Marafiki wa namna hii kaa mbali nao...

Marafiki wa namna hii kaa mbali nao...

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,805
Reaction score
43,230
Habari ya usiku mwingi....

Ni vyema ukikaa mbali nao utaepuka mengi yatayokuletea makwazo, sonono na upweke.

Kaa mbali nao .......

1. Wote wanaokwambia nakupenda pindi wanapokuwa wamekunywa kilevi ila akiwa soba anakuita dada au kaka mpendwa.

2. Wote wanaokwambia wananyege wewe hivo muende mkafanyane pindi wawapo wamekunywa kilevi ila wakiwa soba wanaongea siasa uchumi maisha na elimu tuu.... (to Kasie they are cowards).

3. Wote wanaokufata PM kukwambia wanakupenda kisha wanaomba namba ya simu na uwatumie picha ya taswira yako.

4. Wote wanaokufata PM kukwambia habari za wengine, kuwa makini na utachomjibu maana atatoka na kwenda kuwaambia wengine.

5. Hapa ujitahidi kuwang'amua wote wanaokung'ong'a.... yaani kwenye thread anakusemesha na ID yake ya siku zote halafu PM anakufata na ID mchepuko wengine PM anakufata na ID yake zoefu kisha jukwaani anakuchetua na ID mchepuko hawa jitahidi kuwatambua mapema kabla hawajakuletea sonono na uwaepuke mapemaaa.

6. Wote wanaotaka kukujua undani wako kwa nguvu na haraka na kujifanya wao ni watu wako wa karibu sana ili wakisha kupata wakutangaze kama shilawadu bila kujali hisia zako.

Waepuke mapemaaaa laah ukae nao chonjo kama sungura au panya yaani umelala lakini macho yako wazi na una ng'ata huku unapuliza.

Wako wengi wa kukaa nao mbali ila kwa leo ni hao tuu, waweza ongezea wengine.

Nasema Waepuke Mapemaaaa tenaa

Kaa Mbali Nao.....

Kasinde.
 
Nashukuru Mimi simo kati ya wote mia uliotaja

Sasa unaniweka wapi?

Teh
 
sina usingizi leo .

Kulikoni..... hujaandaa msosi mtamu leo? Ni mpenzi wa kuangalia movie? Weka movie unayoipenda ikiisha macho yamechoka unalala au kama wapenda soma vitabu, chukua kitabu kimoja kitamuu soma walau chapter 2 ukianza kuanzia wahi kitandani ulale.

Polee... ila usisahau kukaa mbali nao..... wotee.
 
Sasa uliyo fanyiwa ww unafikiri wote tutafanyiwa hivyo? Empty Set kabisa

Kaa mbali nao wanaojilinganisha matukio yao na yako ..... ni hatari kwa afya yako, haraka kaa mbali nao.... halafu wengine wa kukaa nao mbali hawaoni kundule wanaona ya wenzao tuu hehehehehee looh.
 
Hao namb 2 nawaogopa

Na wengi wao hawana ujasiri wa kukuangalia usoni wakiwa soba au kukwambia jambo lolote la mzaha au mapenzi. Hadi wavae nyago la pombe usoni ndo. Utawasikia.... lucas wajua kifua chako kinafaa kukumbatiwa muda wote.... waonekana mtundu kwenye mambo ya kikubwa... n.k. n.k. ili akiwa soba ukimjia juu ajitetee ilikuwa pombee nyaambaafff. ..... kaa mbali nao.

Kasinde.
 
Back
Top Bottom