuingia maji.
 
Back
Top Bottom