Marafiki mnaishije? Mwenzenu pesa haikai kabisa

Marafiki mnaishije? Mwenzenu pesa haikai kabisa

ongeza sources of income, kwa sababu inavyoonekana una familia kubwa inayokupelekea kufanya matumizi makubwa.Mwambie pia kila mtu uliyenajye ambaye anauwezo wa kuzalisha(Kiuchumi) na azalishe ili kufidia gap ya ukali wa maisha.
"Mkuu kula maharage mwezi mzima afu No Beers"
 
Nashukuru katika hili watu wamechangia vizuri sana..

Inainesha jamaa alioa mke ambaye awali ulikuwa ukitumia mno pesa, lakini kingine inawezekana huyo mke sio mhasibu mzuri... Hebu jaribu kumshirikisha katika shughuli za kimaendeleo uoe atakuambia lipi tusihe kukupa fact za ku budget na ku make more money kumbe tatizo lipo kwenye familia yako, una mke mpenda kuvaa kipya daily mpesa mtoko daily, mpenda makubwa daily, nk nk etc.

Ukifanya hivyo uki mset au mki set ana. Uturejeshee mrejesho
 
Ninacho hisi
1.hakuna ushirikiano kwenye kuchangia matumizi kati yako na mkeo
2.unamuogopa mkeo kumshirikisha kuchangia mahitaji yenu
3.mnaishi maisha ya kuiga wengine si maisha yenu halisi.
USHAURI WANGU
Muelekeze mkeo achangaie japo 25% ya matumizi yenu ili muweze kupiga hatua za kimaendeleo
 
heshima kwenu wadau..

naombeni mnishauri jinsi ya kukabiliana na gharama za maisha..maana naona siendelei kabisa...

ni kijana naishi na mke na mtoto mmoja.. plus mdogo wangu na house girl.

yaani nikitoa zile fixed cost zote kama kodi.. kwa wastani kwa mwezi natumia laki 7 hadi milioni.. hapo ni chakula nyumban na changu ofisin, maji, umeme, kingamuzi, matumiz madogo madogo ya nyumbani na dharura

kila nikijitahidi kupunguza matumizi hayabadiliki..

yaani hela haishikiki kabisa..

wenzangu mnatumia mbinu gani kuishi kwa bajeti nafuu
Bado iko kwenye bajeti mbona jitahidi tu isizidi hapo halafu tafuta vyanzo vipya vya mapato
 
Kama mkeo ni mama wa nyumbani basi mtafutie shughuli ya kufanya
Nyongeza, Pia kama mke ni mama wa nyumbani, hakuna sababu ya kuwa na house girl.

House girl anahiytajika iwapo wote yeye mleta mada na mke wake ni wafanyakazi hivyo wanahitaji mwangalizi wa mtoto na nyumba pindi wawapo kazini.
 
kifupi angalia fursa za mikopo ufanye mradi ambao utakuwa unahudumia gharama za kila siku, ila kusema kupunguza matumuzi how comes hiyo haiwezekani maana koo zetu nyingi ni za wakulima huwezi sema usisaidie ndugu then utakuwa nani sasa.. na huwezi punguza bajeti ya chakula utatesa familia yako, angalia umiliki hata bodaboda hata mbili kwa wiki zinakupa laki 1 , kwa mwezi laki 4 hapo utaona hela inakaa mkuu. pia jiepushe na marafiki wa bata batani
 
mke wangu ni mwalimu wa msingi.. naongelea matumizi ya mwezi mnayapunguza vipi kwa mnaoishi kwa bajeti ndogo
Acha kulipia king'amuzi, tumia local channel kupata habari, hakikisha unakula nyumbani tu acha kula kazini, punguza matumizi ya simu, punguza kununua mavazi, kuwa mkali kidogo kwenye kutoa pesa hata kwa mkeo, acha pombe, mwisho jifunze kununua mahitaji ya nyumbani kwa jumla baada ya kupata pesa yako mwisho wa mwezi.

Kuna watu wanalalamika pesa haikai huku kutwa haipiti bila kunywa pombe, kuhonga wanawake, kushinda baa na clubs za starehe nk. Pesa itakaaje hapo?
 
kifupi angalia fursa za mikopo ufanye mradi ambao utakuwa unahudumia gharama za kila siku, ila kusema kupunguza matumuzi how comes hiyo haiwezekani maana koo zetu nyingi ni za wakulima huwezi sema usisaidie ndugu then utakuwa nani sasa.. na huwezi punguza bajeti ya chakula utatesa familia yako, angalia umiliki hata bodaboda hata mbili kwa wiki zinakupa laki 1 , kwa mwezi laki 4 hapo utaona hela inakaa mkuu. pia jiepushe na marafiki wa bata batani
Mkuu kama wote wa 2 ni watumishi wenye mshahara tena si mdogo wanashindwa kuupangia matumizi vyema WAKIONGEZA NA MKOPO SI NDO WATAJITUMBUKIZA KWENYE TANURI LA MOTO!
 
Nyongeza, Pia kama mke ni mama wa nyumbani, hakuna sababu ya kuwa na house girl.

House girl anahiytajika iwapo wote yeye mleta mada na mke wake ni wafanyakazi hivyo wanahitaji mwangalizi wa mtoto na nyumba pindi wawapo kazini.
Ni kweli kabisa, kama mke ni mama wa nyumbani maana yake ajira yake ipo nyumbani na hakuna sababu ya kuwa na msaidizi...

Sema kizazi cha leo, ataletwa msaidizi huku mke hafanyi chochote, siku jamaa akitetereka kiuchumi mke aweza hata kukimbia.
 
Mkuu kama wote wa 2 ni watumishi wenye mshahara tena si mdogo wanashindwa kuupangia matumizi vyema WAKIONGEZA NA MKOPO SI NDO WATAJITUMBUKIZA KWENYE TANURI LA MOTO!
hao wa hivyo inakuwa ni matumizi makubwa sana ya pesa,
 
duh tena unamke....matumizi yanatoka wapi....ukiwa alone ndio matumizi juu...ukiwa na mke inakuwa less ...au unagawa njepesa zako
 
Back
Top Bottom